ARUSHA: Askari Polisi 7 waliombambikia pembe za ndovu Prof. Justin Maeda na kuchukua milioni 100 wafukuzwa kazi, Profesa afunguka

ARUSHA: Askari Polisi 7 waliombambikia pembe za ndovu Prof. Justin Maeda na kuchukua milioni 100 wafukuzwa kazi, Profesa afunguka

Usa sio kama Tanga. Tanga ukiwaambia takukuru mambo yako wanamtafuta mlengwa na kula hela. Ukikutana na mlengwa anakuambia kila ulichosema huko. Jamani jamani Tanga eeeee Mungu waonee watu wako huruma. Japo mkuu wa takukuru alisimamishwa kazi lakini hakuna jipya sana. Hongereni takukuru huko Arumeru.
Sio Tanga tu Mkuu, hata Njombe ni hivyo hivyo yaani. TAKUKURU ya huko ukiwapatia tu taarifa za MHALIFU, wanaungana naye na kupiga pesa huku wewe mshitaki ukiachwa SOLEMBA. CCM imeharibu sana nchi hii.
 
Kila mtu angekuwa anakomaa hivi, rushwa ingepungua.

Tatizo wanapata kichwa kwa kuwa kuna watu wengi wanalipa.

Polisi wamekuwa majambazi.
Shida iko huko TAKUKURU bosi, mtu akipeleke malalamiko wanaungana na MHALIFU kupiga hiyo pesa. Mfano ni hapa TAKUKURU Njombe, washenzi hawa wanakula milungula kama hawana akili vile. Haya MAGENGE ya CCM ni vyema katiba mpya ikayafutilia mbali.
 
Sio Tanga tu Mkuu, hata Njombe ni hivyo hivyo yaani. TAKUKURU ya huko ukiwapatia tu taarifa za MHALIFU, wanaungana naye na kupiga pesa huku wewe mshitaki ukiachwa SOLEMBA. CCM imeharibu sana nchi hii.
Sijui watu watakimbilia wapi
 
Shida iko huko TAKUKURU bosi, mtu akipeleke malalamiko wanaungana na MHALIFU kupiga hiyo pesa. Mfano ni hapa TAKUKURU Njombe, washenzi hawa wanakula milungula kama hawana akili vile. Haya MAGENGE ya CCM ni vyema katiba mpya ikayafutilia mbali.
TAKUKURU Tanga wanakalia kesi miaka nenda rudi
Wale wanaotuhumiwa wanakutana nao police mess au kwenye hoteli
 
Askari Polisi saba wakiwemo watano wa kituo cha Polisi Usa Wilayani Arumeru Mkoani Arusha na wawili wa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha wamefukuzwa kazi kwa fedheha kwa kosa la kushawishi na kuomba rushwa ya shilingi milioni 100.

Wiki iliyopita Kamanda wa TAASISI ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Nchini {TAKUKURU}Mkoani Arusha,James Ruge alikiri kuwakamata askari hao kushawishi na kupokea kiasi hicho Cha fedha ili wasimfungulie Kesi ya uhujumu uchumi ambapo angefia gerezani.

Hata hivyo Ruge alisema uchunguzi wa kesi hiyo bado haujakamilika na ukikamilika atatoa taarifa kwa vyombo vya Habari juu ya makasa mzima.

Vyanzo vya Habari vilisema kuwa mienendo ya mashtaka ya kijeshi ya kipolisi ilifanyika katika tarehe Aprill 22,23,24 na tarehe 25 mwaka huu , ambapo Askari hao walifukuzwa kazi rasmi ndani ya jeshi la polisi na sasa wanasubiri kushitakiwa katika Mahakama za kiraia wakati wowote.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo alipoulizwa juu ya jeshi hilo kuchukua hatua hizo alisema kuwa hayo ni mambo ya ndani ya Polisi na sio rahisi kutolewa hadharani kwani ni kinyume na maadili ya kazi.

Naye mhanga wa tukio hilo ambaye ni mfanyabiashara wa mji wa Usariver,Profesa Justin Maeda{77}akizungumza nyumbani kwake katika Kijiji cha Nshuku kata ya Nkoaranga wilayani Arumeru alisema pamoja na mkasa wote alioupata na kuishukuru Polisi kwa hatua walizochukua ila amesikitishwa na kitendo cha polisi hao kukiuka maadili ya kazi na kuomba rushwa katika kituo cha Polisi Usa hatua ambayo ilimshangaa na kushindwa kujua OCD na OC CID washindwe kujua tukio hilo.

Profesa Maeda ambaye alianza kufundisha UDSM Mwaka 1970 na kuwafundisha viongozi wengi wa serikali kabla ya kuwa Mshauri Mkuu wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1981-1985 Ikulu sasa ameanza kuamini maneno ya watu wa Usa kuwa ndani ya kituo cha polisi Usa kinanuka rushwa na kuna askari wa kituo hicho kitendo cha upelelezo ni miungu mtu kwani wako hapo kwa miaka mingi sasa wamejivika ufalme wa kuomba kiasi chochote cha rushwa ndani ya kituo mhicho bila kuogopa chochote.

Alisema kama yeye amebambikiwa kesi ya nyaraka za serikali na kuchomekewa shambani kwake na kutakiwa kutoa rushwa ya shilingi milioni 200 kabla ya kufikia makubaliano ya shilingi milioni 100 kuna raia gani Arumeru wameshafanyiwa unyama wa aina hiyo kwani hiyo ni hatari na viongozi wakuu wa polisi Mkoani Arusha na Makao makuu wanapaswa kutupia macho zaidi kituo hicho maana dhuruma na uhuni umekithiri kupita kiasi hivyo hatua zinapaswa kuchukuliwa sasa.

Profesa Maenda ambaye ana Mke na Watoto watatu ambao wote wako nje ya nchi alisema polisi hao ambao walikuja nyumbani kwake na gari mbili za polisi marchi 19 mwaka huu majira ya kati ya saa 7 mchana na saa 8 wakiwa wamejaa kwenye gari na wakiwa na silaha na gari ndogo aina ya Rv4 ambayo hakufanikiwa kushika namba walijitambulisha kuwa ni polisi ya Us ana makao makuu na alimtambua mmoja{jina tunahifadhi} wameagizwa kwenda kwake kupekua kwa kuwa wanataarifa za kiitelejesia kuwa anafanya biashara ya nyara za serikali ikiwemo meno ya tembo na Ngozi za chui.

Alisema kwa kuwa hajawai na hajui kitu kinaitwa Nyara za serikali na hajawahi kufanya biashara hiyo aliwaruhusu kufanya upekuzi lakini cha kushangza hawakufanya ndani ya nyumba bali walikuwa wakipita nje ya kwenda moja kwa moja shambani kwenye mizinga ya nyuki.

Profesa ambaye ameshafanya kazi UN hususani UNICEF nchi mbali za kiafrika na kumalizia nchi ya Zimbabwe mwaka 2002 alion aaskari mmoja akichukua mzinga na kutoa ndani ya mzinga kitu alichodai ni meno ya tembo na kusema hicho ndio kitu walichokuwa wakikitafuta.

Alisema kuwa yeye alisema shambani kwake hukaa zaidi ya miezi miwili au mitatu kuingia hivyo aliwauliza askari hao hii imeletwa na nani kwani hajawahi kufanya biashara hiyo ila alijibiwa na askari hao kuwa hiyo imekula kwake kwani hii ni kesi ya uhujumu uchumi na angefungwa Maisha hivyo anatakiwa kuweka mambo sawa.

Mzee huyo ambaye isema alistaafu miaka ishirini iliyopita alilipwa kiinua mgongo chake{PENSHENI} cha kiasi cha shilingi milioni 74 na kuweka benki ya CRDB na NMB alichukuliwa hadi kituo cha polisi Us ana kuanza kuchukuliwa maelezo na kuombwa rushwa ya shilingi milioni 200 wakati akitoa maelezo.

Profesa alisema yeye aliwaambia kuwa jana yake yaani marchi 18 mwaka huu alikwenda benki na kuchukua kiasi kidogo cha pesa hivyo kiasi hicho hana na kuwataka wapokee milioni 100 na ndipo alipokwenda benki akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi na kuchukua shilingi milioni 74 na baadae alikwenda dukani kwa mdogo wake hapo Usariver na kuchukua kiasi cha shilingi milioni 30 na zote aliwapa polisi katika kituo cha Usa kwani rushwa ilifanyika hapo.

Alisema na kuiomba serikali iweze kumrudishia kiasi cha pesa yake kwani ni kiunua mgongo cha utumishi wake wa kazi wa miaka mingi kazi.

Mwisho


Jeshi la Polisi kwa ujumla limeoza,it needs complete overhaul.Mbona wanasema wazi kuwa rushwa ni haki yao kwa kuwa wanaweza kuitwa kufanya kazi anytime.Huwa nawauliza,kwani mlipokubali kazi ya uaskari si mlijua nature of work.Wanabaki wana-kenua tu, wala hawana majibu.
 
Huyo Prof. naye TAKUKURU wamfungulie mashitaka kwa kushawishi kutoa rushwa(Corruption transaction) kama alikuwa hausika kwanini aogope kufikishwa mahakamani ili mahakama itoe maamuzi kama alibambikiwa kesi au la, hayo meno ya kwenda kumbambikizia yeye hao askari waliyatoa wapi kama si walipata taarifa kutoka wa raia wema kuwa kuna pembe za ndovu shambani kwa huyo mzee.

Jeshi la POLISI na TAKUKURU wachunguze account za huyo mzee na wapime biashara zake kama kwa haraka tu ametoa milioni mia inatia shaka.Kosa la hao askari ni kukubali kupokea rushwa baada ya kushawishiwa na mtuhumiwa.
Una Changamoto ya uelewa
 
Wakomae wapi wewe kibatala ni mwizi tu km wezi wengine wa serikali.hapo hiyo kesi nenda rudi kwake yeye ndio anataka posho.
Bila kesi huyo jamaa hali.
Kwa hiyo asilipwe kwa kazi yake au?Hiyo ni kazi kama kazi nyingine tumia akili
 
Sijui watu watakimbilia wapi
Tungekua na serikali imara ingefuatilia malalamiko yote yaliyopo kwenye ofisi za TAKUKURU, iwapo huwa yanafanyiwa kazi au kugeuzwa chanzo cha mapato yao binafsi. TAKUKURU Njombe imeoza, inanuka, Waziri mwenye dhamana atoke USINGIZINI sasa.
 
Shida iko huko TAKUKURU bosi, mtu akipeleke malalamiko wanaungana na MHALIFU kupiga hiyo pesa. Mfano ni hapa TAKUKURU Njombe, washenzi hawa wanakula milungula kama hawana akili vile. Haya MAGENGE ya CCM ni vyema katiba mpya ikayafutilia mbali.
Mkuu,

Nakubaliana na wewe kwamba katiba mpya inaweza kuleta mabadiliko mengi ya kimsingi yatakayotufaidisha.

Lakini, huoni kwamba kuna mengi tu ambayo hata kwenye katiba ya sasa yamo, lakini tunayasingizia katiba mpya?

Huoni kwamba tunakosa katiba mpya na utamaduni wa kufuatilia katiba unaotufanya tusisimamie hata yaliyomo katika katiba iliyopo tayari?

Huoni kwamba, kwa mtaji huu, watu watashindwa kuoa mke na kusingizia katiba mpya, wakati suala la kuoa mke limesharuhusiwa hata na katiba ya sasa?

Hii katiba mpya tunaifanya kichaka cha kufichia mapungufu yetu yote sasa?
 
Back
Top Bottom