Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Afisa Upelelezi Wilaya ya Arusha Mjini, Omary Mahita anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumpiga hadi kumvunja mguu mtuhumiwa wakati wa mahojiano akiwa kituo cha polisi.
Askari huyo anatuhumiwa kumvunja mguu wa kushoto Peter Charles (21), mkazi wa Daraja II, jijini Arusha Juni 6, 2024.
Akizungumzia tukio hilo leo Alhamisi Agosti 15, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema wanamshikilia ofisa huyo wa polsi na kwamba uchunguzi umeshaanza na endapo atabainika kuwa na kosa, atachukuliwa hatua za kisheria.
"Ni kweli hilo tukio liko ofisini kwangu na tumeanza uchunguzi tangu Agosti 8, 2024 nilipopata taarifa kwa simu kutoka kwa ndugu wa huyo kijana akimtuhumu askari wangu kumpiga hadi kumvunja mguu,” amesema Masejo alipozungumza na Mwananchi.
Mwananchi