Arusha: Hukumu ya kesi inayomkabili Lengai Ole Sabaya imeahirishwa hadi Oktoba 15, 2021

Arusha: Hukumu ya kesi inayomkabili Lengai Ole Sabaya imeahirishwa hadi Oktoba 15, 2021

Nimesoma mahali kuwa huyu jamaa alikuwa na simu uisiku wa kuamkia leo!
Alipewa na nani?
Alikuwa akiongea na nani?
Nini malengo ya kupewa simu?
Kwanini kesi imeahirishwa?
Nini kipo nyuma ya pazia?
 
Mbona bashite yeye hakamatwi? Wakati alifanya unyama zaidi ya huyu!
 
Wanajukwaa nawasimu,

Hongereni kwa kuendelea kuchapa kazi na kulijenga Taifa letu.

Kama nitakuwa ninakumbuka vema, ilisemwa tarehe ya leo (1/10/2021) Ni siku ya hukumu ya Kesi ya Lengai Ole Sabaya ( Kesi ile ya mwanzo).

Je kumbukumbu zangu ziko sawa?.

=========

Mahakama ya hakimu mkazi Arusha inatarajia kutoa hukumu katika kesi ya Unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai ole sabaya na wenzake wawili.

Sabaya na wenzake wanatuhumiwa kutenda makosa hayo February 9 mwaka huu katika duka la Saad store linalomilikiwa na Mohamed Saad lililopo katikati ya jiji la Arusha wakidaiwa kuvamia na kupora wakitumia silaha.

Kesi hiyo iliendeshwa mfururizo takribani siku 35, mbele ya hakimu mkazi mwandamizi Odiro Amworo kutoka mkoani Geita, ambapo upande wa serikali uliwasilisha mashahidi 11 na vielelezo kadhaa, hivyo Leo kesi hiyo inatarajia kufikia tamati kwa kutoa hukumu kwa washtakiwa hao watatu .

Washtakiwa wengine wanaotarajiwa kuhukumiwa hapo kesho ni Silvester Nyegu na Daniel Mbula

2948393_FB_IMG_1628770975220.jpg


==========

UPDATE:
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imeahirisha kutoa hukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili.

Hukumu imeahirishwa hadi Oktoba 15, 2021


Hizi hukumu kuarishwa na kama vile wanasubiria maelekezo kutoka juu badala ya kesi yenyewe
 
Hawawezi kumfunga
Mbali na miaka 30 aliyokwisha kuipata, leo tena anapanda kizimbani kwa kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji pesa. Nadhani leo atapanda na suti yake mpya.
 
Mahakama; ewe jambazi jitetee

Sabaya; nina mchumba nimemlipia mahari naombeni mniachie nikapashe kiporo

Mahakama;..... Bwahahahaha 😁😁
 
Back
Top Bottom