The Burning Spear
JF-Expert Member
- Dec 23, 2011
- 4,118
- 9,864
Huyu bwana ni moja ya watanzania wachache wenye weledi na uzalendo wa hali ya juu. Kwa Kariba yake ukuu wa mkoa ni nafsi ndogo Sana. Alipaswa awepo kwenye ngazi za juu za maamuzi ya Nchi.
Tatizo linakuja tu ni Nchi aliyopo na mfumo wa sasa wa ubadhilifu mwingi amabao Kwa ufupi hawezi kuingia.
Enzi za magufuli siyo tu kwamba alikuwa anasifiwa bure Hapana, aliyoyatenda simiyu hawatamsahau alikuwa mkombozi wao.
CCM wanajitahidi Sana kumnyamazisha hata DODOMA hakutolewa kwenda njombe Kwa bahati mbaya, maana mitazamo Yake Hakuna kiongozi yeyote anayemfikia hata raisi mwenyewe.
CCM Wanaamini kumwacha aendelee kuhuburi anayoyaamini ni kama anakuwa anawadharirisha viongozi wake.
Ndo hivyo ni binadamu na anaijua CCM vizuri ukiwa jeuri kupindukia unazikwa hii imepelekea watu wengi wenye weledi kukaa kimya wakihofia maisha yao, magufuli tu Ndo alijitoa mhanga.
Mbunge wa sengerema CCM Hamisi Tabasamu alishasema wazalendo Nchi hii ni wakutafuta Kwa tochi, na ukiwa mzalendo utafuatiliwa kwelikweli, Lakini Hata Humphrey polepole kwenye mahojiano na Dar 24 jambo hili alilitamka.
Huyu bwana atabaki kuwa mzalendo pengine utatokea mfumo huko mbele ambao utampa mamlaka ya juu zadi ili aweze kulivusha Taifa kwenda hatua nyingine.
Naamini hata hii Leo ukimuliza MTAKA suluhisho la uhaba wa maji na kukatikakatika Kwa umeme majibu atakayokupa yanaweza kuwa dhihaka kwa watawala.
Lakini hamna namna, Ngoja tuendelee na vilanza wetu ila ipo siku mawe yataongea.