Arab contractor wanakabidhi bwawa la umeme, watu elfu 11 wameshiriki kulijenga, ndio Mradi Mkubwa wa kiuhandisi kuwahi kutokea Tanzania

Arab contractor wanakabidhi bwawa la umeme, watu elfu 11 wameshiriki kulijenga, ndio Mradi Mkubwa wa kiuhandisi kuwahi kutokea Tanzania

Unajua ni miaka mingapi hii!?

1739695720604.png
 
we itakuwa unaishi burund
Sina kumbukumbu vzr Ila nakumbuka N.Wazir dotto biteko kama alifungua baadhi ya mitambo lakini sio ya bwawa zima na ndomana hata thread hii imeanza kw mwandish kusema soon bwawa lotakabidhiwa Rasmi. Au sijaelewa sehem?
 
Huu ni mradi mkubwa mzuri ila sio wa Sgr.

By the way Sgr imetumia gharama kubwa zaidi ya huu kufika tuu pale Dom.

SGR imetumia gharama ila sio biggest na wala sio complex engineering project. SGR wafanyakazi wachache sana wametumika, na hata vifaa vya kazi ni vichache sana vinatumika. SGR haijaleta raia na wataalamu kutoka nchi nyingi kama bwawa sababu sio complex project.

ukitaka kujua ugumu wa bwawa tazama kampuni za engineering zilivyosaidiana kulijenga pale rufiji,, kuna mwamba anaitwa Dongfeng electric alikuwepo , Power china likuwepo, sino hydro alikuwepo, El sewedy electric alikuwepo, hizo kampuni tu, zote ni kubwa kuliko Yapi merkezi aliyejenga SGR

ujenzi wa SGR hauna tofauti na ujenzi wa tazara ama reli ya mkoloni.. ni kazi rahisi ya engineering kuliko ujenzi wa bwawa

engineering projects huwa zinapimwa kwa numbers na complexity
 
Mh! yani uwe na mradi wa mapesa hivyo halafu usumbuliwe na miundo mbinu basi hukustahili kuwa na huo mradi!, mkuu waafrika tuna mambo ya ajabu sana swala.

wangekuwepo wenyewe walioanzisha mradi hata hilo la miundo mbinu lingekwisha pia, kumbuka tanzagiza moja kati ya sababu kuu ya umeme kukatika ni miundo mbinu ya usafirishaji umeme, umeme mwingi sana unapotea njiani ni kama bomba la la kusafirishia maji lililo na matobo, pressure ya maji kule mwisho kwa en user itapungua au maji kutokutoka kabisa kulingana na ukubwa wa matobo …
 
Muda si mrefu kampuni ya ujenzi inakabidhi bwawa la umeme.

Ujenzi wa bwawa hilo ndio biggest engineering project kuwai kufanya Tanzania na Africa mashariki yote.

1. idadi ya watu 11856 wamefika rufiji na kushiriki kulijenga

2. Raia wa mataifa 56 tofauti wamefika rufiji kushiriki kulijenga

3. Magari na equipment 1681 vimetumika kusaidia ujenzi

4. Masaa milioni 72 yametumika kwenye kazi ya kulijenga

5. Ndio mradi pekee ambao subcontractor tu, alikuwa anapewa kazi na kulipwa zaidi ya trilioni.

6. Ndio engineering project ilioleta mizigo mizito kuliko yote kuwai kufika africa mashariki. unakuta Mzigo mmoja tu una tani zaidi 200, sheria na kanuni za tanroads hawaruhusu kupitisha mizigo mizito sana barabarani ila kwenye bwawa walikaa kimyaa kama hawapo vile. Traffic wakiona gari limebeba mzigo wa bwawa tu hawaombi hata leseni ya dereva maana wanajua kibarua kitaota nyasi

7. ndio mradi pekee ulioonesha kwamba taasisi za serikali zinaweza kufanya kazi kwa spidi maana zilifanya kazi kwa spidi ya hali ya juu, bwawa lipo porini mbugani ila siku ambayo mkataba ulisainiwa, mkandarasi aliwaambia anataka akute maji safi site, umeme uwepo site, hospitali iwepo site

wizara ya maji ilitandika mabomba na kufikisha maji safi site kati kati ya pori fasta fasta wakati Dar tu kuna sehemu kibao maji safi hayajafika kwa miaka 60, tanesco nao walitandika nguzo za umeme na kufikisha umeme site fasta fasta, Tazara na yeye alifufua stesheni ya Fuga na kujenga kota za wafanyakazi wa tazara haraka haraka.


8. ndio mradi pekee ambayo serikali iliziba masikio kelele za wazungu, UN, UNESCO , WORLD BANK waliongea maneno yote ila hakuna kilichobadilika

screen shot kutoka website ya unesco 17 april 2020
View attachment 3237536
Twambie pia kwanini Umeme bado bei juu wakati upo mpaka unamwagika na kukata kata kuko pale pale.

Twambie mradi huu wa matrilioni umeacha trilioni ngapi kwa watanzania walionudaika kwa kazi na biashara
 
Kuna miradi ilikamilika na haikuweza ku-deliver kama ilivyokusudiwa...pesa zilipigwa haswa, mradi chini ya usimamizi wa serikali ya JK, ufadhili wa IMF.

Huu pia, pesa zimepigwa haswaaa, na kama wamefikia hatua ya kukabidhi basi angalau DSM yote na ukanda wote wa pwani tungeanza kuona faida za uwepo wa umeme! Ila ndo unakatika kuliko kawaida.
 
Ni miaka zaidi ya 8000 yani mtoa mada anamaanisha bwawa limejengwa kabla ya Kristu hadi leo alafu anasema limejengwa haraka

unaelewa maana ya person hours kwenye engineering project?
 
Kuna miradi ilikamilika na haikuweza ku-deliver kama ilivyokusudiwa...pesa zilipigwa haswa, mradi chini ya usimamizi wa serikali ya JK, ufadhili wa IMF.

Huu pia, pesa zimepigwa haswaaa, na kama wamefikia hatua ya kukabidhi basi angalau DSM yote na ukanda wote wa pwani tungeanza kuona faida za uwepo wa umeme! Ila ndo unakatika kuliko kawaida.

umeme unakatika sababu ya Transmission na distribution lines, Arab contractor hawakuja kujenga transmission line, hivyo mpaka leo transmission line na distribution line ni zile zile za zamani ndio zinasafirisha umeme wa bwawa, hivyo zinazidiwa nguvu sababu uwezo wake ni mdogo na zimechoka, ni kazi ya Tanesco kubadilisha transimission lines
 

mnakosea jinsi ya ku calculate hizo 72 milion hours.

Person-hour Definition & Meaning​


The meaning of PERSON-HOUR is a unit of one hour's work by one person.

sasa chukua hao wafanyakazi elfu 11 kisha jumlisha masaa yao yote waliyofanyia kazi kila mmoja kwa miaka ya kazi, uone total utapata masaa mangapi
 
Miaka 8217 aisee😄

mnakosea jinsi ya ku calculate hizo 72 milion hours.

Maana ya PERSON-HOUR ni kipimo cha saa moja ya kazi inayofanywa na mtu mmoja.

Person-hour Definition & Meaning


The meaning of PERSON-HOUR is a unit of one hour's work by one person.

sasa chukua hao wafanyakazi elfu 11 kisha jumlisha masaa yao yote waliyofanyia kazi kila mmoja kwa miaka ya kazi, uone total utapata masaa mangapi
 
4. Masaa milioni 72 yametumika kwenye kazi ya kulijenga ( person- hours 72 milion hours)
Dah! Hili bwawa limejengwa kwa miaka laki moja na elfu tisini na saba mia mbili ( miaka 197,200+)🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom