Japo kuna wakati anatumia lugha isiyo ya staha, baada ya kufuatilia kwa muda mrefu, taarifa ambazo Mange Kimangi huzitoa kwenye page yake, kwa kiwango kukubwa, huwa ni ukweli mtupu.
Nadhani sababu ya watu wengi kumfuatilia Mange kwenye Instagram page yake ni kutokana na usahihi wa kile anachopost. Leo hii Mange Kimambi amekuwa ndiyo chanzo cha uhakika cha habari kuliko TBC au chombo kingine chochote cha habari nchini. Na kwa hakika atazidi kupata followers wengi zaidi kila siku ipitayo. Kumsema vibaya Mange wala hakuwezi kumpunguzia followers. Products (habari) anazozitoa ndiyo zinaweza kumoandisha au kumshusha.
Na jinsi serikali inavyozidi kugandamiza uhuru wa vyombo vya habari, ndivyo watu kama Kimange au hata JF itakavyozidi kuwapata members wengi zaidi.
Binadamu hupenda kuwa huru na hupenda kupata taarifa sahihi. Kama taarifa sahihi hazitaweza kupatikana kwenye vyombo rasmi kama TBC, ITV, Clouds, Channel Ten, Mwananchi, Nipashe, Uhuru, Habari Leo, Tanzania Daima, etc. kwa sababu wakitangaza wanafungiwa, watu watatafuta habari kutoka vyanzo vingine visivyo rasmi. Na bahati mbaya huko serikali haina hata nafasi ya kujitetea au kutoa ufafanuzi.
Siyo sahihi kabisa kumdharau Mange Kimambi. Mimi si shabiki wake wala siyo follower wake lakini siwezi kuukwepa ukweli.