Ardhi yako ni yako hata bila Hati? Rasimu hii inasema ndiyo, na inaweka Ukuta dhidi ya Unyang'anyi

mrxtz2026

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2026
Posts
609
Reaction score
1,314
Kila mkoa nchini Tanzania una hadithi yake ya ardhi. Kijiji kinachoambiwa kihame kwa ajili ya uwekezaji. Familia inayonyang'anywa ardhi ya mababu kwa sababu haina hati. Mwekezaji wa kigeni anayepewa maeneo makubwa huku wenyeji wakisukumwa pembeni. Swali linalorudia kila mara ni hili: je ardhi ni yangu, au ni ya yeyote mwenye karatasi na madaraka zaidi yangu?
Rasimu iliyopo www.katibampya.com imeshughulikia swali hili kwa undani wa kipekee, na leo napenda kuueleza kwa uwazi.

Kwanza, jambo linalobadilisha kila kitu kwa Wazanzibari wa vijijini na wenye ardhi ya kimila. Rasimu inatambua wazi kwamba ardhi ya kimila, iliyotumiwa na ukoo au jamii kwa kizazi kimoja au zaidi, ina nguvu ya kisheria hata bila hati ya maandishi. Kukosa hati rasmi hakuwezi kutumika kama sababu ya kufuta au kupunguza haki hiyo, ikiwa ushahidi wa matumizi ya muda mrefu, ushuhuda wa jamii, na kumbukumbu za mapokeo unathibitika. Hii ni tofauti kubwa na hali ilivyo mara nyingi, ambapo mtu asiye na hati hukosa msimamo wowote mahakamani.

Pili, ardhi ya vijiji na ya pamoja imelindwa dhidi ya kuuzwa au kuhamishiwa mtu wa nje bila ridhaa ya jamii husika. Hii ina maana kwamba uongozi wa juu hauwezi kuamua peke yake kuikabidhi ardhi ya kijiji kwa mwekezaji bila kuuliza wenyeji. Ridhaa ya jamii ni sharti, si hisani.

Tatu, na hili ni la kina zaidi. Hata ardhi iliyosajiliwa rasmi na Serikali haimpi mtu umiliki kamili, inampa haki ya kukaa. Kwa nini hii ni muhimu? Kwa sababu rasimu inaweka wazi kwamba ardhi yote ya Tanzania inashikiliwa na Rais kwa niaba ya wananchi wote, kama mdhamini, siyo kama mmiliki wa kuiuza apendavyo. Matokeo yake ni makubwa: Serikali haina haki ya kisheria ya kuuza ardhi kwa faida yake yenyewe au kwa manufaa ya kikundi fulani nje ya maslahi ya wananchi wote. Mkataba wowote wa kimataifa unaotoa ardhi kwa mwekezaji bila kuzingatia maslahi ya wakazi na uhifadhi wa mazingira ni batili moja kwa moja.

Nne, jambo hili nalipenda sana kwa kuwa linagusa vizazi vijavyo, si vya sasa tu. Rasimu inaweka wazi kwamba kizazi cha sasa hakina haki ya kumalizia kizazi kijacho ardhi wala uwezo wake wa kuzalisha chakula. Ardhi inayoharibiwa kwa uchimbaji usio endelevu au ujenzi usiozingatia mazingira inakabiliwa na wajibu wa kisheria wa kurejeshwa kwenye hali yake ya asili au kulipwa fidia ya usawa kwa ajili ya kizazi kijacho.

Tano, na hapa ndipo Muhimili wa Nne unapoingia moja kwa moja. Baraza la Usimamizi wa Taifa lina jukumu la kusimamia matumizi ya ardhi na kulinda dhidi ya uvamizi, upokaji na kujinufaisha binafsi. Litaweka daftari la kudumu la usajili wa ardhi zote za mamlaka za nchi, na maeneo yasiyotambulika kwenye daftari hilo yatarudishwa kwenye hifadhi. Kwa maneno mengine, hakuna tena eneo linaloweza "kupotea" kimyakimya kwenda kwa mtu mwenye ushawishi.

Fikiria hivi. Ardhi ya kimila ni kama mkataba wa mdomo uliokaa vizazi vingi, hauandikwi lakini kila mtu kijijini anaujua na kuuheshimu. Mfumo mzuri wa kisheria haupaswi kuudharau mkataba huo kwa sababu tu haujaandikwa. Rasimu hii inajaribu kuufanya mkataba huo uwe na nguvu sawa na hati ya karatasi, mbele ya sheria.

Swali ninalowaachia ni hili: kati ya mifumo yote uliyowahi kuiona au kuisikia ikisimamia ardhi, umewahi kuona moja inayotamka wazi kwamba Serikali ni mdhamini, si mmiliki, wa ardhi ya Taifa? Nawaalika wenye uzoefu wa migogoro ya ardhi, wanasheria wa ardhi, na wananchi wa vijijini kusoma hasa Ibara ya 102(8) na Ibara ya 171(11), na kutoa maoni yao ya kweli kutoka uzoefu wao.

Rasimu kamili ipo www.katibampya.com. Isomeni, ihojini, ikosoeni.
 
Hilo Baraza la usimamizi haliwezi kulinda ardhi wakati wajumbe wake bado wanateuliwa na huyo huyo mdhamini
Big No, katika rasimu hiyo ya katiba, hakuna ibara iliyosema wajumbe wakudumu wa baraza wanateuliwa na Rais wa jamhuri isipokuwa Naibu katibu mkuu wa usalama wa taifa pekee na ni kwa masharti yaliyowekwa kwa mujibu wa katiba yenyewe na kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa taifa.
 
kwani ukiwa na hati ya ardhi , wewe ndiye mmiliki halali?
Ndio, kwa mujibu wa sheria zetu zilizopo hivi sasa, isipokuwa tu pale shaka ya umiliki huo itakapoingia.

Kingine ni kwamba Madaraka ya rais kwa mujibu wa katiba ya mwaka 1977 imeweka nguvu kwa rais kuchukuwa sehemu yako ya ardhi kwa fidia ama bila fidia itakapoitajika.
 
Big No, katika rasimu hiyo ya katiba, hakuna ibara iliyosema wajumbe wakudumu wa baraza wanateuliwa na Rais wa jamhuri isipokuwa Naibu katibu mkuu wa usalama wa taifa pekee na ni kwa masharti yaliyowekwa kwa mujibu wa katiba yenyewe na kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa taifa.
Hata kama ni Naibu Katibu Mkuu wa usalama pekee anayeteuliwa na Rais, pointi yangu bado iko palepale. Kwani huyo Naibu Katibu wa Usalama anaripoti kwa nani?

He reports to the executive branch! Halafu unajua maana ya kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa taifa? Hizo sheria huwa zinatungwa na Bunge linaloongozwa na chama kilichopo madarakani. Structure nzima bado inakuwa inasomeka kiserikali.
 
I think ujasoma bado kwenye rasimu iliyopo kwenye www.katibampya.com.

Naomba nikujibu moja kwa moja na nikutake pia ukife kwenye tovuti hiyo, Kwa mujibu wa rasimu iliyo kwenye tovuti hiyo, Naibu katibu mkuu yupo chini ya baraza la usimamizi wa taifa na yupo chini ya Marais wa baraza la usimamizi wa taifa lakini pia nikutake upite kwenye rasimu na usome masharti ya kuteuliwa kuwa naibu katibu mkuu wa usalama wa taifa hili uone kile ninachomaanisha.

Pili, umesema kuhusu sheria ya usimamizi wa taifa kuundwa na bunge, naomba nikujibu kisomi, na kwa ukweli jinsi ulivyo.
1. Nikikupa mfano wa sheria zilizokuwe hivi sasa kuna sheria ya Tume ya uchaguzi si tu inaandikwa na bunge bali mswada wa sheria hiyo unaandaliwa na tume kisha bunge upitisha au ukataa moja kwa moja bila kuibadirisha, na hapo ndipo mahakama uingia kuangalia uhalali wa kikatiba wa sheria hiyo na ikiwa ni sahihi basi inapita bila hata bunge kuipitisha na ikiwa hipo nje ya katiba inakataliwa na kuundwa mswada mwengine.

2. Mfano niliokupa hapo juu ndio mfano halisi ulio kwenye rasimu kwamba Baraza lenyewe linaunda sheria ya usimamizi wa taifa kama mswada kamili na bunge litapitisha au kukataa na hapo ndipo mahakama inaingia, kitu cha kipekee kwenye rasimu hiyo ni uwepo wa mahakama ya katiba rasmi kabisa kwa kazi hiyo.

Lakini pia nikuombe ukaseome ibara ya 300 chini yake iweka sheria hiyo kama sheria kuu ya taifa na kuweka muundo wa kuandaliwa kwa sheria hiyo.

Umesema pia kwamba baraza litakuwa kama Branch ya serikali, jibu lake ni BIG NO katika rasimu hiyo imeliweka baraza kama chombo huru kuwai kutokea na hili upate majibu hayo kasome ibara ya 98 mbaka ibara ya 116 hili upate majibu wewe mwenyewe kabra ya kuhukumu
 
I think ujasoma bado kwenye rasimu iliyopo kwenye www.katibampya.com.

Naomb nikujibu moja kwa moja na nikutake pia ukife kwenye tovuti hiyo, Kwa mujibu wa rasimu iliyokwenye tovuti hiyo, Naibu katibu mkuu yupo chini ya baraza la usimamizi wa takfa na yupo chini ya Marais wa baraza la usimamizi wa taifa lakini pia nikutake upite kwenye rasimu na usome masharti ya kuteuliwa kuwa naibu katibu mkuu wa usalama wa taifa hili uone kile ninachomaanisha.

Pili, umesema kuhusu sheria ya usimamizi wa taifa kuundwa na bunge, naomba nikujibu kisomi, na kwa ukweli jinsi ulivyo.
1. Nikikupa mfano wa sheria zilizokuwe hibi sasa kuna sheria ya Tume ya uchaguzi si tu inaandikwa na bunge bali mswada wa sheria hiyo unaandaliwa na tume kisha bunge upitisha au ukataa moja kwa moja bila kuibadirisha, na hapo ndipo mahakama uingia kuangalia uhalali wa kikatiba wa sheria hiyo na ikiwa ni sahihi basi inapita bila hata bunge kuipitisha na ikiwa hipo nje ya katiba inakataliwa na kuundwa mswada mwengine.

2. Mfano niliokupa hapo juu nsio mfano halisi ulio kwenye rasimu kwamba Baraza lenyewe linaunda sheria ya usimamizi wa taifa kama mswada kamili na bunge litapitisha au kukataa na hapo ndipo mahakama inaingia, kitu cha kipekee kwenye rasimu hiyo ni uwepo wa mahakama ya katiba rasmi kabisa kwa kazi hiyo.

Lakini pia nikuombe ukaseome ibara ya 300 chini yake iweka sheria hiyo kama sheria kuu ya taifa na kuweka muundo wa kuandaliwa kwa sheria hiyo.

Umesema pia kwamba baraza litakuwa kama Branch
Ya serikali, jibu lake ni BIG NO katika rasimu hiyo imeliweka baraza kama chombo huru kuwai kutokea na hili upate majibu hayo kasome ibara ya 98 mbaka ibara ya 116 hili upate majibu wewe mwenyewe kabra ya kuhukumu
Baraza liandae mswada wenyewe, bunge lipitishe au likatae, alafu mahakama iamue? Unaelewa kweli unachoniambia ?

Huo mzunguko mzima ni recipe for gridlock. Unatengeneza serikali ndani ya serikali. Na huyo Naibu wa Usalama kuwepo hapo, hata kama yuko chini ya marais wa Baraza, kazi ya jasusi ni nini? Ni kulinda maslahi ya aliyempa ajira.
 
BIG NO, hapa tutakuwa tunavutana bila ushaidi kamili wa ibara huku mimi nikikupatia ibara kamili uzisome na uzikosoe hizo ibara zenyewe kwa hoja, pia umesema kazi ya jasusi ni nini...?.
Kwanza kabisa wote tunakubariana kuhusu upelezi ndio kazi yao lakini kwenye rasimu iliyopokqenye tovuti, ndani ya Baraza la usimamizi wa Taifa kuna ofisi ya Tathmini ya usalama wa taifa ambayo kazi yake si ujasusi unaoutambua bali kufanya tathmini ya kile kinachoitwa usalama wa taifa, pia kwa mujibu wa katiba hiyo jsalama wa taifa haujachukuliwa kama ajira bali kama msingi mkuu wa taifa na utawala uliowekwa kwenye sura ya tatu ya katiba yenyewe.

UBISHANI WAKO UNATOKANA NA KWAMBA IBARA NINAZOKUPATIA UNAZITIA KAPUNI KISHA UNAULIZA SWALI AMBALO RASIMU YENYEWE IMELIJIBU MONA KWA MOJA.

kuhusu mahakama kuamua na kudai kwamba pengine sielewi nisemalo naomba nikwambie kwamba Katiba yetu pekee duniani ndio imelipa bunge nguvu kiasi hata baadhi ya hukumu za mahakama kudharauliwa, hili nakuomba ulejee hutuba ya jaji mkuu alipotoa tamko kwamba hukumu ya mahakama inazarauliwa.

Nchi za wenzetu mahakama zake zinakjwa na sberia zao zinazotundwa na wao wenyewe na bunge ukagua kupitia kamati ya kudumu ya bunge ya utawala, katiba na sheria kama ilivyo hapa kwetu.

Soma ibara ya 98 mbaka ibara ya 116 kisha njoo na ukosoaji wako ukikosoa kile kilichondani ya katiba yenyewe.
 
Mkuu, unaandika kwa hisia sana, tulia basi. Shida yako unaitazama katiba kama msahafu ulioshuka mbinguni, mimi naitazama kama chombo cha kisiasa kinachoendeshwa na binadamu wenye tamaa ya madaraka. On paper, kila kitu huwa kinaonekana safi na salama.

Iko hivi mifumo migumu sana huwa inaleta institutional gridlock, mabadiliko ya jina huwa hayabadili asili ya chombo, na taarifa za kiusalama hazijawahi kuwa za wazi, labda nikuulize ni nani anayewafanyia tathmini hao watathmini wenyewe?
 
Kila mkoa nchini Tanzania una hadithi yake ya ardhi. Kijiji kinachoambiwa kihame kwa ajili ya uwekezaji. Familia inayonyang'anywa ardhi ya mababu kwa sababu haina hati. Mwekezaji wa kigeni anayepewa maeneo makubwa huku wenyeji wakisukumwa pembeni. Swali linalorudia kila mara ni hili: je ardhi ni yangu, au ni ya yeyote mwenye karatasi na madaraka zaidi yangu?
Rasimu iliyopo www.katibampya.com imeshughulikia swali hili kwa undani wa kipekee, na leo napenda kuueleza kwa uwazi.

Kwanza, jambo linalobadilisha kila kitu kwa Wazanzibari wa vijijini na wenye ardhi ya kimila. Rasimu inatambua wazi kwamba ardhi ya kimila, iliyotumiwa na ukoo au jamii kwa kizazi kimoja au zaidi, ina nguvu ya kisheria hata bila hati ya maandishi. Kukosa hati rasmi hakuwezi kutumika kama sababu ya kufuta au kupunguza haki hiyo, ikiwa ushahidi wa matumizi ya muda mrefu, ushuhuda wa jamii, na kumbukumbu za mapokeo unathibitika. Hii ni tofauti kubwa na hali ilivyo mara nyingi, ambapo mtu asiye na hati hukosa msimamo wowote mahakamani.

Pili, ardhi ya vijiji na ya pamoja imelindwa dhidi ya kuuzwa au kuhamishiwa mtu wa nje bila ridhaa ya jamii husika. Hii ina maana kwamba uongozi wa juu hauwezi kuamua peke yake kuikabidhi ardhi ya kijiji kwa mwekezaji bila kuuliza wenyeji. Ridhaa ya jamii ni sharti, si hisani.

Tatu, na hili ni la kina zaidi. Hata ardhi iliyosajiliwa rasmi na Serikali haimpi mtu umiliki kamili, inampa haki ya kukaa. Kwa nini hii ni muhimu? Kwa sababu rasimu inaweka wazi kwamba ardhi yote ya Tanzania inashikiliwa na Rais kwa niaba ya wananchi wote, kama mdhamini, siyo kama mmiliki wa kuiuza apendavyo. Matokeo yake ni makubwa: Serikali haina haki ya kisheria ya kuuza ardhi kwa faida yake yenyewe au kwa manufaa ya kikundi fulani nje ya maslahi ya wananchi wote. Mkataba wowote wa kimataifa unaotoa ardhi kwa mwekezaji bila kuzingatia maslahi ya wakazi na uhifadhi wa mazingira ni batili moja kwa moja.

Nne, jambo hili nalipenda sana kwa kuwa linagusa vizazi vijavyo, si vya sasa tu. Rasimu inaweka wazi kwamba kizazi cha sasa hakina haki ya kumalizia kizazi kijacho ardhi wala uwezo wake wa kuzalisha chakula. Ardhi inayoharibiwa kwa uchimbaji usio endelevu au ujenzi usiozingatia mazingira inakabiliwa na wajibu wa kisheria wa kurejeshwa kwenye hali yake ya asili au kulipwa fidia ya usawa kwa ajili ya kizazi kijacho.

Tano, na hapa ndipo Muhimili wa Nne unapoingia moja kwa moja. Baraza la Usimamizi wa Taifa lina jukumu la kusimamia matumizi ya ardhi na kulinda dhidi ya uvamizi, upokaji na kujinufaisha binafsi. Litaweka daftari la kudumu la usajili wa ardhi zote za mamlaka za nchi, na maeneo yasiyotambulika kwenye daftari hilo yatarudishwa kwenye hifadhi. Kwa maneno mengine, hakuna tena eneo linaloweza "kupotea" kimyakimya kwenda kwa mtu mwenye ushawishi.

Fikiria hivi. Ardhi ya kimila ni kama mkataba wa mdomo uliokaa vizazi vingi, hauandikwi lakini kila mtu kijijini anaujua na kuuheshimu. Mfumo mzuri wa kisheria haupaswi kuudharau mkataba huo kwa sababu tu haujaandikwa. Rasimu hii inajaribu kuufanya mkataba huo uwe na nguvu sawa na hati ya karatasi, mbele ya sheria.

Swali ninalowaachia ni hili: kati ya mifumo yote uliyowahi kuiona au kuisikia ikisimamia ardhi, umewahi kuona moja inayotamka wazi kwamba Serikali ni mdhamini, si mmiliki, wa ardhi ya Taifa? Nawaalika wenye uzoefu wa migogoro ya ardhi, wanasheria wa ardhi, na wananchi wa vijijini kusoma hasa Ibara ya 102(8) na Ibara ya 171(11), na kutoa maoni yao ya kweli kutoka uzoefu wao.

Rasimu kamili ipo www.katibampya.com. Isomeni, ihojini, ikosoeni.
Nitarudi
 
Mkuu, unaandika kwa hisia sana, tulia basi. Shida yako unaitazama katiba kama msahafu ulioshuka mbinguni, mimi naitazama kama chombo cha kisiasa kinachoendeshwa na binadamu wenye tamaa ya madaraka. On paper, kila kitu huwa kinaonekana safi na salama.

Iko hivi mifumo migumu sana huwa inaleta institutional gridlock, mabadiliko ya jina huwa hayabadili asili ya chombo, na taarifa za kiusalama hazijawahi kuwa za wazi, labda nikuulize ni nani anayewafanyia tathmini hao watathmini wenyewe?
Asante kwa kujitambulisha kwamba unaitazama katiba kama chombo cha kisiasa, mimi naomba nikujibu jinsi ninavyoitazama katiba kama UTANGULIZI wa rasimu yenyewe na ibara ya 321 iliyofupi kabisa na ukishasoma sehemu hizo, ndivyo ninavyoitazama katiba.

Umeuliza swali kwamba mfanya tathmini amafanyiwa tathmini na nani...? Jibu lako lipo ibara ya 171 iliyoweka idara ya kimahakama ya haki za kibinadamu na Usalama wa taifa.

Ndani ya Rasimu hiyo hipo mahakama ya katiba henye idara tatu za kikatiba moja wapo ni idara ya haki za kibinadamu na usalama wa taifa, kwiyo mambo yote kuhusu usalama wa taifa yanatolewa hukumu ya mwisho kabisa mbele ya mahakama ya katiba.

Pia nakuoba kukumbusha kwamba uzi huu unahusiana na hoja iliyowekwa hapo juu lakini pia sikuzui kuanzisha hoja inayoendana nayo, pia ni muhimu kubishana kwa hoja na pale tunapoweka marejeo husika ni bizuri pia kuyahakikisha kwanza na kuendele na hoja hii itatusaidia kupata picha kamili.
 
Hemu tumia akili yako binafsi kunijibu, usikopi sehemu maana hatutoelewana hapa, duniani kote, hakuna katiba yenye maneno mabaya. Hata Katiba ya Korea Kaskazini ina ibara nzuri sana za haki za binadamu na uhuru wa mahakama, shida huwa ni nguvu ya kisiasa.

Hiyo Idara ya kimahakama ya usalama wa Taifa unayoitolea mfano majaji wake watatoka wapi? Wataishi kwenye sayari nyingine? The moment wanapoteuliwa na mfumo, wanakuwa sehemu ya siasa za nchi tayari

Nikuulize, taarifa za kiusalama zikishakuwa classified, mahakama itajuaje kama kuna ukiukwaji umetokea ili iingilie kati?

Majaji wataenda kupekua mafaili ya siri ya idara ya usalama kwa kutumia mamlaka gani yasiyoingiliwa?
 
Kazi kubwa niliyokuwa nayo hapa ni kwamba wewe unataka maongezi tu ya kawaida mimi nakupa na ibara husika ambazo zina majibu ya maswali yako,

Naomba niendelee kukutaka upitie ibara hizo maana hata haya uulizayo yana majibu ndani ya ibara hizo hizo, nikikupa majibu ya halaka halaka utakuwa umekosa mzizi wa jambo.
 
Ibara haina hayo majibu ya hayo maswali niliyo kuuliza.
 
Back
Top Bottom