Tafuta kitabu cha
James Hadley Chase kinaitwa Dooms Day Conspiracy, ni simulizi lakini
page kumi za mwisho kafanya epiologue inayoelezea Habari za UFO vizuri
sana, namna serikali kubwa zinavyoficha uwepo wa aliens na UFO kwa
kuhofia kuzusha hofu kwa raia. Inshort, kuna viumbe wanaoishi nje ya
dunia ambao wana technolojia kubwa kuliko ya kwetu.. kinachotokea mara
kwa mara vyombo vyao anga vinakuja duniani na inasemekana moja ya jamii
za aliens chombo chao kilidondoka kwenye mashamba mexico, wakulima
waliokiona mwanzoni walisema waliona watu wenye sura za mviringo wakiwa
na rangi ya kijani. Baada ya muda ndege ya kijeshi marekani ikatua na
wanasayansi moja kwa moja wakabeba na kuvipeleka makao makuu ya NASA.
Wanasayansi watano walioshughulia wale viumbe walifanikiwa kugundua
lugha yao, mmoja wao akajaribu kuivujisha siri kwa vyombo vya habari
baada ya hapo haikujulikana hao wanasayansi wamepotelea wapi. Urusi,
Marekani, China, Uingereza na Japan wana hofu Aliens wakipata access
hapa duniani itakuwa ndio mwisho wa ustaarabu wa mwanadamu ndio maana
wanajitahidi sana ku-crack technology yao ili itakapotokea invasion
yoyote tuwe tayari. Lakini all in all kuna siku lazima kitawaka, nna
hamu sana ile ngoma iliyosimuliwa na James Cameron kwenye Avatar iwe
kweli.