Arusha, amuua kaka yake kwa kisu baba yake akishuhudia

Arusha, amuua kaka yake kwa kisu baba yake akishuhudia

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Kijana James mwenye umri wa miaka 16 anatuhumiwa kumuua kaka yake anaitwa Zakayo huku baba mzazi akikiri kushindwa kuwaamua ndugu hao wawili waliokuwa wakigombana kisa mifugo.

Mimi naitwa Paulo Sindio, ni baba mzazi wa watoto hao, walianza kugombana mbele yangu kisa kikiwa ni uswagaji wa mifugo kurudi porini, wote ni Watoto wangu wa mama mmoja.

Akielezea tukio hilo, Paulo amesema: “Walikorofishana baada ya mkubwa kumwambia mdogo kuwa anatakiwa kwenda kuswaga mifugo kauli ambayo ilipingwa na James na baada ya muda wakaanza kupigana.

“Walipigana, mimi nikanyanyuka kwa ajili ya kwenda kuwaamua, kumbe mwenzake tayari alikuwa ameshamchoma kisu kwenye moyo, tulivyompeleka hospitali ikakutwa ameshafariki.

“Sina la kusema, wazee wa ukoo wapo wataamua wenyewe, sina la kufanya, na sijui alipo, kama ameenda kujiua au la sijui alipo. Polisi tayari wana taarifa na wanalifuatilia.”


Source: Globaltv
 
Hii roho ya mauaji Mungu atunusuru nayo

Shetani ameamua kututumia na atutumie tena


Kuna tatizo kubwa sasa katika taifa hili.
Kuna hika imefanyika katika awamu hii?
Roho ya uuaji imetawala taifa

Tuombe sana na kufuata mapenzi ya Mungu ili kuishinda roho ya mauti inayotembea kwa kasi sana ili kushindana na roho ya uhai roho ya Mungu. Yaani kuzimu imefungua mdomo kumeza... tuombeane rehema za mungu

Ufunuo 6:4
"Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa."
 
Back
Top Bottom