KERO Arusha: Barabara ya Lamara ni mbovu kwa muda mrefu sana, Wanasiasa kila mara wanaitumia kwenye kampeni bila kuitengeneza

KERO Arusha: Barabara ya Lamara ni mbovu kwa muda mrefu sana, Wanasiasa kila mara wanaitumia kwenye kampeni bila kuitengeneza

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Barabara ya Lemara imekuwa katika hali mbaya kwa muda mrefu, licha ya kuwa kila kipindi cha uchaguzi baadhi ya wagombea wa udiwani wamekuwa wakiitumia kama sehemu ya kampeni na kuahidi kuiboresha. Hata hivyo, hadi sasa hakuna hatua za maana zilizochukuliwa kuboresha barabara hiyo.

Mara kwa mara barabara hiyo hupaluliwa bila kushindiliwa ipasavyo, hali inayosababisha mashimo na kuharibika tena kwa muda mfupi. Hii imekuwa kero kubwa kwa wakazi wa Kata ya Lemara, hasa ikizingatiwa kuwa barabara hiyo inaunganisha maeneo muhimu kama Viwanja vya Nane Nane, Hospitali ya Jiji, Engosheraton, Njiro Road na njia ya Bypass kuelekea Moshi.

Changamoto ya Usafiri​

Ubovu wa barabara umeathiri pia usafiri wa umma. Bajaji zimechukua nafasi kubwa ya daladala, na kuanzia saa 1:00 jioni nauli hupanda kutoka Sh1,000 hadi Sh1,500 au hata Sh2,000. Hali hii inawaongezea wananchi gharama za usafiri, hasa nyakati za jioni.

Kwa ujumla, baadhi ya kata zinazopakana na Lemara, kama Unga Limited na Muriet, zimeendelea kwa kasi na zina miundombinu bora zaidi, ikiwemo barabara za lami.

Lemara ni eneo muhimu, hasa wakati wa maonesho ya Nane Nane ambapo barabara hii hutumika na watu wengi. Aidha, kwa kuwa Njiro Road huwa na foleni kubwa, barabara ya Lemara inaweza kuwa njia mbadala muhimu kwa wananchi na watumiaji wengine.

Tunaomba viongozi husika kuacha kutumia changamoto hii kama agenda ya kisiasa wakati wa uchaguzi na badala yake kuchukua hatua za kweli za kuiboresha. Wananchi wanahitaji kuona maendeleo na uwajibikaji, si ahadi pekee.

Lengo la kuwasilisha malalamiko haya ni kuhakikisha changamoto za wakazi wa Lemara zinafahamika na viongozi wanawajibika kuchukua hatua.

IMG_20260813_183054_552.jpg




 
Andiko jema la kuhimizana maendeleo na mabadiliko.Ila,mleta uzi,mara nyingine ungeanza na kuainisha eneo moja kwa moja.Siyo kulificha mbali kwenye maelezo ili msomaji ajenge picha ya awali kabla hajachoka kulitafuta.
 
Back
Top Bottom