Arusha: Jeshi la Polisi lasema linafuatilia tukio la msanii Dogo Janja kumjeruhi Mtu kwa kumpiga risasi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

​
Polisi wafanya Uchunguzi kuhusiana na tukio la mtu mmoja kujeruhiwa na risasi.

Jeshi la Polisi mkoani Arusha linafanya uchunguzi kuhusiana na tukio la mtu mmoja aitwaye Bakari Halifa Daud (18) mkazi wa Sombetini Jijini Arusha kujeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni.

Akitoa taarifa hiyo leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 23, 2025 muda wa saa 5:30 usiku huko katika maeneo ya Sombetini Jijini Arusha.
​
Kamanda Masejo ameendelea kufafanua kuwa wakati Abdulaziz Abubakari (30) mkazi wa Levolosi Jijini Arusha akiwa anashuka kwenye gari alidai kutaka kuvamiwa na Bakari Halifa akiwa na mwenzake kwa kutumia silaha ya jadi hali iliyopelekea kutumia silaha aliyokuwa nayo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watu wawili kuhusiana na tukio hilo ambapo limesema bado linaendelea na uchunguzi.
 
CCM

IHUYU DOGO AMECHAFUA CHAMA CHETU

HAFAI KUWA DIWANI PLS

MWONDOEN HARAKA
 
Maskini wakiingia CCM akili zinabadilika sasa dogo baada kujiona maisha kayapatia naona kuishika ccm na kuwtaka udiwani na mazingira aliyotokea anataka kujiona wakina nani.

Dogo janja video zipo ulizofanya
 
1KUNA TAARIFA ZIMEZAGAA MGOMBEA UDIWANI WA CCM
DDOGOJANJA AMEMPIGA RISASI MWANAFUNZI WA FORM 4 AKIMTUHUMU MWIZI

JESHI LA POLISI LIMEKIRI KUPOKEA HIO KESI NA LINAFWATILIA

TUNAOMBA CCM ARUSHA WAKATI UCHUNGUZI UKIENDELEA HUYU DOGO AONDOLEWE KABISA HAFAI KUGOMBEA HATA SERKL ZA MITAA

VYEMA TUKAMWACHIA HUU MSALA AMALIZANE NAO YEYE BINAFSI NA TUNAOMBA TUSIINGIZE SIASA KWENYE UCHUNGUZI

HILI JAMBO LUNAFWATILIWA KULIKO TUNAVYOLIJUA

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
KIDUMU DAIMA
5TENA
 
Sitaongea mengi lakini huyu Teja dogo janja ambaye ni kada wa CCM na amepitishwa kugombea udiwani huko Arusha ni kama ameanza kuwa na kiburi na kulewa Madaraka madogo ambayo anafikiri kuwa tayari anayo lakini kimsingi bado hajayapata,na hata akiyapata ni madogo sana siyo kwa sifa hizi.

Anapita mule mule kama vile wakubwa zake wanavyoteka na kuua watanganyika Kwa maslahi yao na yeye ameanza kutandika risasi watanganyika wenzake bila kujali lolote Wala yeyote.
Tazama video hapo chini.

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…