Anzisheni mahusiano na watu wazima, hawa wa chini ya miaka 35 hawana tofauti na vitoto

Anzisheni mahusiano na watu wazima, hawa wa chini ya miaka 35 hawana tofauti na vitoto

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Anzisheni mahusiano na watu wazima, hawa wa chini ya miaka 35 hawana tofauti na vitoto, kutokana na kuwa na ahadi nyingi hewa.

Kwa upande wangu, mabinti walio chini ya miaka 35 mimi huwa nawaita vitoto; kwa sababu wana usumbufu fulani katika uanzishaji wa mahusiano.

Wengi wao wanatoa ahadi feki, unaweza ukamtumia nauli na asifike, au akajizungusha zungusha huku akiamini kuwa yeye ni mzuri, kwa hiyo lazima akutese.

Yaani mpaka mvutane sana, ndio atakuja kwenye 'appointment' yako. Atajiwekea mazingira 'expensive' ya kutokutaka kuoanana na wewe; mara atakwambia nipo kwenye mzunguko wa mwezi, mara nimetumwa na boss, mara sina nafasi nina majukumu fulani n.k, lengo ni kujiweka wa gharama wakati hana hizo gharama.

Kutokana na huo ujinga wao; mi huwa nawapiga chini, napambana na hawa watu wazima waliokomaa, kuanzia miaka 36+, siwezi kusumbuana na vitoto mimi.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom