App Mpya ya JamiiForums: Fuata hatua hizi
Kuna zile uzi tumesubscribe mbona kwenye hii maboresho sioni kipengele cha subscribed?
Hakuna cha app mpya hapo ni kwamba ,kama mlikuwa hamjui chrome, firefox na browsers jamii hizo zina option ya ku add page kuwa shortcut so walichokifanya hapo ni kuongeza option ya ku add shortcut simple no additional options bali ni shortcuts .
 
Naam wakuu,

Kwa mara nyingine tumeona tuboreshe huduma ya JF ili izidi kuwa rahisi kutumia.

Kwa sasa unaweza ku-Install JF App kwa PC au Tablet (iPad zikiwemo) na Simu za Mkononi (Android na iPhones).

FAIDA:

1) Ni rahisi kutumia na haina tofauti yoyote na main site, hakutakuwa na malalamiko tena kuwa kuna kukosa notifications au kushindwa kufanya actions kadhaa

2) Ni rahisi kufunguka kuliko unavyodhania. Installation yake inachukua sekunde moja au pungufu. Haichukui space kwenye simu yako au kifaa chako

3) Ukiwa offline, bado kuna content utakuwa na access nayo kwa urahisi zaidi. Hulazimiki kuwa mtandaoni

4) na mengine mengi

Hatua za kufuata:

Kwa wanaotumia PC:

Tembelea JF kwa kutumia Google Chrome Browser, kisha utaona sehemu kama hii kwenye browser yako:

View attachment 1791283

View attachment 1791292

Kisha bonyeza Install kama inavyoonekana hapa chini:

View attachment 1791284

Utaona tayari unayo App kwenye PC yako. Kuanzia hapo hutokuwa ukilazimika kutembelea tovuti kwa njia ya browsing ya kawaida.

Mfano, mwenye Macbkook ataona icon ya App ya JF ikiwa hivi:

View attachment 1791290

Kwa wanaotumia Android Devices:

Tumia Google Chrome (au native browser ya simu yako):

Bonyeza mistari mitatu iliyo kushoto mwa LOGO ya JamiiForums, utaona kitu kama hiki chini:

View attachment 1791285

View attachment 1791286

Bonyeza INSTALL kisha utaona hivi (itachukua sekunde 1 ku-Install)

View attachment 1791287

Kwa wanaotumia iPhone au iOS devices:

Tumia Safari Browser, bonyeza sehemu hizi zilizozungushiwa na fuata maelekezo kwenye simu... Just add to your device's home screen.

View attachment 1791288
View attachment 1791289

Ukikwama usisite kuuliza, tupo kwa ajili yako.

TAKE NOTE: Siku zijazo tutaondoa App zilizopo kwenye Google na Apple stores!

PS: Kuna watu wanataka kujua kuhusu kupata notifications. Tafadhali enable push notifications kwenye settings na utazipata bila shaka.

Karibuni
Mungu akuongoze katika ubunifu wako Maxence Melo Mubyazi
 
Kuongeza,hii ni kwa sisi android usersl!!!

Kwenye browser lazima u-log in kwanza ili uweze kuona option ya ku-downloud hii app. hii ni changamoto nimekutana nayo ila ndogo sana ukiwa mtu wa kujiongeza.
Mbona me nimelog in ila bado sioni option ya ku install?
 
Back
Top Bottom