ARUSHA: Askari Polisi 7 waliombambikia pembe za ndovu Prof. Justin Maeda na kuchukua milioni 100 wafukuzwa kazi, Profesa afunguka

ARUSHA: Askari Polisi 7 waliombambikia pembe za ndovu Prof. Justin Maeda na kuchukua milioni 100 wafukuzwa kazi, Profesa afunguka

Duh hao polisi walimgusa mtu ambaye hawakumjua, rof huyo lazima atakuwa na connection
Sasa polisi hao wamembambikia nyara hizo ili wamtemeshe pesa dah.

Ova
Mwez wa 12 Iringa Polis wamemfanyia jamaa yangu mmoja kitu kama hiki cha kihuni.

Almanusura Auze nyumba. Na mteja alikua anatafutwa. Sema connections kadhaa zikasaidia. Ila bado wako kazini. So sad yan
 
Mwez wa 12 Iringa Polis wamemfanyia jamaa yangu mmoja kitu kama hiki cha kihuni

Almanusura Auze nyumba. Na mteja alikua anatafutwa.....Sema connections kadhaa zikasaidia. Ila bado wako kazini. So sad yan
Kuna siku polisi walinikamata, wakawa wanataka kunibabatiza na kesi zao za kipuuzi.

Wakawa wanataka kunipeleka kituoni.

Nikasema sawa, si tatizo. Ngoja nimpigie simu mshua nimtaarifu mmenikamata watu nyumbani wapate habari nimekamatwa na polisi. Halafu mtawaeleza kosa langu ni lipi.

Wakaniuliza kwani mshua wako nani?

Nikawaambia mshua tu.Msijali.

Nikaona wanaanza kuogopa.

Wakang'ang'ania kumjua.

Nikawatajia.

Haraka sana wakaanza kujibaraguza basi nenda tu.

Nikasema hapa kama mtu hajulikani angelala polisi.

Siku nyingine tumekaa maskani Upanga.

Tunaona polisi kama 20 wametanda mtaani wanakuja.

Mimi nikawaambia madogo fulani tumekaa nao, nikasema hapa kama mtu hawezi kuongea nao hawa ajikate kabisa, hapa tunabaki wabishi tu.

Basi wakafika mpaka pale tulipokuwa.

Mmoja akaanza kusema "hapa mnafanya nini nyie?".

Dah, kosa. Jamaa mmoja akamjibu "Hivyo ndivyo mlivyofundishwa kusalimia watu?"

Ikawa kama mzozo. Watu wakasema hapa tupo nyumbani.Polisi wakaanza kuuliza mmoja mmoja, wewe unakaa wapi? Watu wanaonesha nyumbani hapo, nyumbani hapo.

Wakamfikia jamaa mmoja tuko naye maskani.

Wewe unakaa wapi?

Jamaa akajibu "Kwa Ben".

Polisi wakawa wanashangaa, wakauliza, kwa Ben? Ben gani?

Jamaa akajibu, Ben Mkapa huyo huyo wa Jamhuri ya Muungano, kwani wewe unamjua Ben gani?

Hapo rais ni Ben Mkapa.

Askari wakastuka. Ikawa kama hawaamini.

Mmoja wao akawa kama anawanong'oneza, nikamsikia anasema "huyu namjua, nilikuwa namuona nyumbani kwa Mkapa pale Sea View kwenye lindo". Presumably wakati Mkapa akiwa Waziri.

Basi hapo hapo tukaona askari polisi walioanza kutuingia kwa inda wanabadilika mara moja.

Wakaanza kusema "mnajua wazee ni katika kufahamiana tu, hatukuwa na lengo baya, ni kufahamiana tu".

Nikasema hawa huko mitaa ya watu wasio na majina wanawakamata watu na kuwatoa upepo vizuri sana, bila kosa.

Bahati yao mbaya leo wamekutana na kisiki.

Ile maskani waliipigia alama kituoni kwao, waliambizana maskani hii msiguse, kuna mtoto wa rais anakaa hapo.

Haki ya kikatiba ya kila mtu ya kutosumbuliwa na kuchukuliwa hana hatia mpaka atakapopatikana na hatia inavurugwa na inakuwa privilege ya watu wenye majina.
 
Usa sio kama Tanga. Tanga ukiwaambia takukuru mambo yako wanamtafuta mlengwa na kula hela. Ukikutana na mlengwa anakuambia kila ulichosema huko. Jamani jamani Tanga eeeee Mungu waonee watu wako huruma. Japo mkuu wa takukuru alisimamishwa kazi lakini hakuna jipya sana. Hongereni takukuru huko Arumeru.
 
Duh hao polisi walimgusa mtu ambaye hawakumjua,Prof huyo lazima atakuwa na connection
Sasa polisi hao wamembambikia nyara hizo ili wamtemeshe pesa dah...

Ova
Keshakata Mpunga lkn sijui Kama zitarudi.
 
Kuna siku polisi walinikamata, wakawa wanataka kunibabatiza na kesi zao za kipuuzi.

Wakawa wanataka kunipeleka kituoni.

Nikasema sawa, si tatizo. Ngoja nimpigie simu mshua nimtaarifu mmenikamata watu nyumbani wapate habari nimekamatwa na polisi. Halafu mtawaeleza kosa langu ni lipi.

Wakaniuliza kwani mshua wako nani?

Nikawaambia mshua tu.Msijali.

Nikaona wanaanza kuogopa.

Wakang'ang'ania kumjua.

Nikawatajia.

Haraka sana wakaanza kujibaraguza basi nenda tu.

Nikasema hapa kama mtu hajulikani angelala polisi.

Siku nyingine tumekaa maskani Upanga.

Tunaona polisi kama 20 wametanda mtaani wanakuja.

Mimi nikawaambia madogo fulani tumekaa nao, nikasema hapa kama mtu hawezi kuongea nao hawa ajikate kabisa, hapa tunabaki wabishi tu.

Basi wakafika mpaka pale tulipokuwa.

Mmoja akaanza kusema "hapa mnafanya nini nyie?".

Dah, kosa. Jamaa mmoja akamjibu "Hivyo ndivyo mlivyofundishwa kusalimia watu?"

Ikawa kama mzozo. Watu wakasema hapa tupo nyumbani.Polisi wakaanza kuuliza mmoja mmoja, wewe unakaa wapi? Watu wanaonesha nyumbani hapo, nyumbani hapo.

Wakamfikia jamaa mmoja tuko naye maskani.

Wewe unakaa wapi?

Jamaa akajibu "Kwa Ben".

Polisi wakawa wanashangaa, wakauliza, kwa Ben? Ben gani?

Jamaa akajibu, Ben Mkapa huyo huyo wa Jamhuri ya Muungano, kwani wewe unamjua Ben gani?

Hapo rais ni Ben Mkapa.

Askari wakastuka. Ikawa kama hawaamini.

Mmoja wao akawa kama anawanong'oneza, nikamsikia anasema "huyu namjua, nilikuwa namuona nyumbani kwa Mkapa pale Sea View kwenye lindo". Presumably wakati Mkapa akiwa Waziri.

Basi hapo hapo tukaona askari polisi walioanza kutuingia kwa inda wanabadilika mara moja.

Wakaanza kusema "mnajua wazee ni katika kufahamiana tu, hatukuwa na lengo baya, ni kufahamiana tu".

Nikasema hawa huko mitaa ya watu wasio na majina wanawakamata watu na kuwatoa upepo vizuri sana, bila kosa.

Bahati yao mbaya leo wamekutana na kisiki.

Ile maskani waliipigia alama kituoni kwao, waliambizana maskani hii msiguse, kuna mtoto wa rais anakaa hapo.

Haki ya kikatiba ya kila mtu ya kutosumbuliwa na kuchukuliwa hana hatia mpaka atakapopatikana na hatia inavurugwa na inakuwa privilege ya watu wenye majina.
Askari wa bongo njaa kali sana. Kuna siku wamenikuta maskani moja hivi usiku wakanidaka na kunipa kesi ya bangi.

Walianza kuniswaga kuelekea kituoni nikasema sawa twendeni, kituo hakikuwa mbali sana tukaanza kuelekea. Meter kama 200 kutoka kituoni ndio wakaanza kuniuliza nina shilingi ngapi waniachie nikawaambia sina hata mia, wananiambia weka simu bondi hapo dukani sisi tuchukue elfu hamsini nikakataa.

Wakasema wewe utalala sero leo na kesho asubuhi unaenda central nikawaambia poa. Tumekaribia kituoni wanaona sijalainika nikasikia "mfungue pingu mseng.e huyo aondoke zake".
 
Kwa wasiomjua huyu prof. Lile ghorofa pale Leganga ambako TRA wamepanga,NSSF etc ndio la huyo dingi.

Na lile jengo ambako Meru Community bank walikua wamepanga ni la mdogo wake huyo Prof.(ambako ndipo alipoenda kuomba hio mil 30 iliyopelea kwny ile rushwa ya mil 100).
Kwa sasa hivi polisi wakijua una hela wanakutungia kesi, TRA wakijua una hela wanakubambikia kodi.

Labda huyo rais mpya awafunge speed gavana na raia wamsaidie.
 
Back
Top Bottom