Arusha: Afisa Upelelezi (Omary Mahita) akamatwa kwa tuhuma za kumvunja Mguu raia

Arusha: Afisa Upelelezi (Omary Mahita) akamatwa kwa tuhuma za kumvunja Mguu raia

"Tumeanza uchunguzi"
"Nilipopata taarifa kwa simu"
"Kutoka kwa ndugu wa huyo kijana"
"Wakimtuhumu"
"Kumpiga hadi kumvunja mguu"
POLISI........POLISI.........POLISI.........
TUNA D 2 ........
Jeshi unajaza form 4 failure unategemea nini?
 
...uchunguzi umeshaanza na endapo atabainika kuwa na kosa, atachukuliwa hatua za kisheria.
Uongo huu,
Kama daktari amethibitisha mguu umevunjika, na mvunjaji anajulikana kuwa ni huyo Mahita wanachunguza nini?!!
Watalindana tu hao
 
Namkumbuka huyu enzi za kesi ya mbowe alitajwa sana mahakamani mtesi wa watuhumiwa
 
Afisa Upelelezi Wilaya ya Arusha Mjini, Omary Mahita anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumpiga hadi kumvunja mguu mtuhumiwa wakati wa mahojiano akiwa kituo cha polisi.

Askari huyo anatuhumiwa kumvunja mguu wa kushoto Peter Charles (21), mkazi wa Daraja II, jijini Arusha Juni 6, 2024.

Akizungumzia tukio hilo leo Alhamisi Agosti 15, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema wanamshikilia ofisa huyo wa polsi na kwamba uchunguzi umeshaanza na endapo atabainika kuwa na kosa, atachukuliwa hatua za kisheria.

"Ni kweli hilo tukio liko ofisini kwangu na tumeanza uchunguzi tangu Agosti 8, 2024 nilipopata taarifa kwa simu kutoka kwa ndugu wa huyo kijana akimtuhumu askari wangu kumpiga hadi kumvunja mguu,” amesema Masejo alipozungumza na Mwananchi.

Mwananchi
Matukio kama haya kwa kweli yanasikitisha sana. Hayatoi picha nzuri kwa nchi yetu. Mtuhumiwa anayehojiwa, justification ya kuvunjwa mguu kwenye kituo cha polisi inatoka wapi au pengine mimi ni ignorant wa criminal interrogation?
 
Afisa Upelelezi Wilaya ya Arusha Mjini, Omary Mahita anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumpiga hadi kumvunja mguu mtuhumiwa wakati wa mahojiano akiwa kituo cha polisi.

Askari huyo anatuhumiwa kumvunja mguu wa kushoto Peter Charles (21), mkazi wa Daraja II, jijini Arusha Juni 6, 2024.

Akizungumzia tukio hilo leo Alhamisi Agosti 15, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema wanamshikilia ofisa huyo wa polsi na kwamba uchunguzi umeshaanza na endapo atabainika kuwa na kosa, atachukuliwa hatua za kisheria.

"Ni kweli hilo tukio liko ofisini kwangu na tumeanza uchunguzi tangu Agosti 8, 2024 nilipopata taarifa kwa simu kutoka kwa ndugu wa huyo kijana akimtuhumu askari wangu kumpiga hadi kumvunja mguu,” amesema Masejo alipozungumza na Mwananchi.

Mwananchi
Alijikuta Jack Bauwa sio!?
 
Hii nchi inachekesha sana sio siri

Inspector wa Polisi anakiri hilo tukio limetokea na Wanamshikilia Askari huyo THEN anasema tena Uchunguzi unaendelea

Unaendelea ili wagundue nini tena?
Ni vichekesho kwa kweli,
Wanaweza kumkamata mtu kwa cybercrime kwa alichoposti mtandaoni kuhusiana na mambo ya siasa halafu wakasema uchunguzi unaendelea na wakaenda kumpekua hadi nyumbani kwake!
 
Kuna vitu watu wanafanya, hukumu ya kweli watakutana nayo mbele za haki wakishakufa. Tusijisahau kwa vyeo tunavyopewa wakuu
 
Back
Top Bottom