Anthony Diallo aomba radhi kwa waliomuelewa vibaya kauli yake ya 'Viongozi waliopita walikuwa na Matatizo ya Akili'

😂 neno likisha chomoka halirudishiki mdomooni pinda mugongo pinda mugongo pinda muugongo🕺
Halifichiki pembe lang’ombe hiyo ndio asiliyake..💃🏾🕺🏽💃🏾🕺🏽💃🏾🕺🏽
 
Mzee mpumbavu huyu duuh. Alikua anaongea kwa madaha sana jana leo nn kimempata? Wahehe wanasemaga "Igogola Fivi" yaani anazeeka vibaya.
Tv ya kwake,studio yake,camera yake,mtangazaji wake kwa nini asingee kwa madaha
 
Hao ndo wazee wa rockcity,huyu kihongosi asibishane na wazee,yeye ni kijana mdogo sana,,hajui mambo mengi,,kukimbiza mwenge na kupitia chipukizi isiwe kigezo cha kudharau baba zake
 
Amekutana na nguvu ya walinda legacy na baado lazima aachie uenyekiti wa ccm mwanza
 
Sisi tunashika neno la kwanza tu
Hata aliyekuwa mwenyekiti wake anayemsema kichaa alikuwa na tabia ya kuchomekea au kutafuta kisa na kuja kukitengua baada ya wiki nenda.
Unatengeneza dili chafu baadae unakuja ikana.! Hatushangai tunashika la awali. Hakuna awali mbovu.
Embe likishadondoka mtini halirudi kamwe!

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
Hiki ni kipindi cha kila mtu kutaka kujulikana kwamba ni shujaa, hata kama ni kwa sababu za kuipuuzi.

Naagalia maelezo ya Diallo, ni wazi kwamba hajitambui nafasi yake na hatambui matokeo na maelezo yake.

Kwa kiasi kikubwa ni elimu ndogo aliyonayo ambayo haikuongezeka kwa miaka yote aliyoacha kazi yake ya RMA na kujiita daktari.

Kama kweli alijitoa muhanga bila kujali nafasi yake, iweje siku moja tu unaomba radhi? Hii ni kutaka kujinyonga, kitendo ambacho ni cha kipuuzi, halafu pia ukashindwa kuchagua tawi zuri au kamba imara ya kukamata shingo yako, ambao ni upuuzi wa juu zaidi.

Kwa mtindo huu CCM bado muna mbumbumbu wengi tu!
 
Kitu kinachokukera ina budi ukiweke wazi, kuacha moyoni ni unafiki. Yeye ameweka wazi mawazo yake.
 
“mimi nadhani tuwe waangalifu sana hasa wana CCM, tumeanza kuingiliwa sana.”

“Unakuta ni kiongozi wa chama anatoa tamko na kunituhumu kama vile nimefanya kosa, bila hata kuniuliza. Lazima tuwe waangalifu sana wana CCM,” amesema Dk. Diallo.

Dk. Diallo amesema, ametafasiriwa vibaya na baadhi ya watu huku akiwataka wanachama wa chama hicho tawala nchini Tanzania kuwa makini kwani wapo wasiowatakia mema wanatumia mwanya huo kuwachonganisha.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Kenani Kihongosi alisema, viongozi walioaminiwa na “chama chetu, na wanakaa katika vikao vya maamuzi, tunawaomba wawe na nidhamu na chama hiki.”

Ni nani aliyempa PhD huyu mzee? Hivi watanzania wote ni wajinga? Hapo hakuna kauli nyingine ya chama cha siasa, ni kauli za wanachama wenzake still anasema wanaingiliwa, na nani? Mbowe? Zitto? Mrema? Cheyo? Dovutwa? Rungwa? Akapimwe urine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…