Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Sare sio mbaya sana,maana jamaa wako kwao mkuu...Kuna wengine wanaugulia maumivu yasiyofaa leo,wapo jirani tu hapo...Belo,Manda& the Co...
mkuu sare ya stahili ni mbaya sana na inauma mno.ningesema sio mbaya kama jamaa wangetusumbua toka mwanzo lakini game ilikuwa tuna control na tukashindwa kuimaliza na huu ndio mchezo wetu kila siku.walijifanya wamejifunza kutoka game ya juzi champions ligi lakini this is worse than the game against akmaar.nimechukia mno na hakuna cha kujivunia leo.tunaongoza goli 2 na tushajua matokeo mengine yote alafu tunaacha kuchukua point 3 zote?
hatuko serious kabisa kuhusu kutaka kikombe.
 
Kocha wa Westham anastahili pongezi, amefanya sub za maana sana. Kwa mtindo huu Westham hawashuki daraja mwaka huu. Pole sana Arsenal fans bado mnayo nafasi. Mwaka huu ni mbanano tu hakuna kuachana sana.

SAF baada ya kipigo amesema kwamba 'vumbi litakapotulia wapenzi wa Man u watatambua kwamba ligi inasisimua zaidi timu zinapopoteza point' (in english).
 
Mamaaee ligi hii sasa imekaa kiupande upande yani duh!! Arsenal na Man Utd wamefungwa mechi mbili wamedraw moja Chelsea keshafungwa mbili tayari kutabiri kugumu.
Hao Man City na Spurs siwapi nafasi maana wameshaanza kuchechemea.
 
Mamaaee ligi hii sasa imekaa kiupande upande yani duh!! Arsenal na Man Utd wamefungwa mechi mbili wamedraw moja Chelsea keshafungwa mbili tayari kutabiri kugumu.
Hao Man City na Spurs siwapi nafasi maana wameshaanza kuchechemea.

Huwezi kutabili nini? Hujui kama Chelsea ni mwaka wao huu.....najua hutaki ila siwezi kukusaidia!
 
Matatizo yetu ni yaleyale tumeshindwa kuzuia ushindi wa mabao 2 ikiwa zimesalia dakika 20, imetokea mara nyingi kwa Diaby na Song kusababisha freekick maeneo ya hatari, nimekuwa na wasiwasi na tatizo la Mannone kutema mipira ndani ya box, punch zake hazina nguvu na Gallas ni mzito wa ku-react na rebounce balls. Tusubiri Yosso watufurahishe dhidi ya bwawa la maini. Kazi ipo J'mosi na SPUDS.
 
...mechi ya pili muhimu tunapoteza pointi mbili muhimu, aaaarrrggghhhh!
 
RvP-celeb_2376843.jpg
 
Jana Arsenal wamechemsha sana. Unajua hata West Ham walikuwa wakitafuta namna ya kupata mipira ya adhabu na karibu na eneo la hatari na wakapata.

Calton Cole nae alikuwa akijiangusha huku na kule kutafuta "unnecessary fouls" badala ya kumuonesha Fabio Capello ni jinsi gani anaweza kuwa mshambuliaji mzuri wa Uingereza.

Ila kocha wa West Ham nae alipomuingiza Alessandro Diamanti ndie akaleta hamasa kwa kuumiliki mpira kila alipoupata na kuwapa moyo West Ham.

Lakini kwa kuwa ni ugenini si mbaya ingawa tulitaka maximum points. Tuna 13 point kutoka katika possible 18 ambazo zingekuwa bomba sana.

Kuanzia Jumatano tuna mechi tatu nyumbani, na Liverpool (Carling Cup)Emirates, halafu Jumamosi tunawakaribisha Tottenham na tarehe 4 November tunaanza na waharibifu AZ Akmaar kwenye Champions League.

Kama kawaida ya mzee Wenger Jumatano atachezesha timu ya wadogo, kwasababu ya mechi ya jumamosi na Spurs.
 
Matokeo sio mabaya, the only thing is for Wenger and team to be positive, focus on the next games.
 
Tena walivyofanyiwa hawa jamaa hadi raha, kuna wakati huwa nashindwa kuelewa man u wanaweza vipi kuzifunga timu nyingine.
Kila mtu ana kibonde wake, bora wameshinda maana kibarua cha Benitez kingeota nyasi
 
...mchekea hao,

..hata sisi tuliwapiga mengi hao...sita tu!

Tulipowapiga 5 mtungi vijana wa Sam Allardyce, ulisema maneno hayo hapo juu.

...mechi ya pili muhimu tunapoteza pointi mbili muhimu, aaaarrrggghhhh!

Sasa na nyinyi mkikutana na vibonde mnagawana point!!! Ni aibu na noma, ndio maana hivi sasa hatumuangalii nyani usoni; tunakandamija tu hadi kieleweke 09/10. 😀 😀
 
Tulipowapiga 5 mtungi vijana wa Sam Allardyce, ulisema maneno hayo hapo juu.



Sasa na nyinyi mkikutana na vibonde mnagawana point!!! Ni aibu na noma, ndio maana hivi sasa hatumuangalii nyani usoni; tunakandamija tu hadi kieleweke 09/10. 😀 😀

AljuniorTz hats off to you man,
Come January African Cups of Nations...
Drogba, Kalou, Essien, Obi Mikel safarini...😀

Anyway,...
Namuonea huruma sana dogo Vito Mannone...
'Kismeti' kishaota majani, Almunia na Fabianski
wanarudi kwenye nafasi zao...!
 
Back
Top Bottom