Antonio Nugaz, ni saa ngapi unaenda kukinukisha Yanga SC baada ya kukereka na dharau uliyoonyeshwa?

acheni utoto nyie hivi hamkuonq wakati nugaz ana muita manara msukule?

Ni swala la muda tu mbona,Jangwani patatifuka,tutakuja kufukua huu uzi na mtaukimbia
 

Sijui kwa nini Mashabiki wa Yanga wenye kujielewa hili hawalioni pamoja na kukumbushwa na kina Hemed Kivuyo.

Manara aombe sana Yanga ifanye vizuri uwanjani,lakini ikivurunda kama
msimu uliyopita,Jangwani atapakimbia mwenyewe.Kumbuka kuna Watu pale wengi tu hawakubaliani na ujio wake.Ni pesa ya Ghalib ndiyo inamuweka pale,aombe sana Mungu Team ifanye vizuri uwanjani ndiyo itakuwa salama yake.
 
Aisee nitaanza kukufwatilia Kwa karibu sana!!!...Naona habari zako ni pure
 
Kaka watu naona wanajali matumbo yao tu sasa...

Kama Manara yule kaenda Yanga, basi haitashangaza bwana kulia lia Nugaz kuungana na Kamwaga...
Kamwaga anaachia ngazi,wanaopigiwa chapuo ni Mwijaku na Kumbuka,pia na Nugaz akiwemo sio mbaya jamaa yuko makini sana ni mwanasimba yule kule Yanga ni mambo ya kazi tu kama alivyo Manara.
 
Hili suala mbona kitenge na oscar oscar hawajalishikia bango kama la Manara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…