Ardhi ya Tanzania inaendelea kupigwa mnada kwa spidi ya mwanga

Ardhi ya Tanzania inaendelea kupigwa mnada kwa spidi ya mwanga

Kila kitu sio kupinga tu, serikali Ina Nia njema kabisa ngorongoro ikiachwa iendelee kuharibiwa na wamasai basi miaka michache mbele hatutakuwa na ngorongoro
Kama wanyama hai wanapelekewa Uarabuni hai, Patakuwa na utalii hapo, waje kufanya nn.

Nawaombea mabaya yawapate WAOVU wote. Amen
 
Na mama anaupiga mwingi Hana udini Wala ukabila anawahudumia watanzania wote kwa umoja wao
Wewe endelea na mama anaupiga mwingi utakuja kushtuka pamekucha
 
Kama wanyama hai wanapelekewa Uarabuni hai, Patakuwa na utalii hapo, waje kufanya nn.

Nawaombea mabaya yawapate WAOVU wote. Amen
Naungana na wewe kwa moyo wangu wote
 
Tunatambua mchango wa wamasai katika hifadhi yetu kwa miaka mingi, lkn Sasa serikali kwa nia njema imeamua kubadili matumiz ya ardhi Kama sheria inavyoruhusu, ndio maana tunawajengea makazi Safi na salama zaidi
Kwa hiyo malipo yao NI kuwanyang'anya ardhi yao kwa nguvu na kuwauzia waarabu
 
Kila kitu sio kupinga tu, serikali Ina Nia njema kabisa ngorongoro ikiachwa iendelee kuharibiwa na wamasai basi miaka michache mbele hatutakuwa na ngorongoro
Kutakuwa na Pemba pale Ngorongoro?
 
Karl Marx anasema ukitaka kuelewa mgogoro wowote anza na suala la uchumi.

Kilio cha Maasai kule Ngorongoro sio kuhamishwa bali ni suala la uchumi. Kule waliishi kwa boma na wazungu wanaojifunza utamaduni wao wakalipwa, waliuza shanga, waliuza nguo za kimasai kwa wazungu, walilipwa tip kwa kupiga picha na mzungu, waliuza nyama na maziwa, walicheza ngoma zao kwa wazungu wakalipwa, na walifuga ng'ombe na mbuzi, sasa Handeni watapataje pesa nje ya ufugaji? hali zao za kimaisha zitaporomoka sana! pole Maasai nchi yenu imeuzwa!
 
Wanachi wengi hawakumwelewa yule bwana aliposema ipo siku tutapigwa mnada, leo wamasai ardhi yao imepigwa mnada kwa mwarabu.

Yaani anaondolewa Mtanzania kwenye ardhi yake ya urithi anauziwa mwarabu aliyewahi kutuuza Kama ngongwe[emoji16] enzi za utumwa.

Ni ukweli kwamba rasilimali zetu Kama taifa zilishapigwa mnada, si madini,gesi,vitalu, ardhi yenye rutuba n k. Na kwa Sasa visiwa vidogo vidogo vya Zanzibar vinapigwa mnada kwa kisingizio Cha kukodishwa.

Kilichobaki ni wanachi nao kuuzwa kwa Bei ya kuku.

Ngorongoro NI ardhi ya wamasai, tukikubali wauzwe leo kesho ardhi ya mgogo, mnyaturu, mchaga au mhaya itauzwa vilevile.

Raisi Samia na serikali yako acheni kutupiga mnada Watanzania
kumbe wakati mwingine yanakuuma
 
Ni kweli, kwahiyo mwarabu ndio mwenye uwezo wa kuilinda hiyo ngorongoro? Ni lazima Wamasai waondolewe kwa wengine kuuwawa? Kwanini zisitungwe sheria ambazo zingewafanya waondoke wenyewe kwa amani? Mfano ipite sheria hakuna mmasai ataruhusiwa kumiliki ng'ombe zaidi ya 100, na wakati huo huo kila ng'ombe alipiwe kodi kubwa? Ingewekwa kodi ambayo hata ukitaka kumuuza huyo ng'ombe ukifananisha na hiyo kodi ni bora usifuge.

Hii ya kutumia mabavu na kulazimisha waondoke sasa ni kwa faida ya nani? Kibaya zaidi huko wanakopelekwa hakuna hata mazingira wezeshi. Zimejengwa nyumba 2 tatu za kuhadaa umma kuwa wamewekewa miundombinu. Hao Wamasai wakilogwa wakaondoka huko ngorongoro wakaenda huko handeni, watateseka kupita maelezo. Tuna uzoefu na huduma za serikali zinapohamisha watu, hii ni laana ya toka enzi za Nyerere kwenye vijiji vya ujamaa.
Tindo nakuona mstaarabu siku zote, sikujua na wewe unaweza kukamatika katika mtego wa kitoto wa kuamini kweli nchi imeuzwa.

Kinachoendela Ngorongoro kimeelezewa kwa kirefu na kinaendelea kuelezewa kila mahali.

Umewekewa mtego wa wanaharakati na umeuingia mazima.
 
Kama waziri mkuu anaongea uongo wa wazi tena ndani ya bunge, kwanini tusiamini ya kweli ambayo tunayaona, na wakati mwingine ndio yanaletwa na hao wanaharakati? Ni hivi mkuu mimi siamini serikali kwa mambo mengi kutokana na tabia iliyokithiri ya kusema uongo ili kusaka kiki za kisiasa, ama kufunika mambo yaliyo wazi kabisa.
 
Hivi kuandika bandiko unaweza kuthibitisha mahakamani Kama ardhi yetu inauzwa na serikali au unaandika tu?
 
Tindo nakuona mstaarabu siku zote, sikujua na wewe unaweza kukamatika katika mtego wa kitoto wa kuamini kweli nchi imeuzwa.

Kinachoendela Ngorongoro kimeelezewa kwa kirefu na kinaendelea kuelezewa kila mahali.

Umewekewa mtego wa wanaharakati na umeuingia mazima.
Mwambie na msaidie huyo ndugu ili aelewe vizur zaidi
 
Back
Top Bottom