Maandiko yafuatayo yanaonyesha wazi kujichua ni dhambi:
1 Wakorintho 3:16-17
"Je, hamjui kwamba nyinyi ni hekalu la Mungu, na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Basi, mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu; maana hekalu la Mungu ni takatifu, na hekalu hilo ni nyinyi wenyewe.β
Kujichua kunaleta madhara mengi ya kimwili. Ni kuuharibu mwili. Miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, hatupaswi kuiharibu.
Wagalatia 5:19-21
"Basi matendo ya mwili ni dhahiri, nayo ni haya: Uasherati, uchafu, ufisadi, kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha kuwaonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama hayo, hawataurithi ufalme wa Mungu."
Kujichua ni tendo linalofanana na uasherati na uchafu
Wagalatia 5:16
"Basi nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka."
1 Petro 2:11
"Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho."
Mathayo 5:27-32
βMmesikia kwamba ilinenwa, βUsizini.β Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake."
Mara nyingi kujichua huendana na kumtamani mwanamke/mwanaume fulani
Waefeso 5:3
"Lakini uasherati usitajwe miongoni mwenu kamwe, wala uchafu wa aina yoyote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu wa Mungu."
Yuda 1:7
"Kumbukeni pia Sodoma na Gomora, na miji ya kandokando yake; wenyeji wake walifanya kama wale malaika; walifanya uzinzi na mambo yaliyo kinyume cha maumbile, wakapewa hukumu ya moto wa milele, iwe onyo kwa watu wote."
Kujichua ni tendo lililo kinyume na maumbile. Mungu alimuumba mwanaume na mwanamke, waishi pamoja katika ndoa. Mwanadamu hakuumbwa aishi peke yake na kujiridhisha kimwili. Ndio sababu tunaambiwa:
1 Wakorintho 7:9
"Lakini kama hawawezi kujizuia, basi waoe na kuolewa, kwa maana ni afadhali kuoa au kuolewa kuliko kuwaka tamaa."