Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Timu nzima maumbwa tu hayo.
 
Ni maajabu haya, Raheem ni miaka mingi imepita toka aondoke liver nashangaa leo kumkuta arsenal nilitegemea awe IPSWICH huko na sio timu kubwa kama arsenal
Mimi nilijua kuwa alishastaafu mpira zamani sana. Yani asenyeto ni timu la kutupiwa takataka zilizoshindikana kwenye team nyingine kama hao kina Odegaard, Jesus, Havertz, Sterling, Timber n.k
 
Hili goli ambalo mpira uliufuata mkono wa Kai haina hata haja ya kusumbuana. Mechi imeshaisha hata kama ikaonekana ni kweli zaidi ya kugewa barua ya kuombwa msamaha hakuna jipya.

Kilichotokea kimeendeleza ambacho tunakiona mara nyingi. Weka Partey RB observe unavyoshindwa kusecure points 3. Kipindi fulani hivi wakati liva ipo on fire inamiliki mpira mpaka 80% nikawa nasema kwamba tunateseka dhidi ya liva kwakua Arteta ana tabia kama ya Wenger.

Ilikua haijalishi anakutana na mpinzani gani Wenger alikua anataka acheze sexy football huku anascore. Arteta aliwahi kufanya defense iliyowahi semwa haifundishiki kua ya pili kutoruhusu magoli mengi. He did it with back 3.

Kama hatuna RB na inatusumbua hiyo ishu kwanini isichezwe back 3. Nimeona anasema kikosi ni kidogo na wanacheza kila baada ya siku 2. Ok sawa, nani ambaye hachezi kila baada ya siku 2?.

Ratiba hua inatoka ya mwaka mzima. Hakujua hili swala?
 
Ina maana ukuona mkono ulivyobadili uelekeo wa ule mpira au ubishi tu?
Naelewa kwa nini kila mtu anasema hivyo kwa sababu inaonekana kama ni hivyo ila ukweli ni ilikuwa tumbo. Hata ile replay ya mwisho waliyorudia ilionyesha kuwa siyo handball na commentator akasema hivyo. Ila tayari VAR walikuwa wameshakataa goli. Mimi niliona siyo handball tangu mwanzo kabisa. Ila ndiyo hivyo imeshatokea.
 
Aisee makocha wa Kihispania wana viburi sana.. Thomas Partey kama right back na kila siku inatugharinu sana, ukiacha hilo lakini pia ukiangalia hizi sajili za reject wa Chelsea ambazo tangia mwanzo ziliwashangaza pundits wengi walioamini Arsenal sio sehemu tena ya takataka unakuja kuona uondokaji wa Edu Gaspar Arsenal hakukuwa kwa kawaida kama tunavyoaminishwa. Kuna kitu hakipo sawa naamini Edu alikuwa hakubaliani navyo
 

Kweli. Tuachane na yaliyopita. Ila kwa jana nasema ni yale yale ya sisi kukosa kidogo na wao kupata. Je Partey angewahi kidogo au Timber angekuwa RB ile cross ya goli la kwanza ingezuiwa? Haya cross ilipigwa ila...je Merino angefikisha mguu nusu sekunde kabla si Tielemans asingepata header?
Ok, Tielemans amepata header ila kidogo tu Raya aokoe....au je Raya angetokea kuclaim ile cross...? Mambo yote yamekaa sawa Villa wakapata lile goli ila wangeweza kukosa kimoja kati ya hivyo vingetokea. Marubani wanaita hii 'Swiss Cheese Model'.

Goli la pili pia, Havertz angeugusa kidogo zaidi ule mpira, Watkins hafungi. Au Raya angeiclaim ile cross...?

Lakini kwa kweli kwa game ya jana simlaumu sana Partey kwa position yake maana naweza kusema ni lile goli moja la kwanza alichelewa kuzuia cross ila mengine yamgefanyika kuzuia goli.
 
Star wa timu odegaard eti ndio muchukue ubingwa 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Partey kashacheza CB mara kadhaa msimu uliopita. DM kucheza nafasi ya defender siyo jambo la ajabu ila kwa Arsenal ya sasa ukimtoa Partey katikati ndiyo unakuta CMs/DMs wa timu pinzani wanaweza connect vizuri tu kuanzia kati mpaka golini.

All the while unaona katikati panakua location average zaidi. Situations zote ulizoelezea zingeweza saidia but zingefika huko kote kama kocha angefanya game management?

Ugumu niliouona ni kwamba unaona kabisa unahitaji sub lakini ukiangalia benchi huoni sub unaifanyia kwa nani. Ndiyo mwisho unasub Sterling sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…