Application ya mikopo ya ukopeshaji imegonga mwamba, sijui nilipe huu mkopo au niingie mitini?

Beberu Mwitu

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2019
Posts
495
Reaction score
708
Habari zenu wana JF,

Niende moja kwa moja kwenye mada hii tata;

Ipo hivi, mwanzoni mwa mwezi Septemba nilichacha sana kifedha ikabidi nifanye re-installation ya App moja ya mikopo na kuchukua kiasi cha Sh 200,000. Baada ya hapo update ikaja kuwa mkopo ulipwe ndani ya siku saba ilhali mwanzo walionesha siku 120 kiasi cha Sh 270,000!

Ee bwana nikaamua kuiweka laini kando. Baada ya siku kadhaa nikauza simu yangu ya Samsung nikiwa nimefuta data zote na kununua Iphone mtumba uliorekebishwa. Na hiyo laini niliyoombea mkopo sijaiweka kwenye hii simu ya sasa.

Lakini hivi karibuni kuna mawazo mawili yanayopingana, moja ni la kilokole linaniambia walipe jingine linasema achana nao”.
Nilijaribu kuwacheki ili kujua namna bora ya kuwalipa kwa sababu hiyo app haipo kwenye AppStore, nilipewa njia mbadala ya kuwalipa ambayo ni kwa kutumia menu ya kawaida ya mtandao wa simu.

Pia niliwaomba waondoe wanachoita penalty lakini wakagoma, hapo ndipo lile wazo la usiwalipe likaja tena kwa kasi ya 4GπŸ˜†. kuna muda naingiwa na huruma sana kwani hiyo ni biashara ya watu.

Naomba mnishauri kuhusu hili, niwalipe au nisiwalipe?
NB: wadhamini niliowaweka ni namba zangu mwenyewe ambazo sizitumii kabisa na nilishazipoteza hivyo nimeweka Ghost refereesπŸ™‚

Update:
Siku ya jana tarehe 10, nilijaribu kuwatumia Sh 202,500 kama sehemu ya malipo. Nilifanya hivyo mara 4 na mara zote hizo watu wa mtandao wa simu waliniambia niache ufala. Wakaurudisha muamala huoπŸ˜ƒ.
Halafu cha ajabu mpokeaji wa fedha( kampuni),alikuwa na jina tofauti na aliyenikopesha. Sijui kuwa ni ishu ya utakatishaji fedha au vipi!
 

Attachments

  • IMG_0279.jpeg
    335.1 KB · Views: 49
Lipa deni la watu
 
Kwa kifupi tuu Kama ulitoa permission App ya mkopo kuchukua taarifa zako

Alafu uka Uninstall app Yao bila kublock ukasahau kublock
permision ,clear cache na data , walipe hela zao coz watasumbua Sana ndugu jamaa zako wa karibu kuwa
Wewe ni tapeli


mwisho kabisa kama hukubadilisha password zako za google contacts, Facebook watakuchafua Vijaya mnoo
 
Utapigwa blacklist moja matata sana, siku unaenda Bank unataka mkopo unashangaa wanakuambia wewe sio mlipa madeni, unadaiwa sehemu xxxx na hujalipa.
Tatizo haliji mara moja, siku utakwama tena, ukienda kukopa unaambiwa mambo hukutegemea. Lipa mkopo uwe huru.
 
Nilifanya karibu kila kitu hapo kabla ya kuitoa app. Ni mwezi sasa umeshapita na hakuna walichofanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…