Beberu Mwitu
JF-Expert Member
- Mar 31, 2019
- 495
- 708
Habari zenu wana JF,
Niende moja kwa moja kwenye mada hii tata;
Ipo hivi, mwanzoni mwa mwezi Septemba nilichacha sana kifedha ikabidi nifanye re-installation ya App moja ya mikopo na kuchukua kiasi cha Sh 200,000. Baada ya hapo update ikaja kuwa mkopo ulipwe ndani ya siku saba ilhali mwanzo walionesha siku 120 kiasi cha Sh 270,000!
Ee bwana nikaamua kuiweka laini kando. Baada ya siku kadhaa nikauza simu yangu ya Samsung nikiwa nimefuta data zote na kununua Iphone mtumba uliorekebishwa. Na hiyo laini niliyoombea mkopo sijaiweka kwenye hii simu ya sasa.
Lakini hivi karibuni kuna mawazo mawili yanayopingana, moja ni la kilokole linaniambia walipe jingine linasema achana nao”.
Nilijaribu kuwacheki ili kujua namna bora ya kuwalipa kwa sababu hiyo app haipo kwenye AppStore, nilipewa njia mbadala ya kuwalipa ambayo ni kwa kutumia menu ya kawaida ya mtandao wa simu.
Pia niliwaomba waondoe wanachoita penalty lakini wakagoma, hapo ndipo lile wazo la usiwalipe likaja tena kwa kasi ya 4G😆. kuna muda naingiwa na huruma sana kwani hiyo ni biashara ya watu.
Naomba mnishauri kuhusu hili, niwalipe au nisiwalipe?
NB: wadhamini niliowaweka ni namba zangu mwenyewe ambazo sizitumii kabisa na nilishazipoteza hivyo nimeweka Ghost referees🙂
Update:
Siku ya jana tarehe 10, nilijaribu kuwatumia Sh 202,500 kama sehemu ya malipo. Nilifanya hivyo mara 4 na mara zote hizo watu wa mtandao wa simu waliniambia niache ufala. Wakaurudisha muamala huo😃.
Halafu cha ajabu mpokeaji wa fedha( kampuni),alikuwa na jina tofauti na aliyenikopesha. Sijui kuwa ni ishu ya utakatishaji fedha au vipi!