Kwa msisi yetu
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 844
- 1,450
chai 100%
Huu uzi mtam sana utawaingia tu maana mnaombea ufutwe humu jf wapo mods wanaojitambuaJamaa kaishiwa. Jana kauleta huu udaku, leo tena vile vile. Si ajabu akaurudia tena kesho na kesho kutwa.
Mwanahabari Huru, unajua madhara ya kutoa habari kama hiyo, au hujui? Ukikamatwa kuthibitisha nawe utasema haki na uhuru wako umeingiliwa?umeletwa wapi?
wenye uwezo wa kutafakari wanajua kwanini umekimbilia hapa na kuleta uharo wako fasta fasta.Duh!.
Ngurumo, Ngurumo, Ngurumo...
Hii ya Ngurumo kali!, yaani wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wanaripoti kwa Ngurumo!...
bora umekimbia! maana...
Hata hivyo, kwenye tasnia ya media, hakuna kitu kama MBM, kilichopo ni waandishi wasio ma mipaka, Journalists San Frontiers
P
Hoja gani iko katika bandiko hilo zaidi ya uzushi? Hata kama ni ukweli, je, ni taarifa ya kujadili?Mods tafadhali msiunge hii thread na nyingine. Hata kama ikija order kutoka juu.
Naona mnakiuka hadi kanuni zenu.
Mnatunyima Uhuru wa kujadiliana hoja mpya
Uzi mtam sana hiu wacha uendelee tu umeshagonga sehem nyeti [emoji108] [emoji196]Wenye akili tumeshamshtukia zaidi, anajenga mazingira ya kupata hifadhi ya kudumu ya ukimbizi kwa kuichokoza serikali kwa kuandika habari za uzushi.
Ni wazi akiandika habari za kizushi, serikali itamtafuta na yeye atatumia hilo gepu kudai anatafutwa, ila wa nchi za magharibi sio wajinga kama anavyodhani.
Mwanahabari Huru naona sasa umebobea kuleta taarifa za uchochezi hapa JF na Moderator wamekuacha tu!! Sina uhakika kama unaweza kutudhibitishia taarifa hii kama ni ya kweli kwa kuwa wewe ndiyo unaisambaza!!Hakuna siri tena. Leo tarehe 30:03:2018, saa tisa kamili (9:00) alasiri, saa ambayo Bwana Yesu Kristo alikata roho msalabani, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, katika muda ule ule, Paul Makonda, alikuwa anafungua kikao maalumu cha kupanga mambo maovu dhidi ya viongozi waandamizi wa Chadema na wakosoaji wengine wa serikali. Kikao hicho, ambacho alikiita kikao cha “ulinzi na usalama,” katika ukumbi wa polisi Kurasini, kiliahirishwa saa moja kamili (1:00) usiku.
Katika kikao hicho, yalijadiliwa mambo mengi mazito.
Nimechagua machache tu yafuatayo, ndiyo nitaweka bayana, ili kuonyesha dunia jinsi kiburi, jeuri, sifa na madaraka ya watu wawili (JPM na Makonda) vinavyohatarisha usalama wa taifa letu. Mengine yanafanyiwa kazi na vyombo muhimu.
1. Mbali na Freeman Mbowe na viongozi wenzake walio gerezani Segerea, wengine waliojadiliwa na kikao hiki, ambao watakamatwa muda wowote kuanzia sasa ni wabunge: Godbless Lema (Arusha), Halima Mdee (Kawe), John Heche (Tarime Vijijini), Esther Bulaya (Bunda), Joseph Selasini (Rombo), na kiongozi wa Jumuiya za Kiislamu, Ustadhi Rajab Katimba. Eti hawa ni "majasusi wa Chadema!"
2. Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Bw. Cyprian Musiba, ambaye amekuwa anakutana na waandishi wa habari na kutoa matamko ya shari na tuhuma kali dhidi ya watu wanaokosoa serikali. Alikuwa kikaoni - kikao cha “ulinzi na usalama” mkoa wa Dar es Salaam. Katika moja ya hoja zake, alisema Ansbert Ngurumo anachafua serikali akiwa huko Ulaya; na kwamba ingekuwa vema serikali iweke utaratibu wa kumfuatilia huko aliko na kumdhibiti. Baadhi ya wajumbe walisema hakuna haja, bali serikali ibane hawa hawa waliopo nchini, hasa Heche na Lema. Hasira dhidi ya Lema zilitokana zaidi na kauli yake kutaja Dk. Modestus Kipilimba kwamba anashinikizwa na kushirikishwa katika kupanga mateso dhidi ya wapinzani. Mbali na kusaka fursa ya kumtesa, wanatengeneza “mabomu” dhidi ya mbunge huyo wa Arusha.
3. Wamekerwa na suala la ugonjwa wa Abdallah Mtulia (mbunge wa Kinondoni) kujulikana, wakadai kwamba ugonjwa wake umesababishwa na Chadema. Mtulia ana hali mbaya hospitalini. Makonda na Musiba wamejiapiza kuwa watapambana na Chadema kwa mbinu zote kwa kutumia dola na "uchawi."
4. Kesi ya Mbowe inawapasua kichwa, inawatia hofu (kwa sababu ni ya kubumba); hata mawakili wa serikali wamesema wanalinda hadhi ya taaluma yao, hawataki kuchafuka au kuchafua taaluma zao kwa kesi za kubumba za polisi.
5. Serikali inakerwa mno na taarifa za vikao vyao vya siri kuvuja, na jambo hili linawafanya wachelewe kutekeleza uovu wao wanaopanga dhidi ya Mbowe. Wamesema zamu hii watakuwa makini zaidi.
Yapo mengi, lakini haya ndiyo nimeona vema niyaanike hapa, ili Watanzania na dunia nzima ijue kinachoendelea nyuma ya pazia, wajue aina ya “viongozi” walionao, na wajue nani anahatarisha usalama wa nchi. Hivi ndivyo Bashite na kikosi chake walivyoadhimisha Ijumaa Kuu – kwa kumkejeli Mungu!
MASWALI MAGUMU:
a) Bado Watanzania mnajiuliza nani anamtuma Musiba kufanya press conferences na kutoa matamko ya kushambulia watu kwa tuhuma za ajabu ajabu?
b) Bado mnataka kujua mamlaka inayomlinda Musiba?
c) Idara ya Usalama wa Taifa haijui haya au imenyosha mikono, inafuata maagizo, na imeamua kuacha hatima ya usalama wa nchi hii mikononi mwa watu wawili?
d) Kuna mtu anadhani Makonda anafanya haya kwa hiari yake tu, bila idhini na baraka za Rais Magufuli anayesema maneno ya ajabu dhidi ya wapinzani na wakosoaji wake, hadharani bila aibu, kwamba, “sijaribiwi…. nitawavunja miguu?”
e) Kwa mikakati hii, kwa kuhatarisha badala ya kulinda uhai na usalama wetu, rais anadhani nchi iko salama, na yeye mwenyewe yuko salama?
f) Wakati uovu huu unapangwa rasmi, Rais Magufuli alikuwa kanisani kwenye ibada ya Ijumaa Kuu, “anasali.” Je, naye alibusu msalaba? Kama ndiyo, busu lake lina tofauti gani na busu la Yuda kwa Bwana Yesu – busu la usaliti kwa Watanzania alioapa kuwalinda?
g) Mateso na vifo vya wapinzani na wakosoaji wake ndiyo zawadi ya Pasaka ambayo rais anaandalia Watanzania mwaka huu 2018?
h) Kama utawala wa Kaisari uliangukwa kwa sababu ya kiburi, jeuri na ulevi wa madaraka, utawala wa Magufuli utanusurika vipi ukiwa na sifa zile zile?
Mengine nabaki nayo. Tuendelee kutafakari haya.
Ansbert Ngurumo
MHARIRI BILA MIPAKA (MBM)
Nyammbaffff[emoji117] [emoji83] [emoji196] [emoji90]Ulinzi na usalama wa raia na mali zao na pia kujadili masuala ya kiuchumi na kijamii ktk Mkoa.
Anauleta kwa malengo yake anayoyajua, ila anasahau, kwa kujua au makusudi, kuwa anatoa ushahidi dhidi ya viongozi wake walioko rumande.Jamaa kaishiwa. Jana kauleta huu udaku, leo tena vile vile. Si ajabu akaurudia tena kesho na kesho kutwa.
Katika kufanya uharifu si wote wataunga mkono, hivyo hata mkiwa wawili itavuja tu. Mara ngapi watu kwenye ndoa hutoa siri zao wenyewe kwa wenyewe.Inamaana amezipata hizi taarifa akiwa huko ugaibuni? Kama ni hivyo sasa nihatari,nani amemfikishia taarifa za kikao hicho? Kwa kifupi kuna uvujaji mwingi sana wa taarifa kama ni hivyo,haiwezekani mtu yuko ugaibuni akaqeza kudukua siri za vikao hapa kwetuu
Nafikiri wewe unatengeneza taarifa hizi kwa mgongo wa Ngurumo na wengine walioko nje! Nafikiri serikali ianze kukuchunguza na wewe!!umeletwa wapi?
Ulivyoanza nilidhan utasema ukweli ambao ansbert ngurumo hakuusema kumbe na wewe ni walewale tuAnsbert Ngurumo unaweza ukawa na ' Hoja ' kwa mambo mengine yanayoendelea na kama ujuavyo Mimi GENTAMYCINE huwa nasimama katikati na nachukia pia ' Unafiki ' hivyo naomba niseme Kwako kwamba hakuna hata chembe moja ya ukweli juu ya hiki ulichokiandika hapa na kuna hatari zaidi ya Wewe sasa kutoaminika tena na tuliokuwa tunaanza kukuamini kama nawe utaanza ' Kupika ' hizi so called ' classified information ' zako ili tu kutaka kuwateka Watu waanze kukuamini hata Mimi GENTAMYCINE sasa nitaanza Kukudharau na Kukupuuza kwa Kiwango kikubwa tu.
Ushauri wangu mzuri tu Kwako ni kwamba kwakuwa sasa uko huko ' Ng'ambo ' hebu jaribu kutumia ' Kipaji ' chako cha Uandishi wa Habari na Uhariri ili uweze kupata Ajira ambayo itakuwezesha kuendesha maisha yako na hatimaye uachane na kuwa ' tegemezi ' kwa hao wanakukarimu hapo na pia Pesa / Hela zingine uweze kutuma Kwenu ( namaanisha huku Tanzania ) ziweze kuwasaidia Ndugu zako ambao naamini wanahitaji mno msaada wako.
Ni kweli yapo mambo ambayo yanaudhi kwa sasa Tanzania ila ' Mwenzetu ' sasa umezidisha katika Kutudanganya.
Kila la Kheri Kaka.
Inavyoelekea lengo la kwenda nje ni kutafuta uhuru wa kuwatumikia mabepari bila kufikiwa na mkono wa sheria za Tanzania. Anafanya mambo kama yale ya Mange Kimambi nimenza kufikiri hakuwa anafanyiwa vitisho kama alivyasema bali, alitafuta njia ya kwenda kuishi nje ili akafanye anayoyakusudia.' Logically ' tu Mkuu kwa yule aliyebobea hasa katika masuala ya ' Ujasusi / Unjagu ' hawezi kukubaliana hata mara moja na maelezo ya Ansbert Ngurumo hasa haya aliyoyatoa kwani yana ' weak arguments ' mbele ya IQ za Great Thinkers. Kuna sababu kadhaa ila itoshe tu kusema kwamba yapo mengine ambayo ' Kimantiki ' tu alikuwa ana ' Hoja ' nayo na hata Sisi Wadau tulikuwa tumeyaona ila kwa hili la sasa linalomuhusisha moja kwa moja RC Makonda sijui na Watendaji wengi nitakuwa wa mwisho kabisa katika kuliamini. Kikubwa tu atusaidie katika kutatua ' changamoto ' hasa za mambo ya msingi na kamwe asitake sasa kutaka kutumia mwanya wa Yeye kukimbia Tanzania na kuwa huko aliko sasa ili tu ajitengenezee jina, akubalike upesi, aaminike na kisha aanze kutumika na ' Maadui ' wa Tanzania katika ' kuichafua ' nchi. Bado nina imani nae ila ajitahidi sana aachane na kutunga mambo huku akitafuta ' public sympathy ' kwani haitomsaidia kivile na sana sana inaweza kumhatarishia zaidi ' ustawi ' wake hata huko huko aliko sasa. Awe makini!
shut up your ass,unawachagulia watu cha kuandika humu wewe ni nani?go to hell son of bitch.modeators huu upuuzi umekuwa ukiletwa mara kwa mara unafutwa analeta tena/Unaona kabisa uzushi moderators dont tolerate vitu kama hivi
Huo "Msiba" unahudhuriaje hicho kikao?
Kwa position ipi aliyonayo ili ahudhurie?
Kuna ushahidi Musiba alihudhuria? Kama ni kweli alihudhuria, shutuma alizozitooa hadharani anawajibika kudhibitisha. Na kwenye kikao cha ulinzi na usalama, ni sehemu sahihi ya yeye kuitwa kuthibisha hayo mazito aliyoyasema kwa kuwa yanagusa usalama wa Taifa.Kwa hiyo na Musiba ni mjumbe?
Paskal ,Wachache sana wanaweza elewa umekusudia nini kwenye reply yako,ila nimekuelewa mkuu,wajinga ndo waliwaoDuh!.
Ngurumo, Ngurumo, Ngurumo...
Hii ya Ngurumo kali!, yaani wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wanaripoti kwa Ngurumo!...
bora umekimbia! maana...
Hata hivyo, kwenye tasnia ya media, hakuna kitu kama MBM, kilichopo ni waandishi wasio ma mipaka, Journalists San Frontiers
P
This is phishing...... huyu Ngurumo ni mtego. Serikali ina mkono mrefu. Mnaojifanya kunaswa na mtego wa hizi stori za Ngurumo na mwisho wa siku mnampa taarifa za siri mtaishia shimo la hewa. Hawa jamaa walishakunywa maji ya bendera anachofanya ni chambo tu ili uingie kingi. Wenye kuelewa mmenipata