Arusha: Dereva wa Serikali aenda na maiti bar

Arusha: Dereva wa Serikali aenda na maiti bar

Hii story imekaa kichochezi sana yaani nimesafiri misiba kadhaa mnasafiri wee mkifka mahali mna pose kidogo kunyoosha miguu Wa kunywa anakunywa Wa kula anakula then mnaendelea na safari au hii aipo hivyo
 
uzi umekaa kichochezi sana huu, unataka kuniambia wale wanaosafirisha maiti wanaojazana pale korogwe na mombo kwenye hoteki kula wanafanya makosa? hao kina mama wanaolia wako wapi, nani alisema watu waliokuwa wanasafiri hawana uwezo walipewa gari bure? kuna mambo mengi sana hapa ya kujiuliza.
 
Mi ndio huyo dereva nilienda kula mlitaka nile harakaharaka nipaliwe? Au wakati na kula ni kosa kuangakia kinachoendelea kwenye luninga.siku nyingine siwapi lifti

Sent from my Infinix X6517 using JamiiForums mobile app
 
Kuna raia zimepinda aisee dah!

Hii nguruwe ni ya kufukuza kazi straight away yaani na hakika tunahitaji sana adhabu ya viboko irudi kwenye jamii
Mjerumani aliwahi sana kuondoka
 
Cha kushangaza dereva amekuja na maiti hapa Sakina bar, amepaki gari, akawashusha ndugu wa marehemu kisha akaingia ndani kutizama EPL. Nimeumia sana kuona wamama wako nje wanalia

Weka na picha ya ndugu wa marehemu, hao wamama waliokuwa wakilia...
 
Na Malisa GJ

Habari kaka.

Kuna tukio limetokea hapa Arusha usiku huu limenisikitisha sana. Kuna Familia imepata msiba, wanatakiwa kusafirisha kwenda wilayani kuzika lakini hawana uwezo. Hivyo wameomba msaada wa gari ya serikali kusafirisha maiti. Gari hiyo imebeba maiti na ndugu wachache wa marehemu.

Cha kushangaza dereva amekuja na maiti hapa Sakina bar, amepaki gari, akawashusha ndugu wa marehemu kisha akaingia ndani kutizama EPL. Nimeumia sana kuona wamama wako nje wanalia, jamaa yuko ndani anakunywa na kuangalia game. Hakika umaskini ni mbaya sana. Naomba upaze sauti ili serikali iweze kuchukua hatua kwa kitendo hiki cha kinyama na kisicho cha utu.

Binadamu wote wana haki ya kulindiwa utu wao. Umaskini usiwe sababu ya kudhalilisha wengine. Huyu dereva angekua amefiwa na baba yake mzazi, angediriki kwenda kumuanika bar halafu aangalie mpira? Namba za gari ni STM 3708. Tunaomba serikali ichukue hatua kali kwa dereva na wote waliohusika. Huu ni udhalilishaji mkubwa wa utu.


View attachment 2788969View attachment 2788971
Ccm hoyee! Mpaka dereca wao wamejaa kiburi na dharau dhidi ya utu!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Kuna raia zimepinda aisee dah!

Hii nguruwe ni ya kufukuza kazi straight away yaani na hakika tunahitaji sana adhabu ya viboko irudi kwenye jamii
Naunga mkono hoja hizi nidharau zilizokithiri
 
Back
Top Bottom