Anthony Lusekelo adai Uwezekano wa matajiri kuingia mbinguni ni 70% na masikini kuikosa mbingu ni 99.9%,

Jibu hoja Mkuu
Actually, huyu jamaa huwa anasoma Biblia literally kama mtu anavyosoma kitabu Cha historia au jiografia. Biblia haisomwi hivyo. Lugha ya Biblia ni tofauti. Ni lugha inayomtaka msomaji atafsiri kama ilivyo kwa sheria. Huwezi kusoma sheria hivi hivi tu, lazima utafsiri/upate maana yake otherwise you get it wrong. Ndiyo maana kuna watu wanasomea. It's not for fun, bali ili waweze kutapata tafsiri sahihi. Hata kwa sheria lazima usomee ili uweze kutafsiri vizuri, otherwise you get wrong!
 
Labda kachanganyikiwa, ni konyagi inaongea. " hakika nawaambia kwa tajiri kuingia ufalme wa mbinguni ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano "
 
ningekuwa na pesa huyu mzee ningemuweka kwenye kiwanda changu cha pombe kujua asilimia ya pombe kuliko kupeleka TBS
 
Nawaambia tena, Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.

Mathayo 19:24

"Watumishi wa Mungu, wajane na mayatima wanategemea sadaka yako Mungu ameeleza hivyo. Kwahiyo kama wewe ni lofa hauna sadaka usiende kanisani" - amesema mchungaji Anthony Lusekelo maarufu kama Mzee Wa Upako

Source: Swahili World page on Facebook
1 Akainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina.

Luka 21:1
2 Akamwona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili.

Luka 21:2
3 Akasema, Hakika nawaambia, huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote;

Luka 21:3
4 maana, hao wote walitia sadakani katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo.


Luka 21:4


===============
Huyo Lusekelo Yuko kinyumenyume na bosi wake YESU. Tumwamini nani? YESU au Lusekelo?

Hao ndiyo manabii wa uongo waliozungumzwa katika bible πŸ‘‡πŸ‘‡

1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.

1 Yohana 4:1
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ jamani
 
Yeye ataingia wapi na bapa lake la konyagi mkononi?
 
Aliyekuwa anamuhoji huyo fala, angemuuliza je yule Lazaro aliyeandikwankatika Biblia kuwa ni amskini na alipokufa akaenda mbinguni, alimzidi vipi sadaka yuke tajiri aliyeenda jehanamu baada ya kufa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…