Arusha: Hakimu Benson Ngowi(32) anashikiliwa na Polisi kwa kosa la kumlawiti kijana mwenye umri wa miaka 29


Huenda hii ni Mikasa itokanayo na Visasi.

Baada ya kufanya tafiti nyingi za kina kabisa kuhusiana na masuala ya mikasa kama hii, imebainika dhahiri kwamba kuna Mambo mengi sana ambayo huwa yapo yamejificha nyuma ya Kesi za namna hii. Kuna masuala ya Visasi kwenye masuala haya.

Mathalani, mwanzoni mwa miaka ya nyuma kati ya 2000 na 2009, Mwalimu mmoja wa Shule moja ya Sekondari (nisingependa kuitaja jina) alikuwa ana mahusiano na Mke wa DSO katika Wilaya hiyo aliyokuwepo huyo Mwalimu. Wakati huyo DSO alipopata taarifa hizi allisuka mipango kwa kushirikiana na baadhi ya Askari Polisi wasio waadilifu, walimbambika Kesi ya Uvakaji wa Mwanafunzi wake mmojawapo katika Shule aliyokuwa akifundisha. Yule Mwalimu alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, alikuja kutolewa baadaye Sana baada ya kushinda Kesi ya Rufaa Mahakama Kuu. Nakumbuka Hukumu ya Mhe. Jaji Mihayo ndiyo iliyomnusuru yule Mwalimu kutoka gerezani na kuachiwa huru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…