Ardhi ya Tanzania inaendelea kupigwa mnada kwa spidi ya mwanga

Kila kitu sio kupinga tu, serikali Ina Nia njema kabisa ngorongoro ikiachwa iendelee kuharibiwa na wamasai basi miaka michache mbele hatutakuwa na ngorongoro
Kama wanyama hai wanapelekewa Uarabuni hai, Patakuwa na utalii hapo, waje kufanya nn.

Nawaombea mabaya yawapate WAOVU wote. Amen
 
Na mama anaupiga mwingi Hana udini Wala ukabila anawahudumia watanzania wote kwa umoja wao
Wewe endelea na mama anaupiga mwingi utakuja kushtuka pamekucha
 
Kama wanyama hai wanapelekewa Uarabuni hai, Patakuwa na utalii hapo, waje kufanya nn.

Nawaombea mabaya yawapate WAOVU wote. Amen
Naungana na wewe kwa moyo wangu wote
 
Tunatambua mchango wa wamasai katika hifadhi yetu kwa miaka mingi, lkn Sasa serikali kwa nia njema imeamua kubadili matumiz ya ardhi Kama sheria inavyoruhusu, ndio maana tunawajengea makazi Safi na salama zaidi
Kwa hiyo malipo yao NI kuwanyang'anya ardhi yao kwa nguvu na kuwauzia waarabu
 
Kila kitu sio kupinga tu, serikali Ina Nia njema kabisa ngorongoro ikiachwa iendelee kuharibiwa na wamasai basi miaka michache mbele hatutakuwa na ngorongoro
Kutakuwa na Pemba pale Ngorongoro?
 
Karl Marx anasema ukitaka kuelewa mgogoro wowote anza na suala la uchumi.

Kilio cha Maasai kule Ngorongoro sio kuhamishwa bali ni suala la uchumi. Kule waliishi kwa boma na wazungu wanaojifunza utamaduni wao wakalipwa, waliuza shanga, waliuza nguo za kimasai kwa wazungu, walilipwa tip kwa kupiga picha na mzungu, waliuza nyama na maziwa, walicheza ngoma zao kwa wazungu wakalipwa, na walifuga ng'ombe na mbuzi, sasa Handeni watapataje pesa nje ya ufugaji? hali zao za kimaisha zitaporomoka sana! pole Maasai nchi yenu imeuzwa!
 
kumbe wakati mwingine yanakuuma
 
Tindo nakuona mstaarabu siku zote, sikujua na wewe unaweza kukamatika katika mtego wa kitoto wa kuamini kweli nchi imeuzwa.

Kinachoendela Ngorongoro kimeelezewa kwa kirefu na kinaendelea kuelezewa kila mahali.

Umewekewa mtego wa wanaharakati na umeuingia mazima.
 

Kama waziri mkuu anaongea uongo wa wazi tena ndani ya bunge, kwanini tusiamini ya kweli ambayo tunayaona, na wakati mwingine ndio yanaletwa na hao wanaharakati? Ni hivi mkuu mimi siamini serikali kwa mambo mengi kutokana na tabia iliyokithiri ya kusema uongo ili kusaka kiki za kisiasa, ama kufunika mambo yaliyo wazi kabisa.
 
Hivi kuandika bandiko unaweza kuthibitisha mahakamani Kama ardhi yetu inauzwa na serikali au unaandika tu?
 
Mwambie na msaidie huyo ndugu ili aelewe vizur zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…