Mpaka sasa hakuna aliyeweza kuthibitisha kuwa Mungu yupo.
Watu wanabishana, wanauana, familia zinatengana, taifa linapigana na taifa, kwa sababu ya tofauti za kidini na mambo ya Mungu.
Hivi nyie mnaoamini kuwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo, hamuoni kwamba utata wa kujulikana Mungu yupo, utata unaosababisha matatizo mengi, vita vya kidini, mufarakano ya nchi na nchi, unaonesha kuwa huyo Mungu hayupo?
Hamuoni kwamba Mungu huyo angekuwapo, kwa kuwa ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote angejifunua ili aeleweke bila shida kwa viumbe wake wote, na angewapa viumbe wake wote uwezo wa kumjua bila utata wala shida?
Hamuoninkwamba uwezekano wa kuwapo huu mjadala tu wa watu wengine kutaka uthibitisho kwamba Mungu huyo yupo ni ushahidi mkubwa sana kwamba huyo Mungu hayupo?
Hamuoni kwamba, Mungu huyo angekuwapo, mjadala huu usingewezekana kufanyika, kwa sababu Mungu angejidhihirisha kwa wazi kwa kila mtu, na kumpa kila mtu uwezo wa kumjua, katika namna ambayo huu mjadala hata tusingejua pa kuuanzia?
Hamuoni kwamba mjadala huu kuweza kuwapo ni ushahidi mkubwa sana kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo?