Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Arusha, Saipulani Ramsey, amekiri kuwa rushwa bado ni tatizo ndani ya chama hicho, akisema inasababisha kuchaguliwa kwa viongozi wasio bora wanaowadharau wananchi.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Jambo TV, Ramsey amesema baadhi ya wanachama wanaotangaza nia ya kugombea mapema kabla ya muda rasmi hufanya hivyo kwa sababu ya rushwa. Ameonya kuwa tabia hiyo inaweza kuwaondoa kabisa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi.
Ameongeza kuwa viongozi wanaopatikana kwa njia ya rushwa mara nyingi hawajali maslahi ya wananchi, hali inayosababisha malalamiko kutoka kwa wanachama na wananchi kwa ujumla.
Kauli hii inakuja huku Tanzania ikielekea kwenye uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka 2025.