Anthony Diallo aomba radhi kwa waliomuelewa vibaya kauli yake ya 'Viongozi waliopita walikuwa na Matatizo ya Akili'

Anthony Diallo aomba radhi kwa waliomuelewa vibaya kauli yake ya 'Viongozi waliopita walikuwa na Matatizo ya Akili'

Hiki ni kipindi cha kila mtu kutaka kujulikana kwamba ni shujaa, hata kama ni kwa sababu za kuipuuzi.

Naagalia maelezo ya Diallo, ni wazi kwamba hajitambui nafasi yake na hatambui matokeo na maelezo yake.

Kwa kiasi kikubwa ni elimu ndogo aliyonayo ambayo haikuongezeka kwa miaka yote aliyoacha kazi yake ya RMA na kujiita daktari.

Kama kweli alijitoa muhanga bila kujali nafasi yake, iweje siku moja tu unaomba radhi? Hii ni kutaka kujinyonga, kitendo ambacho ni cha kipuuzi, halafu pia ukashindwa kuchagua tawi zuri au kamba imara ya kukamata shingo yako, ambao ni upuuzi wa juu zaidi.

Kwa mtindo huu CCM bado muna mbumbumbu wengi tu!

Imefikia wakati mtu hawezi kuwa na mkweli na kusema ya moyoni kwasababu wengi wa wanasiasa wanapenda watu wabaki wanafiki. Namshikuru mzee huyu kuongea ya moyoni. Sasa wengine wanamwita mjinga🤔
 
Kilicho muhimu ni kwamba Diallo ameuelezea utawala wa awamu iliyopita katika uhalisia wake.

Tatizo la afya ya akili ya marehemu ni dhahiri, na wengi walikuwa wanajua. Juu ya yeye kutibiwa Mirembe na Ujerumani, inafahamika. Lakini kwaajili ya heshima ya mgonjwa, miiko ya kitabibu inasema ugonjwa ni siri ya mgonjwa. Hata hivyo illikuwa siyo sahihi mtu mnayefahamu ana tatizo linaloweza kuleta madhara makubwa kwa Taifa na wananchi, mkampa nafasi ya uongozi wa juu kabisa.
Diallo asiye na tatizo la akili ameifanyia nini nchi hii?

Bila shaka tunahitaji wenye matatizo ya akili zaidi ili tuendelee kuona maendeleo
 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, bwana Anthony Diallo amewaomba radhi watanzania kwa kauli zake alizozitoa kuwa viongozi wa Serikali waliopita walikuwa na mafaili mirembe.
View attachment 1849688

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Dk. Anthony Diallo ameomba radhi ‘kiaina’ baada ya kauli yake kuzua mjadala ndani na nje ya chama chake.

Dk. Diallo amesema, ametafasiriwa vibaya na baadhi ya watu huku akiwataka wanachama wa chama hicho tawala nchini Tanzania kuwa makini kwani wapo wasiowatakia mema wanatumia mwanya huo kuwachonganisha.

Ni baada ya jana Jumamosi, tarehe 10 Julai 2021, kuzungumza masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika utawala wa awamu ya tano akigusia suala la nchi kuongozwa kwa matamko.

Dk. Diallo aliyewahi kuwa waziri, alizungumza hayo katika kipindi cha Ajenda, kinachorushwa na kituo chake cha televisheni cha Star TV, jijini Mwanza.

Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kupata maoni yake juu ya nchi kuongozwa kwa matamko bila kufuata Katiba na sheria, Dk. Diallo alisema, kuna umuhimu wa kuangalia historia ya mtu kabla ya kupewa dhamana ya kuongoza.

Mimi nafikiri tuwe waangalifu tu katika kuchagua tuwe tuna ‘track record’ kwani huko nyuma tuliwahi kuchagua watu walikwisha kwenda hospitali za vichaa ‘milembe’ harafu unamwachia aongoze nchi, kwa hiyo tuwe makini,” alisema.

Kauli hiyo ilizua mjadala na leo Jumapili, tarehe 11 Julai 2021, akizungumza na waandishi wa habari amesema “nilifanya kosa kwa kutolea mfano wa wakati uliopita badala ya wakati ujao kuwa tusipokuwa waangalifu tunaweza kuchagua viongozi wenye matatizo ya akili.”

Na sijasema mtu kuwa aliyekuwa na tatizo ila nilikosea tu kwenye maelezo. Nawataka radhi wale ambao walinielewa vibaya kwani wapo waliotafasiri wanavyojua wao,” amesema Dk. Diallo.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini amsema “mimi nadhani tuwe waangalifu sana hasa wana CCM, tumeanza kuingiliwa sana.”

Dk. Diallo amekosoa kitendo cha baadhi ya viongozi wa chama hicho kuanza kutoa matamko kabla ya kumsikiliza au kumuuliza alikuwa ana maanisha nini.

“Unakuta ni kiongozi wa chama anatoa tamko na kunituhumu kama vile nimefanya kosa, bila hata kuniuliza. Lazima tuwe waangalifu sana wana CCM,” amesema Dk. Diallo.

Miongoni mwa viongozi waliomshtumu ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Kenani Kihongosi alisema, viongozi walioaminiwa na “chama chetu, na wanakaa katika vikao vya maamuzi, tunawaomba wawe na nidhamu na chama hiki.”

“Chama hiki ni kikubwa kuliko mtu, kwa hiyo mwenyekiti na katibu mkuu wetu, niwaombe sisi kama UVCCM, kauli ile imetuudhi sana, mwenyekiti wa CCM anapozungumza hivyo hapaswi kuungwa mkono.”

Kihongosi aliongeza kwa kusema “kama yeye aliona wanapaswa kwenda milembe hapa anafanya nini, kama ni vikao vya maamuzi yeye ni miongoni na kauli zile kama sisi vijana zinatuvunja moyo.”

Mwanahalisi

Hii kawaida kwa wanasiasa kasema makusudi ujumbe ufike. Huyu mzee hana shida yeyote zaidi ya mapenzi kwa nchi yake. Tushukuru hakuwa mnafikiri hata kama hatupendi aliyosema huu ndiyo uhuru wenyewe. Tusikimbilie kuita kila kitu tusi
 
Ujumbe wa Dr. Diallo umenyooka kama rula. Ni nadra sana kwa wana CCM kuziishi ahadi zao za nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko kama alivyofanya Dr. Diallo. Tumpongeze kwa hili.
Diallo na watu wa aina yake ni WANAFIKI, hizi kelele ni baada ya maslahi yake kuguswa, na kwa hakika hautasikia akisema lolote baya likifanywa na chama chake na Serikali inayoongozwa na chama chake.

Baada ya JPM kuondoka kila aina ya ubaya utaelekezwa kwake, kila mtu atajiepusha kujihusisha nae, na hili limeanza kuonekana toka 'juu'. Hata JK alivyoenda kutembelea SGR pamaoja na kutoa credits na pongezi kwa watu walihusika na ujenzi alishindwa kutoa credits kwa JPM.

Mbaya zaidi ni Wapinzani kudandia hoja nyepesi kama hizi hasa kila mtu akisema jambo la kuwafurahisha, leo hata Musiba, Polepole, Diamond na wengine wakimponda JPM wataonekana malaika mbele ya macho ya jamii ya Wapinzani.
 
Hivi ni doctor wa kitu gani huyu shujaa wetu mpya aliyeuzungumza ukweli wa lile sanamu la chato kuwa na valid certificate ya uwendawazimu
Nimeona hapo juu mmoja kaandika kuwa ni RMA lkn akajiita daktari.
 
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Dk. Anthony Diallo ameomba radhi ‘kiaina’ baada ya kauli yake kuzua mjadala ndani na nje ya chama chake.

Dk. Diallo amesema, ametafasiriwa vibaya na baadhi ya watu huku akiwataka wanachama wa chama hicho tawala nchini Tanzania kuwa makini kwani wapo wasiowatakia mema wanatumia mwanya huo kuwachonganisha.

Ni baada ya jana Jumamosi, tarehe 10 Julai 2021, kuzungumza masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika utawala wa awamu ya tano akigusia suala la nchi kuongozwa kwa matamko.

Dk. Diallo aliyewahi kuwa waziri, alizungumza hayo katika kipindi cha Ajenda, kinachorushwa na kituo chake cha televisheni cha Star TV, jijini Mwanza.

Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kupata maoni yake juu ya nchi kuongozwa kwa matamko bila kufuata Katiba na sheria, Dk. Diallo alisema, kuna umuhimu wa kuangalia historia ya mtu kabla ya kupewa dhamana ya kuongoza.

“Mimi nafikiri tuwe waangalifu tu katika kuchagua tuwe tuna ‘track record’ kwani huko nyuma tuliwahi kuchagua watu walikwisha kwenda hospitali za vichaa ‘milembe’ harafu unamwachia aongoze nchi, kwa hiyo tuwe makini,” alisema.

Kauli hiyo ilizua mjadala na leo Jumapili, tarehe 11 Julai 2021, akizungumza na waandishi wa habari amesema “nilifanya kosa kwa kutolea mfano wa wakati uliopita badala ya wakati ujao kuwa tusipokuwa waangalifu tunaweza kuchagua viongozi wenye matatizo ya akili.”

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Kenani Kihongosi

“Na sijasema mtu kuwa aliyekuwa na tatizo ila nilikosea tu kwenye maelezo. Nawataka radhi wale ambao walinielewa vibaya kwani wapo waliotafasiri wanavyojua wao,” amesema Dk. Diallo.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini amsema “mimi nadhani tuwe waangalifu sana hasa wana CCM, tumeanza kuingiliwa sana.”

Dk. Diallo amekosoa kitendo cha baadhi ya viongozi wa chama hicho kuanza kutoa matamko kabla ya kumsikiliza au kumuuliza alikuwa ana maanisha nini.

“Unakuta ni kiongozi wa chama anatoa tamko na kunituhumu kama vile nimefanya kosa, bila hata kuniuliza. Lazima tuwe waangalifu sana wana CCM,” amesema Dk. Diallo.

Miongoni mwa viongozi waliomshtumu ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Kenani Kihongosi alisema, viongozi walioaminiwa na “chama chetu, na wanakaa katika vikao vya maamuzi, tunawaomba wawe na nidhamu na chama hiki.”

“Chama hiki ni kikubwa kuliko mtu, kwa hiyo mwenyekiti na katibu mkuu wetu, niwaombe sisi kama UVCCM, kauli ile imetuudhi sana, mwenyekiti wa CCM anapozungumza hivyo hapaswi kuungwa mkono.”

Kihongosi aliongeza kwa kusema “kama yeye aliona wanapaswa kwenda milembe hapa anafanya nini, kama ni vikao vya maamuzi yeye ni miongoni na kauli zile kama sisi vijana zinatuvunja moyo.”

Chanzo: Mwanahalisi

---
Japokuwa ameomba msamaha, Dkt. Diallo asisamehewe na apewe adhabu kubwa ili iwe fundisho.

Amejua kuwa alifanya fyongo na kuongea pumba. Ili iwe fundisho kwa wanafiki kama Diallo apewe adhabu kali na kutimuliwa kabisa.
Hata mrembe vipi sisi tunajua message sent and delivered! Hata chizi Magufuli alikuwa anasema hivi hivi message sent and delivered!
 
Hiki ni kipindi cha kila mtu kutaka kujulikana kwamba ni shujaa, hata kama ni kwa sababu za kuipuuzi.

Naagalia maelezo ya Diallo, ni wazi kwamba hajitambui nafasi yake na hatambui matokeo na maelezo yake...
 
Alimaanisha future time....tuzingatie hapo maneno yasiwe mengi na aachwe aendeleze maisha, msisumbue wawekezaji pls
 
Diallo lazima watamvaa sana maana dah!
20210711_190418.jpg
 
Cdm mmebaki kuwa wacheza Ngoma za ccm tu kwa sasa, hakuna operation haki, maandamano Wala wabunge wa covid 19, kila sehemu mnaangukia pua.
Mchukueni sasa huyo Dialo wenu
Hakuna jambo linanikera kama hili, CCM ndio wanapiga ngoma CDM wanacheza tena kwenye mambo ya kitoto sana, Mambo ya msingi yote yanakosa mwendelezo na kufa kimyakimya.

Nakumbuka ishu ya Diamond ilichukua wiki moja na zaidi ikafa, Rais na ishu ya Katiba, na sasa hili la Diallo. CDM na wengine wajitafakari.
 
😂 neno likisha chomoka halirudishiki mdomooni pinda mugongo pinda mugongo pinda muugongo🕺
Wanachofanya CCM ni damage control,kumlazimisha mwanaume aombe radhi,lakini jini limeishatoka kwenye chupa.
Kitakachofuata Diallo atajiuzulu wadhifa wake labda baada ya miezi kama sita.
Maneno ya Diallo kudai Mkuu wa kaya alitibiwa na ana file Mirembe imeiweka CCM na serikali yake njia panda kitaifa na kimataifa.
 
Mkwepa Kodi aliyenyooka?

Kweli tatizo ni sisi
... Mahakama ya mafisadi si ipo? Mnasubiri ni kumfungulia mashtaka? Ufisadi wake umeonekana leo? Mwenyekiti wa CCM mkoa tena mkoa muhimu kiuchumi ujue. Mna ndimi elfu enyi wanafiki.
 
Back
Top Bottom