Ansbert Ngurumo: Paul Makonda aongoza kikao cha maangamizi ya CHADEMA ambacho ni hatari kwa Taifa

Ansbert Ngurumo: Paul Makonda aongoza kikao cha maangamizi ya CHADEMA ambacho ni hatari kwa Taifa

Kikao cha ulinzi na usalama si vikao vigeni kila Wilaya huongozwa DC. ngazi ya Mkoa ni RC ni vikao muhimu hasa kipindi hiki tunakoelekea sikukuu
Wajumbe wake mkoa wa Dsm ni pamoja na Cyprian Musiba? Kama ni kweli alihudhuria!!
 
Sina sababu ya kutomuamini Ngurumo. Kitu kimoja ambacho ni sharia ya asili, ni kwamba kila penye dhuluma, lazima atatokea mtu au watu ambao hawakubaliani na hali na watatoa taarifa za "siri" Hongera sana Ngurumo, Mungu akulinde na ailinde familia yako. akulipe mara mia kwa kujitoa muhanga, hapa duniani na huko mbinguni
 
Bashite huwa anashinda kutwa TISS tena anafanya na kinyume na taratibu za uingiaji ndani ya ule mjengo lakini watakaomshughulikia wapo humo2 asubiri muda sio mrefu
 
.
1. Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wanajulikana ki-protokali. Je, ktk kikao hicho Musiba alihudhulia kama nani? Na kati ya wajumbe hao, nani ana report kwa Ngurumo? Je, hii inaweza kuwa inathibitisha madai ya Musiba kuwa ndani ya CHADEMA kuna watu wenye vifaa vya kudukua mawasiliano ya viongozi wa serikali?

2. Kama records zangu ziko sawa, ni kama Musiba alifanyia Press Conference yake Dodoma. Waandishi waliohudhuria wanaweza kutuambia hapa kuwa hiyo Press iliisha saa ngapi. Baada ya hapo Musiba alisafiri kwa usafiri gani mpaka akawahi kikao cha saa 9.00 alasiri Dar? Kama alipanda ndege, alijigharimia safari yake hiyo? Kama siyo, nani aligharimia na kwa maslahi yepi?


1. CHADEMA hawajawahi kuficha, hata kwa kauli zao kwamba wana uwezo wa kujua chochote kinachoendelea ndani ya serikali. Hiyo siyo breaking news.

2. Musiba anadai yeye ni mfanyabiashara (ingawa nyie waandishi sijaona mkifanya juhudi kutibitisha biashara zake) na wafanyabiashara pekee wanaoingiaga directly kwenye siasa kwa style yake ya kufanya press conferences nk ni wale wenye uwezo hasa, kina Bloomberg na Koch brothers. Labda mwenzetu ana private jet. Yoyote mwenye akili timamu anajua huyo jamaa ni mouthpiece ya watu fulani. Even the devil can use a yumani fesi sometimes!

PS. Mimi sina mbwa wangu kwenye mapambano haya ila nachukia ushetani.
 
Duh!.
Ngurumo, Ngurumo, Ngurumo...
Hii kali...
Kwanza kwaheri

kisha karibu

Hii ya kwako Ngurumo kali!, yaani wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Dar es Salaam wanaripoti kwako Ngurumo!...
bora umekimbia! maana...

Hata hivyo, kwenye tasnia ya media, hakuna kitu kama MBM, kilichopo ni waandishi wasio ma mipaka, Journalists San Frontiers
P
Paskali,
hayo maswali, maoni na maelezo ulimpa Ngurumo hayawezi ondoa ukweli kwamba kikao kimefanyika (KAMA KIMEFANYIKA) na kwamba kikao hakijafanyika (KAMA HAKIJAFANYIKA). Namaanisha hakubadili kitu..
Iwe kuna MBM au hakuna...
Iwe JSF au hakuna....
Iwe wajumbe wa kamati ya ulinzi wanaripoti kwa kwake au hapana..
Iwe amekimbia au amekimbizwa....
 
Kuna mtu wa ndani kabisa anayempenyezea huyu mambo mazito sana ya kidhalimu yanayopangwa kufanywa dhidi ya Cuna Viongozi wake.

Ushukuriwe sana weye Mtanzania unayejali zaidi maslahi ya Tanzania na kukataa kuona udhalimu unaopangwa ukifanikiwa. Tunakuomba sana uendelee kutuhabarisha kupitia Ansbert Ngurumo. Mwenyezi Mungu awajaalie sana.

Alikuwa Wakwanza kutujuza maazimio ya Kikao kilichoketi (Ukumbi wa BOT) na kuazimia Viongozi wakuu wa CHADEMA wakamatwe wapelekwe mahakamani na kunyimwa dhamana.

Ikatokea exactly sawa na vile alivyoeleza kabla.


Hivyo anafaa kuaminika!
 
Utumbo mtupu huu , nilijua kuna la maana dah , na huyu hana tifauti na yule dada wa marekani nani nani kimav
 
Hutaki au?
Unashangaa nini sasa?
Sio sitaki, bali lazima nishangae, vipi wewe hushangai?,
Watu tumeonyeshwa video Musiba amefanya Press Conference Dodoma jana mchana, mara jana hiyo hiyo anakuja kuhudhuria kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wakati yeye sio mjumbe!, halafu miongoni mwa wajumbe wa kikao hicho, kuna mjumbe mmoja anaripoti kwa Ngurumo!,haya hayakushangazi?!.

P.
 
Sio sitaki, bali lazima nishangae, vipi wewe hushangai?,
Watu tumeonyeshwa video Musiba amefanya Press Conference Dodoma jana mchana, mara jana hiyo hiyo anakuja kuhudhuria kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wakati yeye sio mjumbe!, halafu miongoni mwa wajumbe wa kikao hicho, kuna mjumbe mmoja anaripoti kwa Ngurumo!,haya hayakushangazi?!.

P.
Ndugu yangu Mayalla issue ya kuwepo Dodoma asubuhi na jioni akawepo Dsm hilo linawezekana kabisa maana usafiri upo mwingi wa kutosha tu,juu ya kupata habari nayenyewe siyo issue maana ni kuwa na mtandao wa kutosha tu
 
1. CHADEMA hawajawahi kuficha, hata kwa kauli zao kwamba wana uwezo wa kujua chochote kinachoendelea ndani ya serikali. Hiyo siyo breaking news.

2. Musiba anadai yeye ni mfanyabiashara (ingawa nyie waandishi sijaona mkifanya juhudi kutibitisha biashara zake) na wafanyabiashara pekee wanaoingiaga directly kwenye siasa kwa style yake ya kufanya press conferences nk ni wale wenye uwezo hasa, kina Bloomberg na Koch brothers. Labda mwenzetu ana private jet. Yoyote mwenye akili timamu anajua huyo jamaa ni mouthpiece ya watu fulani. Even the devil can use a yumani fesi sometimes!

PS. Mimi sina mbwa wangu kwenye mapambano haya ila nachukia ushetani.
Umetuelimisha sana mkubwa
 
Ngurumo tunakutegemea sanaa endelea kutupa taarifa juzi ulisema na kweli yakatokea...sema upande wa pili zero brain mambo yanasemwa kabla na bado wanaendelea na mipango yao
 
Ni Ngurumo huyu huyu alisema kuwa Mbiwe na viongozi wengine watakamatwa, kweli walikamatwa.

Ni Ngurumo huyi huyu alisema viongoxi wa CHADEMA watafikishwa mahakamani, kweli walifikishwa mahakamani.

Ni Ngurumonhuyu huyu akisema viongozi wa CHADEMA watashtakiwa kwa kosa la uhaini, wameshtakiwa kwa kosa la uasi.

Ni Ngurumo huyu huyu alusema viongozi wa CHADEMA watanyimwa dhamana, nibkweli walinyimwa dhamana.

Ni lazima niwe mjinga hasa au mpumb.avu kabisa, kuweza kumpuuza mtu kama huyo. Mtu ambaye anatamka kitu kabla hakijatokea, na kikatokea. Siamini kama Ngurumo ni nabii lakini atakuwa na watu ndani ya mfumo ovu wasiopenda uovu, ndio wanaompeleka taarifa zote za uovu dhidi ya Watanzania wasio na hatia.

Mungu azidi kuwabariki watu kama akina Ngurumo au Mange ambao wamejitoa kuwataarifu Watanzania mbinu ovu na chafu zinazopangwa na kufanywa na shetani kwa mikono ya wanadamu.
Vipi na hii ilikuwa kweli. Si ndiyo huyo jamaa na kina Kubenea waliandika hayo. Akili za kuambiwa changanya na zako
 

Attachments

  • FB_IMG_1484944703142.jpg
    FB_IMG_1484944703142.jpg
    23.7 KB · Views: 45
H
Ngurumo tunakutegemea sanaa endelea kutupa taarifa juzi ulisema na kweli yakatokea...sema upande wa pili zero brain mambo yanasemwa kabla na bado wanaendelea na mipango yao
Hahaaaa hata taarifa hii alikupa yeye na majambazi wenzie. Endelea kumuamini na uamini na hili pia
 

Attachments

  • FB_IMG_1484944703142.jpg
    FB_IMG_1484944703142.jpg
    23.7 KB · Views: 40
Hakuna siri tena. Leo tarehe 30:03:2018, saa tisa kamili (9:00) alasiri, saa ambayo Bwana Yesu Kristo alikata roho msalabani, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, katika muda ule ule, Paul Makonda, alikuwa anafungua kikao maalumu cha kupanga mambo maovu dhidi ya viongozi waandamizi wa Chadema na wakosoaji wengine wa serikali. Kikao hicho, ambacho alikiita kikao cha “ulinzi na usalama,” katika ukumbi wa polisi Kurasini, kiliahirishwa saa moja kamili (1:00) usiku.
Katika kikao hicho, yalijadiliwa mambo mengi mazito.

Nimechagua machache tu yafuatayo, ndiyo nitaweka bayana, ili kuonyesha dunia jinsi kiburi, jeuri, sifa na madaraka ya watu wawili (JPM na Makonda) vinavyohatarisha usalama wa taifa letu. Mengine yanafanyiwa kazi na vyombo muhimu.

1. Mbali na Freeman Mbowe na viongozi wenzake walio gerezani Segerea, wengine waliojadiliwa na kikao hiki, ambao watakamatwa muda wowote kuanzia sasa ni wabunge: Godbless Lema (Arusha), Halima Mdee (Kawe), John Heche (Tarime Vijijini), Esther Bulaya (Bunda), Joseph Selasini (Rombo), na kiongozi wa Jumuiya za Kiislamu, Ustadhi Rajab Katimba. Eti hawa ni "majasusi wa Chadema!"

2. Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Bw. Cyprian Musiba, ambaye amekuwa anakutana na waandishi wa habari na kutoa matamko ya shari na tuhuma kali dhidi ya watu wanaokosoa serikali. Alikuwa kikaoni - kikao cha “ulinzi na usalama” mkoa wa Dar es Salaam. Katika moja ya hoja zake, alisema Ansbert Ngurumo anachafua serikali akiwa huko Ulaya; na kwamba ingekuwa vema serikali iweke utaratibu wa kumfuatilia huko aliko na kumdhibiti. Baadhi ya wajumbe walisema hakuna haja, bali serikali ibane hawa hawa waliopo nchini, hasa Heche na Lema. Hasira dhidi ya Lema zilitokana zaidi na kauli yake kutaja Dk. Modestus Kipilimba kwamba anashinikizwa na kushirikishwa katika kupanga mateso dhidi ya wapinzani. Mbali na kusaka fursa ya kumtesa, wanatengeneza “mabomu” dhidi ya mbunge huyo wa Arusha.

3. Wamekerwa na suala la ugonjwa wa Abdallah Mtulia (mbunge wa Kinondoni) kujulikana, wakadai kwamba ugonjwa wake umesababishwa na Chadema. Mtulia ana hali mbaya hospitalini. Makonda na Musiba wamejiapiza kuwa watapambana na Chadema kwa mbinu zote kwa kutumia dola na "uchawi."

4. Kesi ya Mbowe inawapasua kichwa, inawatia hofu (kwa sababu ni ya kubumba); hata mawakili wa serikali wamesema wanalinda hadhi ya taaluma yao, hawataki kuchafuka au kuchafua taaluma zao kwa kesi za kubumba za polisi.

5. Serikali inakerwa mno na taarifa za vikao vyao vya siri kuvuja, na jambo hili linawafanya wachelewe kutekeleza uovu wao wanaopanga dhidi ya Mbowe. Wamesema zamu hii watakuwa makini zaidi.

Yapo mengi, lakini haya ndiyo nimeona vema niyaanike hapa, ili Watanzania na dunia nzima ijue kinachoendelea nyuma ya pazia, wajue aina ya “viongozi” walionao, na wajue nani anahatarisha usalama wa nchi. Hivi ndivyo Bashite na kikosi chake walivyoadhimisha Ijumaa Kuu – kwa kumkejeli Mungu!

MASWALI MAGUMU:
a) Bado Watanzania mnajiuliza nani anamtuma Musiba kufanya press conferences na kutoa matamko ya kushambulia watu kwa tuhuma za ajabu ajabu?
b) Bado mnataka kujua mamlaka inayomlinda Musiba?
c) Idara ya Usalama wa Taifa haijui haya au imenyosha mikono, inafuata maagizo, na imeamua kuacha hatima ya usalama wa nchi hii mikononi mwa watu wawili?
d) Kuna mtu anadhani Makonda anafanya haya kwa hiari yake tu, bila idhini na baraka za Rais Magufuli anayesema maneno ya ajabu dhidi ya wapinzani na wakosoaji wake, hadharani bila aibu, kwamba, “sijaribiwi…. nitawavunja miguu?”
e) Kwa mikakati hii, kwa kuhatarisha badala ya kulinda uhai na usalama wetu, rais anadhani nchi iko salama, na yeye mwenyewe yuko salama?
f) Wakati uovu huu unapangwa rasmi, Rais Magufuli alikuwa kanisani kwenye ibada ya Ijumaa Kuu, “anasali.” Je, naye alibusu msalaba? Kama ndiyo, busu lake lina tofauti gani na busu la Yuda kwa Bwana Yesu – busu la usaliti kwa Watanzania alioapa kuwalinda?
g) Mateso na vifo vya wapinzani na wakosoaji wake ndiyo zawadi ya Pasaka ambayo rais anaandalia Watanzania mwaka huu 2018?
h) Kama utawala wa Kaisari uliangukwa kwa sababu ya kiburi, jeuri na ulevi wa madaraka, utawala wa Magufuli utanusurika vipi ukiwa na sifa zile zile?

Mengine nabaki nayo. Tuendelee kutafakari haya.

Ansbert Ngurumo
MHARIRI BILA MIPAKA (MBM)
I hope you are no longer stupid! Tangu umekimbia kwa vijisababu vya kijinga. Siamini tena unachoandika. Siyo kawaida ya wa-TZ kuamini tunayoandikiwa na walioko nje ya nchi. Ni umbeya! Mtu uliyezeekea nchi hii na ukiwa hata hujui uzuri na ubaya wa nje ya nchi hukustahili kuripuka kwa kuamini huko kuna maisha matamu.
 
kama kweli I'm disappointed in you Makonda,

Dar inahitaji mambo mengi,

kuangamiza upinzani sio mojawapo!
 
Mkuu Mwanahabari huru, kumbe upo?, kwa vile Ngurumo mwenyewe ameishaingia humu mazima in person akiwa ni verified, nakushauri sasa pumzika, acha mwenyewe aje, tubanane nae humu humu.

Ni kweli kuna kitu nimeona hapo sio tuu ni hatari kweli bali kinatisha, sisi ambao hatuna mahali pa kukimbilia, kuna wakati, unapaswa kufunga tuu mdomo na kushangaa, kama mimi ninavyoshangaa kwenye bandiko hili na haswa the authenticity of the story, ikizingatiwa imeripotiwa na mhariri wa kuaminika, ila pia inaweza kabisa kuwa ni concoction kwa sababu hata waandishi wakubwa na wahariri kama kina Salva, na Mtanzania, waliwahi ku concoct na kushuka na concoction kumhusu Dr. Salim Ahmed Salim.

This is something serious, something big, something very dangerous, mpaka sasa mimi bado siamini!.

Tusubiri.

P
nimekupata lakini tumjuavyo mhariri ngurumo sidhani kama anaweza kufanya kosa pengine kunakaukweli wacha tuone
 
Du!, nimeamini wabongo ni wabunifu sana yaani ikitokea Gape wanacheza nalo.
Siku hizi kila mtu anaenda Ulaya anaanza kunganganiza Ugomvi na Serikali ili apate uhakika wa kuishi huko.
Muhimu kumbuka hao Ulaya wanamila zao za hovyo sana. Wewe unaweza ukapona kwakua umelelewa hapa TZ hivyo unayomaadili mema. Lakini ukaangamiza kizazi chako chote kikawa Wake za watu si mwanaume wala Mwanamke wote wanaolewa na waume wenye jinsia yao.
 
Back
Top Bottom