Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Kwa mara nyingine tena daladala zote zinazoenda katikati ya jiji. zimegoma kufanya biashara ikiwa ni mgomo wa pili ndani ya kipindi kisichozidi mwezi na nusu.
Mussa njuga ambae ni katibu wa daladala amesema mgomo huo hauna kikomo hadi wapate kauli kutoka kwa waziri Mkuu au Makamu wa Rais.
Sababu za mgomo huo inatajwa ni Serikali kushindwa kufikia muafaka kati yao na Bajaji kwa kuruhusu Bajaji kufanya kazi kama daladala ndani ya Jiji la Arusha
Uongozi huo umeeleza kuwa mbali na kuandika barua kwa mkuu wa mkoa kuikumbusha Serikali kutekeleza maadhimio ya vikao vya kamati ya suluhu lakini barua hiyo haikupatiwa majibu jambo ambalo limewakatisha tamaa madereva na viongozi wao.
Aidha viongozi hao wanataka kauli kutoka kwa waziri Mkuu Au makamu wa Rais kwa madai kuwa viongozi wa Arusha wameshindwa kutekeleza madai yao.
Zaidi ya Bajaji 2500 zinafanya kazi ndani ya jiji la Arusha kama daladala.
=============
LATRA YASEMA MGOMO UKIENDELEA WATAFUTA LESENI ZA DALADALA
Joseph Michael, Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Mkoa wa Manyara anazungumzia kinachoendelea:
Tunasikitika kitendo cha Daladala kufanya mgomo kwa kuwa tayari Serikali inafanyia kazi suala hilo chini ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye alishaunda Kamati inayohusisha watu wa Bodaboda, Daladala, Bajaj, Barabara na taasisi za Serikali zinazohusisha masuala ya Usafirishaji.
Kamati iliundwa maalum kufuatilia suala hilo na ilishamaliza kazi yake, kilichokuwa kinafuata ni kwenda kwenye hatua ya pili ya utekelezaji, kinachoshangaza wamefanya mgomo wakati wao watu wa Daladala wana wawakilishi wao kwenye Kamati.
Tunashauri warejee kutoa huduma na Kamati iendelee kutoa mchakatoa, mgomo una madhara, waliendelea hivyo Sheria inaeleza kuwa tutafuta leseni.
Nimeenda kuzungumza nao watu wa Daladala pale Kilombero Kituoni, inavyoonekana Wanachama wa Daladala hawawaheshimu viongozi wao wanaowawakilisha, kwenye umoja wao huo kuna shida.
Pia tumeruhusu Coaster za Arusha – Moshi zianze kufanya kazi wakati huu wa mgomo huku tukiwasisitiza watu wa Daladala wasitishe mgomo, wafuate Sheria na Taratibu kwa kuwa wakiendelea hivyo tutafuta leseni zao, tupo ‘serious katika hilo.