Arnold Schwarzenegger: Heaven is 'Fantasy' and 'Nothing' happens when we die

Arnold Schwarzenegger: Heaven is 'Fantasy' and 'Nothing' happens when we die

Kuna sehemu hapo nimetaja sayansi imetoa majibu kuhusu uwepo wa Mungu?

Nime kwambia hivi , Imani ya binadamu ilifeli kuwapa majibu na uthibitisho wa maswali yao yaliyo watatiza.
(mfano wa maswali hayo ni kama, kifo ni nini? Maisha ni nini?)

Waka anza uvumbuzi na ugunduzi wa Kisayansi.
Sawa.
 
Maisha ana formula once ukizaliwa lazima ufe! Utakufaje? ni juhudi zako
Hii hoja hai address point yangu ya kwamba Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hayupo.
 
Yes ana uwezo wa kukupa uhai na kuuchukua mda wowote
Hujathibitisha hata kwamba yupo, usharukia kwamba ana uwezo wa kunipa uhai na kuuchukua wakati wowote?

Unajuaje kwamba Mungu yupo kweli, na hizo habari za kuwepo kwake si hadithi za uongo za watu tu?
 
Hujathibitisha hata kwamba yupo, usharukia kwamba ana uwezo wa kunipa uhai na kuuchukua wakati wowote?

Unajuaje kwamba Mungu yupo kweli, na hizo habari za kuwepo kwake si hadithi za uongo za watu tu?
Unaweza kuthibitisha wewe upo?
 
Unaweza kuthibitisha wewe upo?
Hata mimi nikishindwa kuthibitisha kwamba nipo, hilo halithibitishi Mungu yupo.

Suala ni uthibitisho kwamba Mungu yupo, suala si uthibitisho kwamba mimi nipo.

Usibadilishe hoja kutoka uthibitisho wa kuwapo Mungu kuja uthibitisho wa kuwapo mimi.

Hata mimi nikifa leo nisipokuwapo, kama Mungu yupo, atakuwapo tu, kama hayupo, hatakuwapo.

Sasa, wewe unathibitishaje Mungu yupo?

Unahakikishaje Mungu yupo kweli, na kwamba habari za kuwapo kwake si hadithi za uongo za watu tu?
 
Hujathibitisha hata kwamba yupo, usharukia kwamba ana uwezo wa kunipa uhai na kuuchukua wakati wowote?

Unajuaje kwamba Mungu yupo kweli, na hizo habari za kuwepo kwake si hadithi za uongo za watu tu?
Sio kila kitu ni touchable ni kama jamii forum ipo lakini usha wahi kuiona au kuishika?
 
Unataka kumuona Mungu?
Hapana,

Kuona si uthibitisho wa kitu kuwapo, unaweza kuona kisichokuwepo, halafu usione kilichopo.

Mimi nataka uthibitisho kwamba Mungu yupo.

Wewe unaweza vipi kuthibitisha kwamba Mungu yupo kweli, na kwamba habari za kuwepo kwake si hadithi za kutungwa na watu tu?

Ni hilo tu.
 
Hapana,

Kuona si uthibitisho wa kitu kuwapo, unaweza kuona kisichokuwepo, halafu usione kilichopo.

Mimi nataka uthibitisho kwamba Mungu yupo.

Wewe unaweza vipi kuthibitisha kwamba Mungu yupo kweli, na kwamba habari za kuwepo kwake si hadithi za kutungwa na watu tu?

Ni hilo tu.
Nithibitishie dunia ilitoka wapi, (founder)
 
Nmekwambia utakufaje ni juhudi zako ila Mungu ana kanuni zake ndio maana anawanyeshea mvua hata kina Kiranga wanao mpinga
Huyo Mungu hujathibitisha yupo, ushakimbilia kusema ana kanuni zake.

Unathibitishaje Mungu yupo kwanza, kabla ya kwenda kwenye yeye kuwa na kanuni zake.

Maana, kama hayupo, hawezi kuwa na kanuni zake.

Unathibitishaje Mungu yupo, na kwamba habari za kuwapo kwake si hadithi z auongo za watu tu?
 
Nithibitishie dunia ilitoka wapi, (founder)
Nakwambia hivi, hata nikiwa sijui jibu la swali hilo, kutokujua huko hakuthibitishi Mungu yupo.

Kutathibitisha tu kwamba sijui jibu.

Sasa, wewe unayesema Mungu yupo, ndiye unatakiwa kuthibitisha yupo.

Kama hoja yako ni kwamba dunia imeumbwa na Mungu, thibitisha hilo.

Factually, si kwa mambo ya imani.

Imani kila mtu anaweza kutunga yake.
 
Mpaka sasa hakuna aliyeweza kuthibitisha kuwa Mungu yupo.

Watu wanabishana, wanauana, familia zinatengana, taifa linapigana na taifa, kwa sababu ya tofauti za kidini na mambo ya Mungu.

Hivi nyie mnaoamini kuwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo, hamuoni kwamba utata wa kujulikana Mungu yupo, utata unaosababisha matatizo mengi, vita vya kidini, mufarakano ya nchi na nchi, unaonesha kuwa huyo Mungu hayupo?

Hamuoni kwamba Mungu huyo angekuwapo, kwa kuwa ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote angejifunua ili aeleweke bila shida kwa viumbe wake wote, na angewapa viumbe wake wote uwezo wa kumjua bila utata wala shida?

Hamuoninkwamba uwezekano wa kuwapo huu mjadala tu wa watu wengine kutaka uthibitisho kwamba Mungu huyo yupo ni ushahidi mkubwa sana kwamba huyo Mungu hayupo?

Hamuoni kwamba, Mungu huyo angekuwapo, mjadala huu usingewezekana kufanyika, kwa sababu Mungu angejidhihirisha kwa wazi kwa kila mtu, na kumpa kila mtu uwezo wa kumjua, katika namna ambayo huu mjadala hata tusingejua pa kuuanzia?

Hamuoni kwamba mjadala huu kuweza kuwapo ni ushahidi mkubwa sana kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo?
 
It's better to believe there's a heaven because it's not cost full, than not and you find it....[emoji15][emoji15][emoji15]
If God does not exist, and you pay all your alms money and tithes to the church, believing that you are fulfilling God's wishes, meanwhile God does not exist, you are just being exploited as an ignorant believer to subsidize a luxurious lifestyle of your pastor, this could cost you so much.

So, your premise is very much erroneous.
 
Gari lime tengenezwa na binadamu

Wewe unalazimisha kila kitu kiwe na mtengenezaji si ndio? Tufanye basi binadamu katengenezwa na huyo Mungu.

Kama kila kitu lazima kiwe na mtengenezaji na huyo Mungu lazima awe ametengenezwa, Sasa Mungu ametengenezwa na nani?

Yani wewe unalazimisha binadamu awe na mtengenezaji Lakini una amini Mungu Hana mtengenezaji kwamba alitokea tu from no where!!!!

Kwa nini ushindwe kuamini na ulazimishe Binadamu alitengenezwa na uweze kuamini na ulazimishe Mungu Haku tengenezwa?

Huoni kwamba una ji contradict na msimamo wako wa kwamba lazima kila kitu kiwe na mtengenezaji?
Mungu ametoa vitabu vyake kuwa kamuumba binadamu kama yupo aliyemuumba mungu na yeye atoe vitabu vyake aseme alivyomtengeneza mungu
 
Mungu ametoa vitabu vyake kuwa kamuumba binadamu kama yupo aliyemuumba mungu na yeye atoe vitabu vyake aseme alivyomtengeneza mungu
Ametoa vitabu gani? Cha wakristo au Cha waislam? Ama ametoa vyote? Vipi kuhusu dini nyingine pia nje ya kristo na Islam? Au hizo nyingine ni dini za uongo yako ndio sahihi

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom