Ansbert Ngurumo: Paul Makonda aongoza kikao cha maangamizi ya CHADEMA ambacho ni hatari kwa Taifa

Ansbert Ngurumo: Paul Makonda aongoza kikao cha maangamizi ya CHADEMA ambacho ni hatari kwa Taifa

Hakuna siri tena. Leo tarehe 30:03:2018, saa tisa kamili (9:00) alasiri, saa ambayo Bwana Yesu Kristo alikata roho msalabani, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, katika muda ule ule, Paul Makonda, alikuwa anafungua kikao maalumu cha kupanga mambo maovu dhidi ya viongozi waandamizi wa Chadema na wakosoaji wengine wa serikali. Kikao hicho, ambacho alikiita kikao cha “ulinzi na usalama,” katika ukumbi wa polisi Kurasini, kiliahirishwa saa moja kamili (1:00) usiku.
Katika kikao hicho, yalijadiliwa mambo mengi mazito.

Nimechagua machache tu yafuatayo, ndiyo nitaweka bayana, ili kuonyesha dunia jinsi kiburi, jeuri, sifa na madaraka ya watu wawili (JPM na Makonda) vinavyohatarisha usalama wa taifa letu. Mengine yanafanyiwa kazi na vyombo muhimu.

1. Mbali na Freeman Mbowe na viongozi wenzake walio gerezani Segerea, wengine waliojadiliwa na kikao hiki, ambao watakamatwa muda wowote kuanzia sasa ni wabunge: Godbless Lema (Arusha), Halima Mdee (Kawe), John Heche (Tarime Vijijini), Esther Bulaya (Bunda), Joseph Selasini (Rombo), na kiongozi wa Jumuiya za Kiislamu, Ustadhi Rajab Katimba. Eti hawa ni "majasusi wa Chadema!"

2. Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Bw. Cyprian Musiba, ambaye amekuwa anakutana na waandishi wa habari na kutoa matamko ya shari na tuhuma kali dhidi ya watu wanaokosoa serikali. Alikuwa kikaoni - kikao cha “ulinzi na usalama” mkoa wa Dar es Salaam. Katika moja ya hoja zake, alisema Ansbert Ngurumo anachafua serikali akiwa huko Ulaya; na kwamba ingekuwa vema serikali iweke utaratibu wa kumfuatilia huko aliko na kumdhibiti. Baadhi ya wajumbe walisema hakuna haja, bali serikali ibane hawa hawa waliopo nchini, hasa Heche na Lema. Hasira dhidi ya Lema zilitokana zaidi na kauli yake kutaja Dk. Modestus Kipilimba kwamba anashinikizwa na kushirikishwa katika kupanga mateso dhidi ya wapinzani. Mbali na kusaka fursa ya kumtesa, wanatengeneza “mabomu” dhidi ya mbunge huyo wa Arusha.

3. Wamekerwa na suala la ugonjwa wa Abdallah Mtulia (mbunge wa Kinondoni) kujulikana, wakadai kwamba ugonjwa wake umesababishwa na Chadema. Mtulia ana hali mbaya hospitalini. Makonda na Musiba wamejiapiza kuwa watapambana na Chadema kwa mbinu zote kwa kutumia dola na "uchawi."

4. Kesi ya Mbowe inawapasua kichwa, inawatia hofu (kwa sababu ni ya kubumba); hata mawakili wa serikali wamesema wanalinda hadhi ya taaluma yao, hawataki kuchafuka au kuchafua taaluma zao kwa kesi za kubumba za polisi.

5. Serikali inakerwa mno na taarifa za vikao vyao vya siri kuvuja, na jambo hili linawafanya wachelewe kutekeleza uovu wao wanaopanga dhidi ya Mbowe. Wamesema zamu hii watakuwa makini zaidi.

Yapo mengi, lakini haya ndiyo nimeona vema niyaanike hapa, ili Watanzania na dunia nzima ijue kinachoendelea nyuma ya pazia, wajue aina ya “viongozi” walionao, na wajue nani anahatarisha usalama wa nchi. Hivi ndivyo Bashite na kikosi chake walivyoadhimisha Ijumaa Kuu – kwa kumkejeli Mungu!

MASWALI MAGUMU:
a) Bado Watanzania mnajiuliza nani anamtuma Musiba kufanya press conferences na kutoa matamko ya kushambulia watu kwa tuhuma za ajabu ajabu?
b) Bado mnataka kujua mamlaka inayomlinda Musiba?
c) Idara ya Usalama wa Taifa haijui haya au imenyosha mikono, inafuata maagizo, na imeamua kuacha hatima ya usalama wa nchi hii mikononi mwa watu wawili?
d) Kuna mtu anadhani Makonda anafanya haya kwa hiari yake tu, bila idhini na baraka za Rais Magufuli anayesema maneno ya ajabu dhidi ya wapinzani na wakosoaji wake, hadharani bila aibu, kwamba, “sijaribiwi…. nitawavunja miguu?”
e) Kwa mikakati hii, kwa kuhatarisha badala ya kulinda uhai na usalama wetu, rais anadhani nchi iko salama, na yeye mwenyewe yuko salama?
f) Wakati uovu huu unapangwa rasmi, Rais Magufuli alikuwa kanisani kwenye ibada ya Ijumaa Kuu, “anasali.” Je, naye alibusu msalaba? Kama ndiyo, busu lake lina tofauti gani na busu la Yuda kwa Bwana Yesu – busu la usaliti kwa Watanzania alioapa kuwalinda?
g) Mateso na vifo vya wapinzani na wakosoaji wake ndiyo zawadi ya Pasaka ambayo rais anaandalia Watanzania mwaka huu 2018?
h) Kama utawala wa Kaisari uliangukwa kwa sababu ya kiburi, jeuri na ulevi wa madaraka, utawala wa Magufuli utanusurika vipi ukiwa na sifa zile zile?

Mengine nabaki nayo. Tuendelee kutafakari haya.

Ansbert Ngurumo
MHARIRI BILA MIPAKA (MBM)
Gurumo isee Mhaya bure kabisa hivi wafinish walitoaje hadhi ya ukimbizi kwa mtu Kama huyu. Mambo mengine ni chuki binafsi.
Ila hapa kilinichonifurahisha ni kuwa chadema sasa wanaanza kujishuku wenyewe na kutoa Siri zao wenyewe niombe Vyombo vya dola nendeni nao taratibu mwisho wa siku vyote vitakuwa wazi bila kutumia nguvu nyingi. Tumeanza kusikia Mabomu ya Lema tumesikia Ustaadh Katimba na bado mpk mfike kwenye kikundi cha Tume
 
Ebu kemea uasi wa viongozi waCHADEMA kwanza ndio hilo lako liwe na uhalali.
Kemea Udikteta wa Naibu Rais Maliyamungu idd Amin Bashite kwanza ndipo ujue na hizo Propaganda zenu za kolomije na chato
 
Duh!.
Ngurumo, Ngurumo, Ngurumo...
Hii ya Ngurumo kali!, yaani wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wanaripoti kwa Ngurumo!...
bora umekimbia! maana...

Hata hivyo, kwenye tasnia ya media, hakuna kitu kama MBM, kilichopo ni waandishi wasio ma mipaka, Journalists San Frontiers
P
Acha kukariri sio kila kitu mpaka uanzishiwe ,walioanzisha Journalists San Frontiers ni watu....na yeye kaanzisha MBM as brilliant creative
 
Sijawai kusikia Raia kuingia Kamati ya ulinzi na Usalama wa ngazi yoyote Kama siyo Mjumbe hii ya Leo kusikia Syprian Musiba kuingia huko duh hii Kali uongo mwingine wadanganyeni Majinga Wenzenu
 
Acha kukariri sio kila kitu mpaka uanzishiwe ,walioanzisha Journalists San Frontiers ni watu....na yeye kaanzisha MBM as brilliant creative
Katafsiri tu toka kifaransa kwenda kiswahili hamna creativity yoyote
 
Huyu Ngurumo kumbe ni wa hovyo hivi. Yaani ukisoma hii thread utajua ni hadithi za kubumba na za kijinga
 
Duh!.
Ngurumo, Ngurumo, Ngurumo...
Hii ya Ngurumo kali!, yaani wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wanaripoti kwa Ngurumo!...
bora umekimbia! maana...

Hata hivyo, kwenye tasnia ya media, hakuna kitu kama MBM, kilichopo ni waandishi wasio ma mipaka, Journalists San Frontiers
P
We nae naona unahitaji ugodwin gondwe endelea lakini mwisho wa ubaya ni aibu na dhiki
 
Pia usipuuze shutuma za Musiba na uzito wa maneno ya viongozi, maana kuna mambo mengi yenye harufu kali ya uhaini na uasi,
Msiba yafaa atandikwe makofi na mitaani live maana kawa punguani kiasi cha kutisha, adhabu yake ni kuchezea kichapo live maana mahakamaccm ni vigumu chadema kupata haki hata wakimfungulia kesi.
 
Serikali ndio ilitakiwa kuchukua hatua ila iko kimya sasa kwanini na sisi tusimpuuze?
Una ushahidi kwamba Serikali hajachukua hatua? Je, unasemaje kuhusu uzushi wa Mwanahabari Huru na bandiko lake tunalojadili?
 
Duh wazee kumbe wapo nilifikri wamebaki wanaume wa Dar tu! Sumbawanga miti yote imekatwa kutengeneza mkaa sasa ukombozi unatoka kwa wazee wa toka CONGO
Wapiga kura wa Kinondon walioibiwa kura zao walipiga magoti na kumlilia Mungu
 
Msiba akitunga Uongo dhidi ya chadema yy hasitahili drip? au mnataka Msiba, Jerry muro na Le mutuz wapewe mimba na chadema?
Msiba yuko Tanzania namhurumia huyo Ngurumo aliye Finland akilaghai wazungu kwa utapeli wa kihaya
 
Wenye akili tumeshamshtukia zaidi, anajenga mazingira ya kupata hifadhi ya kudumu ya ukimbizi kwa kuichokoza serikali kwa kuandika habari za uzushi.
Ni wazi akiandika habari za kizushi, serikali itamtafuta na yeye atatumia hilo gepu kudai anatafutwa, ila wa nchi za magharibi sio wajinga kama anavyodhani.
Wataendelea tu kumuhifadhi tena hifadhi ya kudumu kwa justification za kwanza hata asipoandika kitu,uyo hamumpati na amegeuka MBM au Mange Kimambi2,watazaliwa wengi tu
 
Sijawai kusikia Raia kuingia Kamati ya ulinzi na Usalama wa ngazi yoyote Kama siyo Mjumbe hii ya Leo kusikia Syprian Musiba kuingia huko duh hii Kali uongo mwingine wadanganyeni Majinga Wenzenu
Wewe mbona ndiyo fala mjinga unaamini Uzushi wa Msiba? Kama unaweza kuamini Propaganda za msiba kaa uamini kuwa hata Le mutuz, Jerry muro na Heri Kisanduku makapero huingia kwenye hivyo vikao kwani si vikao vya Aman ni vikao vya kuua upinzani na kurejesha mfumo wa chama kimoja.
 
Duh!.
Ngurumo, Ngurumo, Ngurumo...
Hii ya Ngurumo kali!, yaani wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wanaripoti kwa Ngurumo!...
bora umekimbia! maana...

Hata hivyo, kwenye tasnia ya media, hakuna kitu kama MBM, kilichopo ni waandishi wasio ma mipaka, Journalists San Frontiers
P
With all due respect kaka Pascal, nadhani sote mimi na wewe hatujui chanzo cha taarifa cha ndg. Ngurumo,kwahiyo sidhani kama ni busara Ku "rubbish" andiko lake.Busara ilikuwa ni kwa wewe kujenga hoja fikirishi zitazoweza kuleta ushawishi kwamba hili andiko la ndg. Ngurumo halina any substance ya truth ndani yake Bali ni ukurupukaji na upuuzi.Kwa taaluma yako na heshima uliyonayo katika jamii,sidhani kama umejitendea haki kwa kutoa majibu kwa tuhuma nzito namna hii,pasipo kuweka hoja pingamizi.
 
Msiba yuko Tanzania namhurumia huyo Ngurumo aliye Finland akilaghai wazungu kwa utapeli wa kihaya
Msiba akitengeza Uzushi wa kishamba shamba toka kolomije na chato unauamini lakini Ngurumo anayesema Ukweli umeamua kumuita tapela na muhaya, ama kweli huyo Maliyamungu idd Amin Bashite kawalisha Limbwata mmejitoa fahamu zote bila Aibu na kuwadharau Watanzania mkidhani hawajui kutafakari ujinga wenu.
 
Ngurumo alichobakiza ni kusajiliwa MODERN TAARAB,

Maana kwa uongo huu na propaganda za miaka ya 1940s anazileta Leo

Yaani ngurumo ana taarifa za kiinterejensia ambazo hata kipilimba na Magufuli hana

Hawa wana siasa sijui huwa wanatuoanaje Watanzania?
Ngurumo sio mwanasiasa kaka/dada,na ukae ukijua kupata taarifa ktk utawala uliogawanyika ni rahisi sana kwa sababu sio wote wanaofurahia haya yanayotendeka,watatafuta wasaliti nje ya ccccmm na mwisho watagundua kumbe wasaliti wapo miongomi mwao by then it would be too late...actually ndivyo Mungu anavyofanya kazi it's beyond human control.
Uovu haujawahi kushinda dhidi ya wema not in human history
 
Kemea Udikteta wa Naibu Rais Maliyamungu idd Amin Bashite kwanza ndipo ujue na hizo Propaganda zenu za kolomije na chato
Ninachowasifia wapenzi, wanazi na wafuasi wa Mh Mbowe, humu jamvini, ni mawazo yao ya ndani ya kisanduku.

Mnastahili hongera kwa kuwa nyuma ya kiongozi wenu iwe mvua au jua kali. Lakini, sijui kama mnajua maneno yenu ni kama kutwanga maji kwenye kinu!

Kama mlivyo ninyi kwenye mitandao ya kijamii na uzushi na vimaneno ambavyo, bila kujijua, yamewapa kiburi viongozi wenu, zamu yai sasa wako rumande. Na kama watahamasisha maandamano, itakuwa zamu yenu kuwa huko.

BINADAMU NI:
KUHESHIMIANA;
KUKUBALI KUTOFAUTIANA KISTAARABU;
KUTUMIA NJIA ZILIZO HALALI KUBADILISHA UONGOZI; NA
KUSAMEHEANA.
 
Back
Top Bottom