Moisemusajiografii
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 43,960
- 77,533
Stupid!Huna adabu.Asa jaman mtu si amekufa huyo , ukweli ni kuwa mazishi yasingefanyika usku , jamaa kaona hii sa moja na nusu achek game mana atafika tuu mda mwafaka , imekuwa nongwa duuh
Magari mengi toka Dar kwenda ma Maiti Moshi hupaki Mombo mbele ya zile baa na waombolezaji hushuka kwenda kutandika pombe kwenye baa kabla ya kuendelea na safariDah kwakwel huu ni udhalilishaji aswaaa
Mjerumani aliwahi sana kuondokaKuna raia zimepinda aisee dah!
Hii nguruwe ni ya kufukuza kazi straight away yaani na hakika tunahitaji sana adhabu ya viboko irudi kwenye jamii
Cha kushangaza dereva amekuja na maiti hapa Sakina bar, amepaki gari, akawashusha ndugu wa marehemu kisha akaingia ndani kutizama EPL. Nimeumia sana kuona wamama wako nje wanalia
Ccm hoyee! Mpaka dereca wao wamejaa kiburi na dharau dhidi ya utu!Na Malisa GJ
Habari kaka.
Kuna tukio limetokea hapa Arusha usiku huu limenisikitisha sana. Kuna Familia imepata msiba, wanatakiwa kusafirisha kwenda wilayani kuzika lakini hawana uwezo. Hivyo wameomba msaada wa gari ya serikali kusafirisha maiti. Gari hiyo imebeba maiti na ndugu wachache wa marehemu.
Cha kushangaza dereva amekuja na maiti hapa Sakina bar, amepaki gari, akawashusha ndugu wa marehemu kisha akaingia ndani kutizama EPL. Nimeumia sana kuona wamama wako nje wanalia, jamaa yuko ndani anakunywa na kuangalia game. Hakika umaskini ni mbaya sana. Naomba upaze sauti ili serikali iweze kuchukua hatua kwa kitendo hiki cha kinyama na kisicho cha utu.
Binadamu wote wana haki ya kulindiwa utu wao. Umaskini usiwe sababu ya kudhalilisha wengine. Huyu dereva angekua amefiwa na baba yake mzazi, angediriki kwenda kumuanika bar halafu aangalie mpira? Namba za gari ni STM 3708. Tunaomba serikali ichukue hatua kali kwa dereva na wote waliohusika. Huu ni udhalilishaji mkubwa wa utu.
View attachment 2788969View attachment 2788971
Naunga mkono hoja hizi nidharau zilizokithiriKuna raia zimepinda aisee dah!
Hii nguruwe ni ya kufukuza kazi straight away yaani na hakika tunahitaji sana adhabu ya viboko irudi kwenye jamii