Aomba Rais Samia amsaidie mtoto wake aliempatia jina la SAMIA

Aomba Rais Samia amsaidie mtoto wake aliempatia jina la SAMIA

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
"Ninaitwa Eza Ashindikene. Kwa sasa ninaishi Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Mkuranga.

Mwaka 2025, wakati wa uchaguzi Mkuu Tanzania, nilipata nafasi ya kuandika nyimbo kama msanii kwa ajili ya kuunga mkono harakati za kuwaombea kura wagombea wetu. Wakati huo nilikuwa na ujauzito wa miezi tisa.

Mungu akajaalia, siku tatu kabla ya uchaguzi nilijifungua mtoto wa kike. Kwa upendo na heshima, nilimpa jina Samia, ambalo ni jina la Rais Samia Suluhu Hassan

Ombi langu kwa Mheshimiwa Rais ni aweze kutambua uwepo wa mtoto wangu ambaye ni wajina, wake 'Samia', anisaidie kwa changamoto za malezi ambazo napitia.

Kwa sasa, shughuli yangu ni sanaa, ambapo ninafanya kazi ya kuimba na kuigiza. Mtoto anaendelea vizuri, ingawa anakabiliwa na changamoto ya malezi bora kutokana na hali duni ya kipato kidogo nilicho nacho. Kwa sasa mtoto yupo Mkoa wa Lindi. Baba wa mtoto alifariki mwezi Oktoba, mwaka 2025.

Hali yangu ya maisha ilizidi kuwa ngumu. Nikalazimika kumwachisha mtoto kunyonya na kumpeleka Kusini (Lindi) ili akaishi na mama yangu, huku mimi nikiendelea kutafuta maisha na kupambana kupata pesa ya kutunza familia

Hivyo ndivyo hali yangu ilivyo kwa sasa. Ninapopata shughuli za sanaa na kulipwa, nagawana na familia yangu kijijini."


1787895719409.png
 
Back
Top Bottom