Apata kipigo kwa kufanya masturbation(kujichua)

Apata kipigo kwa kufanya masturbation(kujichua)

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Nakuletea habari nyingine ya ukweli kabisa isiyochanganyika na chembe yoyote ya uongo. Hivi majuzi, kuna mtu alipata kipigo kwa sababu ya tabia yake ya kupenda kujichua(punyeto). Mtu huyu alionywa mara nyingi kuwa kujichua(masturbation) ni dhambi, lakini aliendelea tu kukaidi. Nani alimpa kipigo?

Mtu huyu alipigwa na Mungu mwenyewe. Ilikuwa hivi: alianza kuhisi hali isiyo ya kawaida katika macho yake. Akaenda kufanyiwa check-up katika hospitali kubwa, ya kisasa, yenye daktari aliyebobea katika kutibu magonjwa ya macho. Akaambiwa kuna vipele vipele vidogo pembezoni mwa macho (kwa ndani). Akapewa dawa ya kutumia wiki tatu na kuhakikishiwa kuwa shida hiyo itaisha kabisa.

Akaanza kutumia dawa, wiki ya kwanza ikapita bila nafuu. Wiki ya pili akaanza kusikia ahueni. Siku ya 14, hali ikabadilika ghafla. Akawa hawezi kabisa kutazama mwanga wowote ule - wa jua, wa tochi, wa taa, na hata mwanga wa simu! Akitazama tu mwanga kidogo unayachoma macho yake kama sindano na kumsababishia maumivu makali sana. Hivyo ikabidi awe anafumba macho tu.

Baadaye akang'amua dhambi ya kujichua ndiyo iliyomsababishia shida hiyo. Akatubu sana kwa machozi na kumwahidi Mungu kuwa hatarudia tena. Ndani ya dakika chache tatizo hilo likaisha! Akaanza kuona vizuri kabisa bila kusumbuliwa na mwanga. Hakuendelea tena kutumia ile dawa na mpaka leo hajasikia tatizo lolote katika macho yake. Tangu siku ile aliacha kujichua na anaendelea kuishi maisha yanayompendeza Mungu.
 
Labda sasa unajiuliza: je, Mungu anaweza kumpiga au kumwadhibu mtu? Na je, kujichua ni dhambi? Imeandikwa wapi? Majibu ya maswali yote hayo ni: "NDIYO".
Waebrania 12:6-7
"Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humuonya. Naye humpiga kila mwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya kuonywa mnastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyeonywa na babaye?"

Andiko hilo linaonyesha kwamba Mungu anaweza kuwaadhibu wale anaowapenda, kwa lengo la kuwafundisha waache mabaya, watende mema. Mungu anawatendea hivyo watoto wake, kwa kuwa ni mtoto yupi asiyeadhibiwa na mzazi wake?
 
Maandiko yafuatayo yanaonyesha wazi kujichua ni dhambi:
1 Wakorintho 3:16-17
"Je, hamjui kwamba nyinyi ni hekalu la Mungu, na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Basi, mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu; maana hekalu la Mungu ni takatifu, na hekalu hilo ni nyinyi wenyewe.”

Kujichua kunaleta madhara mengi ya kimwili. Ni kuuharibu mwili. Miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, hatupaswi kuiharibu.

Wagalatia 5:19-21
"Basi matendo ya mwili ni dhahiri, nayo ni haya: Uasherati, uchafu, ufisadi, kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha kuwaonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama hayo, hawataurithi ufalme wa Mungu."

Kujichua ni tendo linalofanana na uasherati na uchafu

Wagalatia 5:16

"Basi nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka."

1 Petro 2:11
"Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho."

Mathayo 5:27-32
“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Usizini.’ Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake."

Mara nyingi kujichua huendana na kumtamani mwanamke/mwanaume fulani

Waefeso 5:3
"Lakini uasherati usitajwe miongoni mwenu kamwe, wala uchafu wa aina yoyote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu wa Mungu."

Yuda 1:7
"Kumbukeni pia Sodoma na Gomora, na miji ya kandokando yake; wenyeji wake walifanya kama wale malaika; walifanya uzinzi na mambo yaliyo kinyume cha maumbile, wakapewa hukumu ya moto wa milele, iwe onyo kwa watu wote."

Kujichua ni tendo lililo kinyume na maumbile. Mungu alimuumba mwanaume na mwanamke, waishi pamoja katika ndoa. Mwanadamu hakuumbwa aishi peke yake na kujiridhisha kimwili. Ndio sababu tunaambiwa:
1 Wakorintho 7:9
"Lakini kama hawawezi kujizuia, basi waoe na kuolewa, kwa maana ni afadhali kuoa au kuolewa kuliko kuwaka tamaa."
 
Pale jitegemee kambi ya Jeshi kitengo cha salvation army Kuna shule ya watoto walemavu.unataka kuniambia wale watoto wamemkosea nini mungu mpaka kuwapa ile adhabu?
Huyo amepiga punyeto amepewa adhabu ya upofu je wale watoto wenye ulemavu walitenda uovu gani?
 
Nakuletea habari nyingine ya ukweli kabisa isiyochanganyika na chembe yoyote ya uongo. Hivi majuzi, kuna mtu alipata kipigo kwa sababu ya tabia yake ya kupenda kujichua(punyeto). Mtu huyu alionywa mara nyingi kuwa kujichua(masturbation) ni dhambi, lakini aliendelea tu kukaidi. Nani alimpa kipigo?

Mtu huyu alipigwa na Mungu mwenyewe. Ilikuwa hivi: alianza kuhisi hali isiyo ya kawaida katika macho yake. Akaenda kufanyiwa check-up katika hospitali kubwa, ya kisasa, yenye daktari aliyebobea katika kutibu magonjwa ya macho. Akaambiwa kuna vipele vipele vidogo pembezoni mwa macho (kwa ndani). Akapewa dawa ya kutumia wiki tatu na kuhakikishiwa kuwa shida hiyo itaisha kabisa.

Akaanza kutumia dawa, wiki ya kwanza ikapita bila nafuu. Wiki ya pili akaanza kusikia ahueni. Siku ya 14, hali ikabadilika ghafla. Akawa hawezi kabisa kutazama mwanga wowote ule - wa jua, wa tochi, wa taa, na hata mwanga wa simu! Akitazama tu mwanga kidogo unayachoma macho yake kama sindano na kumsababishia maumivu makali sana. Hivyo ikabidi awe anafumba macho tu.

Baadaye akang'amua dhambi ya kujichua ndiyo iliyomsababishia shida hiyo. Akatubu sana kwa machozi na kumwahidi Mungu kuwa hatarudia tena. Ndani ya dakika chache tatizo hilo likaisha! Akaanza kuona vizuri kabisa bila kusumbuliwa na mwanga. Hakuendelea tena kutumia ile dawa na mpaka leo hajasikia tatizo lolote katika macho yake. Tangu siku ile aliacha kujichua na anaendelea kuishi maisha yanayompendeza Mungu
Huyo mtu ni wewe au ni mwingine alitoa ushuhuda kanisani?... Kupiga kunyeto ni udhaifu mkubwa sana
 
1. Hiyo dhana ya kwamba punyeto huleta upofu iliyoibuka marekani ilishathibitishwa kuwa ni uongo. Usipotoshe watu.

2. Punyeto ni uraibu mbaya, waathirika wanapaswa kusaidiwa na sio kunangwa. Wapiga punyeto ni waathirika, sio wahalifu.

3. Hatuchagui kuingia kwenye uraibu, uraibu unaharibu jinsi akili inavyofanya kazi, unakufanya kuwa tegemezi. Ndio maana kutoka ni mchakato.

4. Kama Mungu hataki watu wapige punyeto, asiruhusu watu wapige punyeto! Anakupa vichochezi, ubongo dhaifu na hisia za ngono halafu hataki upige punyeto?
 
Hizi sababu ndizo zilizokufanya mpaka uka-dislike post ya mtoa mada?
Kila mtu na mtazamo wake, na si kila post ni ya ku-dislike hasa ikiwa na neno la hekima ndani yake

Anyway, kila mtu na mawazo yake.
Jioni njema kaka.
 
Yaani kuna watu seriously wanakaa wanatudanganya kuhusu mazara ya punyeto seriously....

Mimi nikikuta mtu anamsema mwenzake kuhusu punyeto kwanza naweza mchapa vibao alaaaah..

Hivi mnajua faida ya punyeto.
Uwezi jua mpaka siku ukaja kupata magonjwa ya STDs na STIs.

Kwanini mnaleta story za vijiweni kuhusu madhara ya punyeto...
Wakuu wanasema everything is harmful kama tuu kita exceed ile limit...

Sasa mpaka anafikia mtu anapigwa kisa punyeto what kind of that behaviour..
Mnajua ni kiasi gani punyeto inaokoa matumizi ya pesa..

Hvi mnajua ulevi wa ngono ndio unapelekea watoto wa mtaani.
Mimba za utotoni...
Single maza
Magonjwa na kazarika

Ndugu jamaa na marafiki kama bado upo katoka rika la kujitafuta piga punyeto kwa kiasi.

Kama ni mtu upo katika ndoa una constantly timetable ya kupata kitumbua wewe ukipiga punyeto huna budi kupigwa mpaka uzimii huo utakua ni uvunjaji wa sheria
 
Back
Top Bottom