Kuna wakati bila roho mbaya maono hayawezi kutimia, hakuna nchi imejengwa duniani bila viongozi/ kiongozi mkuu kuwa na roho mbaya.
Fikiria, una plan yakujenga daraja/shule mahala halafu kuna mafala hiyo hela wanaigawana na ujenzi haufanyiki au inafanyika chini ya kiwango.
Fikiria una plan yakujenga bwawa la kuzarisha umeme kwa manufaa ya Taifa lako, halafu ndani ya Taifa lako kuna watu wanapewa rushwa iliujenzi usifanyike na watu waendelee kulinyonya Taifa lako.
Fikiria maendeleo vijijini yanashindwa kufanyika halafu mjini Dar es salaam watu wanakwiba hela la hiyo miradi wanahonga vimada, wananunua magari, wanasomesha watoto Ulaya na kununua majumba SA na Dubai.
Fikiria watu unaowaongoza ni masikini, halafu watu kila siku wanajilipa posho za vikao na kuvifanyia kwenye mahoteli ya kifahari wenye connection nayo na wanalipa hela nyingi.
Fikiria watu unaowaongoza masikini, mashuleni hakuna vitabu, mahospitali hayana dawa halafu watumishi wako wanaanzisha michezo ya mashirika ya umma wanakwenda kucheza sijui mikoani huko, wakitumia mamilioni ya hela kwenye posho na muda wa serikali.
Hebu niambie Kwanini kama kiongozi usiwe na roho mbaya dhidi ya hawa watu?