Arsenal (The Gunners) | Special Thread


Shukran mkuu nilikuwa sijatembelea tovuti hio.

Kwa hio timu itakuwa kati ya zifuatavyo:

Almunia, Sagna, Gibbs, Toure Sylvester,Diaby,Walcort,Fabregas,Van Persie Nasri na Adebayo.

Au Denilson anaweza kumbadilisha Diaby na Bendtner kumbadilisha Ade.

Na watacheza system yao ya 4-4-2
 
Dah! hii mechi nitakuwa kwenye paper. Ila nitaicheki recorded. Masanilo anaweza fikiri nimemkimbia jamvini. Go go Gooners!
 
Na wasichana wa Arsenal wameshinda kombe la FA.

Wakicheza mtindo uleule wa pasi za chini na kupanga mashambulizi kutoka kwenye backline ya ulinzi, Arsenal hawakuchukua muda sana kufunga goli la kwanza katika dakika ya 32 liliofungwa na Katie Chapman baada ya mpira uliopigwa awali na Laura Basset kumshinda kipa wa Sunderland.

Baada ya mapumziko mchezo ulikuwa wa pasi za hapa na pale na timu zote zilijaribu mashuti na kusogea langoni mwa kila mwenzie.

Na katika dakika ya 90 msichana Kim Little nae akaifungia Arsenal goli la pili baada ya move nzuri baina ya viungo wa Arsena waliongozwa na Rachel Yankee ambae pia ni mshambuliaji wa pembeni wa timu ya taifa ya wanawake ya Uingereza.

Sunderland walipata goli la kufutia machozi lililofungwa katika dakika ya nyongeza mfungaji akiwa msichana Kelly McDougall ambae aliunganisha cross ya msichana Demi Stokes.

Ulikuwa ni mchezo mzuri kutizama na labda umeleta baraka kwa wavulana wa Arsenal hio kesho.
 
Last edited:
...Van Persie...aaa aaaaaaa
Goooooooooooooooooooooooooooooool !!!

....ala! kumbe 'naota', ...masaa yanakaribia wazeeeeeeee!

ha ha aa

πŸ˜€
 
Leo lazima mtoke na kesho msikimbie
 
...nawahakikishia, leo tutabanana humu humu! asitoke mtu leo πŸ˜€ kazini nisha 'call- a sickie!'...

"asie mwana aeleke jiwe!!!"
 
Kesho ni 2-0 Go go Gooners! The Bluez najua daraja limeshavunjwa tayari na the trinity strickers of Barca.

Shadow!wewe sema matokeo yoyote kwa mechi ya kesho ila elewa Chelsea anacheza fainali,siwezi jua tutapita kwa goli ngapi kwa hiyo club bora ya dunia msimu huu,ila nasikitika kuwaambia ya kwamba Barca hatutamwona Roma.kama itakuwa 5-4 au 9-8 mimi sijui but at the end of the day Chelsea will play final game at Rome
For today!kama Arsenal wakitulia watashinda 3-1,ila Mashetani wakibana na Ade akashindwa kulenga goli,mechi itaenda Extra time baada ya ushindi wa goli 1-0 watakaoupata Arsenal.
All the Best Bello!sisi tuachia hao vicheche wa kiispaniola tuwaoneshe mji wa London ilivyo.
 

Mkuu Kisale,

Nimekupata. Kesho tutakuwa hapo darajani. Kazi kwenu na hao trio strickers. Kesho isije ikawa wamebana wameachia 3-0.
 
Wapenzi wa Arsenal leo kaeni mkao wa kula πŸ™‚ Leo tunampiga bao 2 kwa bila SAF na MANU watuni Manchester wakkapange mikakati ya kuwazuia L'pool wasiwanyang'anye tonge lao mdomoni.
 
Wapenzi wa Arsenal leo kaeni mkao wa kula πŸ™‚ Leo tunampiga bao 2 kwa bila SAF na MANU watuni Manchester wakkapange mikakati ya kuwazuia L'pool wasiwanyang'anye tonge lao mdomoni.

BAK

Impossible things do happen!
 
Mbu,BAK na Shadow!...

Naombeni tu leo msije mkapata midadi mpaka mkaparamia screen zenu!..Haya, naona masaa yanakatika..Leo ni leo! All the best
 
Mbu,BAK na Shadow!...

Naombeni tu leo msije mkapata midadi mpaka mkaparamia screen zenu!..Haya, naona masaa yanakatika..Leo ni leo! All the best

BJ wasalaamu!

Hakuna cha mdadi wala nini! . BJ, Leo naomba umwangalie kwa makini mtafuna "big G" anavyocheza lizombe au Sangula! bila kujijua...
 
BJ wasalaamu!

Hakuna cha mdadi wala nini! . BJ, Leo naomba umwangalie kwa makini mtafuna "big G" anavyocheza lizombe au Sangula! bila kujijua...

Shadow!

Nina wasiwasi na taya zake tu japo ngome yake imara!..Leo siongei sana, baada ya mechi ndo mambo yote jamvini. Kama vile nakuona,umeshajipangia magoli ya arsenal dhidi ya man u..he he! Ushabiki una raha yake ila kufungwa kunauma kweli tena mechi muhimu..
 
Ikawa jioni ikawa asubuhi..........! or hayawi hayawi.......! Welcome on board Emirates!
 

BJ, Leo kwa raha zetu. Bunduki kwa kwenda mbele. Van Parsie na Bendner ndo watakaomaliza kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…