Anthony Diallo aomba radhi kwa waliomuelewa vibaya kauli yake ya 'Viongozi waliopita walikuwa na Matatizo ya Akili'

Anthony Diallo aomba radhi kwa waliomuelewa vibaya kauli yake ya 'Viongozi waliopita walikuwa na Matatizo ya Akili'

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Dk. Anthony Diallo ameomba radhi ‘kiaina’ baada ya kauli yake kuzua mjadala ndani na nje ya chama chake.

Dk. Diallo amesema, ametafasiriwa vibaya na baadhi ya watu huku akiwataka wanachama wa chama hicho tawala nchini Tanzania kuwa makini kwani wapo wasiowatakia mema wanatumia mwanya huo kuwachonganisha.

Ni baada ya jana Jumamosi, tarehe 10 Julai 2021, kuzungumza masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika utawala wa awamu ya tano akigusia suala la nchi kuongozwa kwa matamko.

Dk. Diallo aliyewahi kuwa waziri, alizungumza hayo katika kipindi cha Ajenda, kinachorushwa na kituo chake cha televisheni cha Star TV, jijini Mwanza.

Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kupata maoni yake juu ya nchi kuongozwa kwa matamko bila kufuata Katiba na sheria, Dk. Diallo alisema, kuna umuhimu wa kuangalia historia ya mtu kabla ya kupewa dhamana ya kuongoza.

“Mimi nafikiri tuwe waangalifu tu katika kuchagua tuwe tuna ‘track record’ kwani huko nyuma tuliwahi kuchagua watu walikwisha kwenda hospitali za vichaa ‘milembe’ harafu unamwachia aongoze nchi, kwa hiyo tuwe makini,” alisema.

Kauli hiyo ilizua mjadala na leo Jumapili, tarehe 11 Julai 2021, akizungumza na waandishi wa habari amesema “nilifanya kosa kwa kutolea mfano wa wakati uliopita badala ya wakati ujao kuwa tusipokuwa waangalifu tunaweza kuchagua viongozi wenye matatizo ya akili.”

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Kenani Kihongosi

“Na sijasema mtu kuwa aliyekuwa na tatizo ila nilikosea tu kwenye maelezo. Nawataka radhi wale ambao walinielewa vibaya kwani wapo waliotafasiri wanavyojua wao,” amesema Dk. Diallo.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini amsema “mimi nadhani tuwe waangalifu sana hasa wana CCM, tumeanza kuingiliwa sana.”

Dk. Diallo amekosoa kitendo cha baadhi ya viongozi wa chama hicho kuanza kutoa matamko kabla ya kumsikiliza au kumuuliza alikuwa ana maanisha nini.

“Unakuta ni kiongozi wa chama anatoa tamko na kunituhumu kama vile nimefanya kosa, bila hata kuniuliza. Lazima tuwe waangalifu sana wana CCM,” amesema Dk. Diallo.

Miongoni mwa viongozi waliomshtumu ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Kenani Kihongosi alisema, viongozi walioaminiwa na “chama chetu, na wanakaa katika vikao vya maamuzi, tunawaomba wawe na nidhamu na chama hiki.”

“Chama hiki ni kikubwa kuliko mtu, kwa hiyo mwenyekiti na katibu mkuu wetu, niwaombe sisi kama UVCCM, kauli ile imetuudhi sana, mwenyekiti wa CCM anapozungumza hivyo hapaswi kuungwa mkono.”

Kihongosi aliongeza kwa kusema “kama yeye aliona wanapaswa kwenda milembe hapa anafanya nini, kama ni vikao vya maamuzi yeye ni miongoni na kauli zile kama sisi vijana zinatuvunja moyo.”

Chanzo: Mwanahalisi

---
Japokuwa ameomba msamaha, Dkt. Diallo asisamehewe na apewe adhabu kubwa ili iwe fundisho.

Amejua kuwa alifanya fyongo na kuongea pumba. Ili iwe fundisho kwa wanafiki kama Diallo apewe adhabu kali na kutimuliwa kabisa.
Mic inawekwa sikioni,huyu ni kichaa period
tapatalk_1626121136163.jpeg
 
CHADEMA mmebaki kuwa wacheza Ngoma za CCM tu kwa sasa, hakuna operation haki, maandamano Wala wabunge wa covid 19, kila sehemu mnaangukia pua.
Mchukueni sasa huyo Dialo wenu
Chizi karogwa tena
tapatalk_1626121136163.jpeg
 
Kila mtu kiasili ana kiasi fulani cha ukichaa.
Wale wanaovuka kiwango kinachovumilika ndiyo wanaonekana vichaa kutokana na maneno au vitendo vyao.
Vichaa waweza kujibizana na mtu mwenye akili timamu au wenywewe kwa wenywewe. Watatambulika kwa maneno na vitendo vyao.
 
Ukweli umeshajulikana, wanaojalibu kuupindisha wanajihangaisha. Tumekwelewa Dialo. Ndio maana tulikuwa tunashangaa sana iwapo ile ilikuwa ni hali ya kawaida.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Nimesoma na kupokea maoni,ushauri na kila aina ya hisia ambazo naamini ni kwa upendo juu ya Clip yangu kuhusu kambi za Kitaaluma nilipokuwa nikizungumza na wananchi wetu katika tafsiri yoyote ile naomba Radhi kwa wote waliokwazika ,

wananchi na Viongozi wenzangu hasa pale matumizi ya neno "Waziri" lilipobeba hisia tofauti nawaheshimu Mawaziri wote na nafanya nao kazi kwa ushirikiano mkubwa natambua pia kazi nzuri inayofanywa na Mawaziri wetu wanaosimamia sekta ya elimu -

Wapo wanaodhani maelezo ya hisia zangu ni kuanza kupandisha mabega,na pengine mgema akisifiwa tembo hutia maji-niwaondoe hofu sina sababu ya kupandisha mabega .
 
Tujifunze kuomba radhi na kuwajibika,huwezi kutoa kauli za kubeza wateule wenzako wenye dhamana walizokabidhiwa wasimamie kama wewe.
 
Tujifunze kuomba radhi na kuwajibika,huwezi kutoa kauli za kubeza wateule wenzako wenye dhamana walizokabidhiwa wasimamie kama wewe.
 
Tujifunze kuomba radhi na kuwajibika,huwezi kutoa kauli za kubeza wateule wenzako wenye dhamana walizokabidhiwa wasimamie kama wewe.
Sasa Jiwe nani alimkabidhi zamana isipokuwa alipitishwa kwa LAZIMA na NEC. Tulikuwa na Rais uchwara kuwahi kutokea.
 
Nimesoma na kupokea maoni,ushauri na kila aina ya hisia ambazo naamini ni kwa upendo juu ya Clip yangu kuhusu kambi za Kitaaluma nilipokuwa nikizungumza na wananchi wetu katika tafsiri yoyote ile naomba Radhi kwa wote waliokwazika ,wananchi na Viongozi wenzangu hasa pale matumizi ya neno "Waziri" ...

Sasa kichwa cha habari na habari Mbona vitu viwili tofauti Vipi umepagawa ?!
 
Hapo ni Diallo au Mtaka
Heading na content ni ccm/chadema
 
Nimesoma na kupokea maoni,ushauri na kila aina ya hisia ambazo naamini ni kwa upendo juu ya Clip yangu kuhusu kambi za Kitaaluma nilipokuwa nikizungumza na wananchi wetu katika tafsiri yoyote ile naomba Radhi kwa wote waliokwazika ,wananchi na Viongozi wenzangu hasa pale matumizi ya neno "Waziri" lilipobeba hisia tofauti nawaheshimu Mawaziri wote na nafanya nao kazi kwa ushirikiano mkubwa natambua pia kazi nzuri inayofanywa na Mawaziri wetu wanaosimamia sekta ya elimu - Wapo wanaodhani maelezo ya hisia zangu ni kuanza kupandisha mabega,na pengine mgema akisifiwa tembo hutia maji-niwaondoe hofu sina sababu ya kupandisha mabega .
Ujumbe umefika na kugonga kwenye kidonda kibichi. Jiwe alikuwa Milembe material.
 
Mimi nimeandika mtaka naona moderator wamebadilisha sijui wana nini hebu wekeni vizuri heading hiyo
 
Back
Top Bottom