Application ya mikopo ya ukopeshaji imegonga mwamba, sijui nilipe huu mkopo au niingie mitini?

Jitahidi usikimbie deni la 200,00.

Ni aibu sana kukimbia deni la pesa ambayo kwetu wengine hata haitoshi kununua mswaki.

Namaanisha ule mswaki wa kusafishia kinywa kila siku asubuhi na kabla ya kulala ninaotumia hiyo hela huwezi kuupata.
Kwahiyo mswaki ni 200K?
 
PHILIPS Sonicare 9000 Special Edition Rechargeable Toothbrush, Blue/Black, HX9911/92

Currently $193 at Amazon.

You do the math using the current exchange rate.
Ila ya bei za kawaida nayo si ipo?
 
Labda kama unasema uchague kulipa sasa au baadae,
Ila kulipa ni lazima labda usihitaji huduma za kibenki au uwe umekufa. Hapo inayodaiwa ni namba yako ya nida sio line ya simu
 
Kuna wakati ukisoma contents za hawa jamaa inabidi ucheke tu. Sio.kwa kujikweza huku!!
Umeiona hii? Kibongo bongo mpaka mtu unakopa ni dhahiri hali ni tete.
 
Kwa mtu aliyekulia bongo, anayejua maisha halisi ya mtanzania wa kawaida, hayo ni maneno ya kujikweza tu. Laiti wote tumgekuwa mbelez penye fursa na maisha ya juu, huenda ingekuwa sawa ila mtu anajua tunavyoishi, daaah!!
Kibongo bongo 200K ni mshahara wa Intelligent businessman pale lindoni kwake. 120K mshahara wa dada wa usafi nabado unakatwa.
 
Mkuu,

Hujawahi kusikia habari mtu aliukubali umasikini mpaka alipopewa motivation na mtu fulani?

Motivation zenyewe ndiyo hizi sasa.
Hizi za mswaki wa shilingi laki mbili? Huku nna mswaki wangu wa buku tena wenyewe naona ndio bei ghali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…