Ansbert Ngurumo: Paul Makonda aongoza kikao cha maangamizi ya CHADEMA ambacho ni hatari kwa Taifa

Ansbert Ngurumo: Paul Makonda aongoza kikao cha maangamizi ya CHADEMA ambacho ni hatari kwa Taifa

Ngurumo sio mwanasiasa kaka/dada,na ukae ukijua kupata taarifa ktk utawala uliogawanyika ni rahisi sana kwa sababu sio wote wanaofurahia haya yanayotendeka,watatafuta wasaliti nje ya ccccmm na mwisho watagundua kumbe wasaliti wapo miongomi mwao by then it would be too late...actually ndivyo Mungu anavyofanya kazi it's beyond human control.
Uovu haujawahi kushinda dhidi ya wema not in human history
Kwenye vyombo vya Dola wapo watumishi ambao ni Wapinzani mioyoni mwao na wengine hawana mapenzi na vyama lakini wana huruma hawapendi Udikteta wa Naibu Rais Maliyamungu Bashite na Mtukufu malaika toka chato, hao wana ndugu zao, Rafiki zao chadema huwaletea taarifa zote za vikao vya kudhoofisha na kuua upinzani kwa ujumla, hakuna siri kwani huko napo wamegawanyika wengi hawapendi jinsi Nchi inavyoendeshwa kibabe kwa Uonevu na unyanyasaji mwingi
 
Musiba ni mjumbe wa kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa wa Dar? We have some very hopeless people with hopeless minds. No doubt you are among them.
Mwenyekiti hawezi kuamua kukualika hata wewe kwenye kikao hicho kama anaona unaweza kuongeza value ktk ulinzi wa eneo lake?

Vv
 
na hukiona habari zinavuja basi ujue kuwa waliomo ndani ya kikao hawaridhishwi na uovu huo ila wana.kokotwa tu,
Ndivyo ilivyokuwa siku zote pia kuna udhaifu mwingine kwenye kikundi cha Naibu Rais Maliyamungu Bashite ambapo Le mutuz akilewa na akalala na mchepuko hutoa siri zote na wengi wamepata siri za Maliyamungu Bashite baada ya kupandikiza wanawake kwa Le mutuz na Jerry muro ambao ni wadhaifu kwa wanawake sana.
 
Alikuwa Wakwanza kutujuza maazimio ya Kikao kilichoketi (Ukumbi wa BOT) na kuazimia Viongozi wakuu wa CHADEMA wakamatwe wapelekwe mahakamani na kunyimwa dhamana.

Ikatokea exactly sawa na vile alivyoeleza kabla.


Hivyo anafaa kuaminika!
Bro... Ww ni great thinker
 
Musiba anatuhumu, ngurumo anatuhumu. Mambo wanayoongea yamekaa kimachafuko machafuko tu. Haijalishi nani mkweli nani muongo, Ila Kwa sababu hali inaachwa hivi na haidhibitiwi wala kusuluhishwa na vyombo husika naamini Kuna kitu tunakitafuta kwa nguvu sana tu. Tunahamu ya kuonja kitu ambacho hatujui kama ndimi zetu zitahimili ladha yake au la. Huu udhaifu unaoonekana unatakiwa udhibitiwe.
Kuna cha kujiuliza hapo: hivi kauli za Musiba na za gazeti la Jamvi la habari zingetolewa na gazeti ambalo sio Uhuru, Daily News au Habari Leo, Serikali kupitia Waziri Mwakyembe au Msemaji wake Dr. Abbas ingekuwa kimya hadi leo kweli? Bado huoni Kuna hoja hapo?

Vv
 
Hakuna siri tena. Leo tarehe 30:03:2018, saa tisa kamili (9:00) alasiri, saa ambayo Bwana Yesu Kristo alikata roho msalabani, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, katika muda ule ule, Paul Makonda, alikuwa anafungua kikao maalumu cha kupanga mambo maovu dhidi ya viongozi waandamizi wa Chadema na wakosoaji wengine wa serikali. Kikao hicho, ambacho alikiita kikao cha “ulinzi na usalama,” katika ukumbi wa polisi Kurasini, kiliahirishwa saa moja kamili (1:00) usiku.
Katika kikao hicho, yalijadiliwa mambo mengi mazito.

Nimechagua machache tu yafuatayo, ndiyo nitaweka bayana, ili kuonyesha dunia jinsi kiburi, jeuri, sifa na madaraka ya watu wawili (JPM na Makonda) vinavyohatarisha usalama wa taifa letu. Mengine yanafanyiwa kazi na vyombo muhimu.

1. Mbali na Freeman Mbowe na viongozi wenzake walio gerezani Segerea, wengine waliojadiliwa na kikao hiki, ambao watakamatwa muda wowote kuanzia sasa ni wabunge: Godbless Lema (Arusha), Halima Mdee (Kawe), John Heche (Tarime Vijijini), Esther Bulaya (Bunda), Joseph Selasini (Rombo), na kiongozi wa Jumuiya za Kiislamu, Ustadhi Rajab Katimba. Eti hawa ni "majasusi wa Chadema!"

2. Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Bw. Cyprian Musiba, ambaye amekuwa anakutana na waandishi wa habari na kutoa matamko ya shari na tuhuma kali dhidi ya watu wanaokosoa serikali. Alikuwa kikaoni - kikao cha “ulinzi na usalama” mkoa wa Dar es Salaam. Katika moja ya hoja zake, alisema Ansbert Ngurumo anachafua serikali akiwa huko Ulaya; na kwamba ingekuwa vema serikali iweke utaratibu wa kumfuatilia huko aliko na kumdhibiti. Baadhi ya wajumbe walisema hakuna haja, bali serikali ibane hawa hawa waliopo nchini, hasa Heche na Lema. Hasira dhidi ya Lema zilitokana zaidi na kauli yake kutaja Dk. Modestus Kipilimba kwamba anashinikizwa na kushirikishwa katika kupanga mateso dhidi ya wapinzani. Mbali na kusaka fursa ya kumtesa, wanatengeneza “mabomu” dhidi ya mbunge huyo wa Arusha.

3. Wamekerwa na suala la ugonjwa wa Abdallah Mtulia (mbunge wa Kinondoni) kujulikana, wakadai kwamba ugonjwa wake umesababishwa na Chadema. Mtulia ana hali mbaya hospitalini. Makonda na Musiba wamejiapiza kuwa watapambana na Chadema kwa mbinu zote kwa kutumia dola na "uchawi."

4. Kesi ya Mbowe inawapasua kichwa, inawatia hofu (kwa sababu ni ya kubumba); hata mawakili wa serikali wamesema wanalinda hadhi ya taaluma yao, hawataki kuchafuka au kuchafua taaluma zao kwa kesi za kubumba za polisi.

5. Serikali inakerwa mno na taarifa za vikao vyao vya siri kuvuja, na jambo hili linawafanya wachelewe kutekeleza uovu wao wanaopanga dhidi ya Mbowe. Wamesema zamu hii watakuwa makini zaidi.

Yapo mengi, lakini haya ndiyo nimeona vema niyaanike hapa, ili Watanzania na dunia nzima ijue kinachoendelea nyuma ya pazia, wajue aina ya “viongozi” walionao, na wajue nani anahatarisha usalama wa nchi. Hivi ndivyo Bashite na kikosi chake walivyoadhimisha Ijumaa Kuu – kwa kumkejeli Mungu!

MASWALI MAGUMU:
a) Bado Watanzania mnajiuliza nani anamtuma Musiba kufanya press conferences na kutoa matamko ya kushambulia watu kwa tuhuma za ajabu ajabu?
b) Bado mnataka kujua mamlaka inayomlinda Musiba?
c) Idara ya Usalama wa Taifa haijui haya au imenyosha mikono, inafuata maagizo, na imeamua kuacha hatima ya usalama wa nchi hii mikononi mwa watu wawili?
d) Kuna mtu anadhani Makonda anafanya haya kwa hiari yake tu, bila idhini na baraka za Rais Magufuli anayesema maneno ya ajabu dhidi ya wapinzani na wakosoaji wake, hadharani bila aibu, kwamba, “sijaribiwi…. nitawavunja miguu?”
e) Kwa mikakati hii, kwa kuhatarisha badala ya kulinda uhai na usalama wetu, rais anadhani nchi iko salama, na yeye mwenyewe yuko salama?
f) Wakati uovu huu unapangwa rasmi, Rais Magufuli alikuwa kanisani kwenye ibada ya Ijumaa Kuu, “anasali.” Je, naye alibusu msalaba? Kama ndiyo, busu lake lina tofauti gani na busu la Yuda kwa Bwana Yesu – busu la usaliti kwa Watanzania alioapa kuwalinda?
g) Mateso na vifo vya wapinzani na wakosoaji wake ndiyo zawadi ya Pasaka ambayo rais anaandalia Watanzania mwaka huu 2018?
h) Kama utawala wa Kaisari uliangukwa kwa sababu ya kiburi, jeuri na ulevi wa madaraka, utawala wa Magufuli utanusurika vipi ukiwa na sifa zile zile?

Mengine nabaki nayo. Tuendelee kutafakari haya.

Ansbert Ngurumo
MHARIRI BILA MIPAKA (MBM)
Mnafanya maovu makusudi huku mkijua hatima yake.....mnageuka manabii...mnajitabiria!tumeshawabaini!endeleeni kutumika
 
Inamaana amezipata hizi taarifa akiwa huko ugaibuni? Kama ni hivyo sasa nihatari,nani amemfikishia taarifa za kikao hicho? Kwa kifupi kuna uvujaji mwingi sana wa taarifa kama ni hivyo,haiwezekani mtu yuko ugaibuni akaqeza kudukua siri za vikao hapa kwetuu
Hakuna kitu kama hicho wewe! Hana cha kufanya huko na akikaa kimya mtamsahau. Umeusahau msemo wa "An idle's mind is a devil's house"?
 
Duh!.
Ngurumo, Ngurumo, Ngurumo...
Hii ya Ngurumo kali!, yaani wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wanaripoti kwa Ngurumo!...
bora umekimbia! maana...

Hata hivyo, kwenye tasnia ya media, hakuna kitu kama MBM, kilichopo ni waandishi wasio ma mipaka, Journalists San Frontiers
P
Nakumbuka kauli ya Dr.Slaa ya nchi imegawanyika.Ikulu imegawanyika,usalama wa Taifa umegawanyika,Polisi wamegawanyika.Na mimi naongeza HATA CCM WENYEWE WAMEGAWANYIKA.

Kwa msingi huo, Ngurumo atapata taarifa zote za UOVU toka kwa watu wema ili KULINUSURU TAIFA LISIANGAMIE.
 
Mnafanya maovu makusudi huku mkijua hatima yake.....mnageuka manabii...mnajitabiria!tumeshawabaini!endeleeni kutumika
CCM sasa ni mwendo wa piga Risasi, bambikia kesi, funga jela poteza na wazushie chochote chadema kupitia Msiba na wenzake ni hatari kwa kweli, CCM ndiyo chanzo cha uharibu wa Amani ya Nchi endapo hawataacha Udikteta wanaoendelea kuukuza kwa kasi.
 
Ansbert Ngurumo unaweza ukawa na ' Hoja ' kwa mambo mengine yanayoendelea na kama ujuavyo Mimi GENTAMYCINE huwa nasimama katikati na nachukia pia ' Unafiki ' hivyo naomba niseme Kwako kwamba hakuna hata chembe moja ya ukweli juu ya hiki ulichokiandika hapa na kuna hatari zaidi ya Wewe sasa kutoaminika tena na tuliokuwa tunaanza kukuamini kama nawe utaanza ' Kupika ' hizi so called ' classified information ' zako ili tu kutaka kuwateka Watu waanze kukuamini hata Mimi GENTAMYCINE sasa nitaanza Kukudharau na Kukupuuza kwa Kiwango kikubwa tu.

Ushauri wangu mzuri tu Kwako ni kwamba kwakuwa sasa uko huko ' Ng'ambo ' hebu jaribu kutumia ' Kipaji ' chako cha Uandishi wa Habari na Uhariri ili uweze kupata Ajira ambayo itakuwezesha kuendesha maisha yako na hatimaye uachane na kuwa ' tegemezi ' kwa hao wanakukarimu hapo na pia Pesa / Hela zingine uweze kutuma Kwenu ( namaanisha huku Tanzania ) ziweze kuwasaidia Ndugu zako ambao naamini wanahitaji mno msaada wako.

Ni kweli yapo mambo ambayo yanaudhi kwa sasa Tanzania ila ' Mwenzetu ' sasa umezidisha katika Kutudanganya.

Kila la Kheri Kaka.
Lakini hata habari za kukamatwa kwa kina Mbowe na kufunguliwa kesi ya uhaini ambayo DPP kwa makusudi au bahati mvaya ( baada ya Ngurumo kum-pre empty aliamua kuweka neno UASI ) wengi walichukulia poa kama hivi, ilipotokea wengi wakakaa kimya kwa aibu.

Vv
 
Lakini hata habari za kukamatwa kwa kina Mbowe na kufunguliwa kesi ya uhaini ambayo DPP kwa makusudi au bahati mvaya ( baada ya Ngurumo kum-pre empty aliamua kuweka neno UASI ) wengi walichukulia poa kama hivi, ilipotokea wengi wakakaa kimya kwa aibu.

Vv
Vikao vyote vya CCM kuna watu wanaleta taarifa chadema kwani hawapendezewi na unyama wanaotendewa watanzania wenzao.
 
Ansbert Ngurumo unaweza ukawa na ' Hoja ' kwa mambo mengine yanayoendelea na kama ujuavyo Mimi GENTAMYCINE huwa nasimama katikati na nachukia pia ' Unafiki ' hivyo naomba niseme Kwako kwamba hakuna hata chembe moja ya ukweli juu ya hiki ulichokiandika hapa na kuna hatari zaidi ya Wewe sasa kutoaminika tena na tuliokuwa tunaanza kukuamini kama nawe utaanza ' Kupika ' hizi so called ' classified information ' zako ili tu kutaka kuwateka Watu waanze kukuamini hata Mimi GENTAMYCINE sasa nitaanza Kukudharau na Kukupuuza kwa Kiwango kikubwa tu.

Ushauri wangu mzuri tu Kwako ni kwamba kwakuwa sasa uko huko ' Ng'ambo ' hebu jaribu kutumia ' Kipaji ' chako cha Uandishi wa Habari na Uhariri ili uweze kupata Ajira ambayo itakuwezesha kuendesha maisha yako na hatimaye uachane na kuwa ' tegemezi ' kwa hao wanakukarimu hapo na pia Pesa / Hela zingine uweze kutuma Kwenu ( namaanisha huku Tanzania ) ziweze kuwasaidia Ndugu zako ambao naamini wanahitaji mno msaada wako.

Ni kweli yapo mambo ambayo yanaudhi kwa sasa Tanzania ila ' Mwenzetu ' sasa umezidisha katika Kutudanganya.

Kila la Kheri Kaka.
Nadhani ni vema ukangojea na kuona yaliyosemwa yatatokea??? Cdhani kama huu ni wakat wa kumpinga kwakuwa tayari alituambia kuhusiana na maazimio ya kikao cha BOT na kweli yakatimia.. Let's wait and see my brother
 
Back
Top Bottom