Application ya mikopo ya ukopeshaji imegonga mwamba, sijui nilipe huu mkopo au niingie mitini?

Application ya mikopo ya ukopeshaji imegonga mwamba, sijui nilipe huu mkopo au niingie mitini?

Habari zenu wana JF,

Niende moja kwa moja kwenye mada hii tata;

Ipo hivi, mwanzoni mwa mwezi Septemba nilichacha sana kifedha ikabidi nifanye re-installation ya App moja ya mikopo na kuchukua kiasi cha Sh 200,000. Baada ya hapo update ikaja kuwa mkopo ulipwe ndani ya siku saba ilhali mwanzo walionesha siku 120 kiasi cha Sh 270,000!

Ee bwana nikaamua kuiweka laini kando. Baada ya siku kadhaa nikauza simu yangu ya Samsung nikiwa nimefuta data zote na kununua Iphone mtumba uliorekebishwa. Na hiyo laini niliyoombea mkopo sijaiweka kwenye hii simu ya sasa.

Lakini hivi karibuni kuna mawazo mawili yanayopingana, moja ni la kilokole linaniambia walipe jingine linasema achana nao”.
Nilijaribu kuwacheki ili kujua namna bora ya kuwalipa kwa sababu hiyo app haipo kwenye AppStore, nilipewa njia mbadala ya kuwalipa ambayo ni kwa kutumia menu ya kawaida ya mtandao wa simu.

Pia niliwaomba waondoe wanachoita penalty lakini wakagoma, hapo ndipo lile wazo la usiwalipe likaja tena kwa kasi ya 4G😆. kuna muda naingiwa na huruma sana kwani hiyo ni biashara ya watu.

Naomba mnishauri kuhusu hili, niwalipe au nisiwalipe?
NB: wadhamini niliowaweka ni namba zangu mwenyewe ambazo sizitumii kabisa na nilishazipoteza hivyo wameshindwa kuwapata kabisa. Pia app haikuomba permission yoyote wakati wa kuomba mkopo.
Jitahidi usikimbie deni la 200,00.

Ni aibu sana kukimbia deni la pesa ambayo kwetu wengine hata haitoshi kununua mswaki.

Namaanisha ule mswaki wa kusafishia kinywa kila siku asubuhi na kabla ya kulala ninaotumia hiyo hela huwezi kuupata.
 
Utapigwa blacklist moja matata sana, siku unaenda Bank unataka mkopo unashangaa wanakuambia wewe sio mlipa madeni, unadaiwa sehemu xxxx na hujalipa.
Tatizo haliji mara moja, siku utakwama tena, ukienda kukopa unaambiwa mambo hukutegemea. Lipa mkopo uwe huru.
Nia ya kuwalipa hiyo 270,000sh ipo lakini kulipa penalty siwezi. Wasiwasi wangu ni kwamba naweza kuwalipa hiyo 270K lakini wakaniripoti kama defaulter kwa sababu ya penalty yao inayoongezeka kila siku.
Na hapo ndio wazo la kutokuwalipa kabisa linakuja.
 
Jitahidi usikimbie deni la 200,00.

Ni aibu sana kukimbia deni la pesa ambayo kwetu wengine hata haitoshi kununua mswaki.

Namaanisha ule mswaki wa kusafishia kinywa kila siku asubuhi na kabla ya kulala ninaotumia hiyo hela huwezi kuupata.
Sikimbii deni kwa sasa ila wakiendelea na msimamo wao wa kuniwekea penati siwalipi, yaani wapate faida ya laki moja kwa wiki nne kwa mtaji wa laki mbili🤣
 
Sababu zilizo nje ya uwezo wangu zilipelekea marejesho kuchelewa. Kama nawe ni mhusika waambie waondoe hiyo penalty ili walipwe hiyo 270,000 au wang’ang’anie kuibakiza ili waambulie sifuri. Uamuzi ni wao.
Pambana ulipe uondokane na aibu ndogondogo katika maisha.

Hata ukiwa na tatizo la kulipa mkopo, mkopo wenyewe uwe mzito basi.

Siyo unakimbia kulipa mkopo wa hizo pesa ambazo hata kwenda out dinner ya maana na mtu wako huwezi.

Unakimbiaje mkopo ambao hata nikitaka kujaza mafuta full tank nitembee weekend tu pesa haitoshi?
 
Back
Top Bottom