Arusha: Binti adai kuvuliwa nguo na kuchomwa na pasi na mwajiri wake

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
BINTI ATOKA KIGOMA ADAI KUVULIWA NGUO NA KUCHOMWA PASI YA MOTO NA MWAJIRI WAKE ARUSHA

Binti anayetokea mkoani Kigoma amedai kufanyiwa ukatili mkubwa na mwajiri wake, Nema Mushi, mkazi wa Moshono jijini Arusha, akisema alivuliwa nguo, akaachwa akiwa uchi na kisha kuchomwa kwa pasi ya moto sehemu mbalimbali za mwili.Akizungumza na Kusaga TV, binti huyo amesema tukio hilo lilitokea baada ya kurudi nyumbani kutoka kazini, ambapo mwajiri wake alianza kumpiga, akamvua nguo zote na baadaye akachukua pasi ya moto iliyokuwa imechomolewa kwenye umeme na kuanza kumchoma mwilini akiwa sebuleni.

Pia amedai kuwa kabla ya tukio hilo, mume wa mwajiri wake aliwahi kutaka kumbaka lakini alikataa na kutoa taarifa kwa mama yake. Aidha, amesema katika kipindi cha mwaka mmoja alioishi na kufanya kazi kwa mwajiri huyo alikuwa akipigwa mara kwa mara bila kufahamishwa kosa lake.Kwa upande wake, Nema Mushi amekanusha tuhuma hizo, akisema hajawahi kumvua nguo wala kumchoma mfanyakazi wake kwa pasi ya moto kama inavyodaiwa.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi limemkamata Nema Mushi na linaendelea na hatua za kisheria kufuatia tuhuma zinazomkabili za kudaiwa kumfanyia binti huyo vitendo vya ukatili na unyanyasaji wakati uchunguzi ukiendelea.

Pia soma: Mwajiri wa Binti aliyedai kuchomwa na pasi akanusha kutenda kosa hilo, adai yeye alimchapa tu
 
Picha
 
Huyo binti hawezi kutunga uwango kama huo wa pasi ya moto tena imetoka kwenye umeme. Huo ni ukatili wa hali ya juu. Mtoto wa mwenzio unamgeuza nguo iliyojikunja kunja sasa unainyoosha kwa pasi ya umeme!. Dunia sio mbaya ila walimwengu ndo wabaya.
 
Kuna watu ni wakatili sana, sio ajabu ukashangaa huyo aliyefanya huo ukatili jumapili anaendaga kanisani, na anatoa sadaka ya ahadi
 
Back
Top Bottom