Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Binti mmoja ajulikanae kwa jina la Hadija mwenye umri wa miaka 17 amefariki dunia baada ya kuchomwa visu kadhaa na kijana wa mwenye nyumba aliyofikia kufanya kazi.
Sababu za kijana huyo kufanya hivyo inaelezwa kuwa ni kijana huyo kutaka kumbaka binti huyo na ndipo yalipotokea kupishana kati yao.
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Nambere kata ya Sokoni 2 wilayani Arumeru.
Mama mwenye nyumba hiyo anasema alimleta hadija wiki iliyopita kuja kumsaidia kulea mtoto , na wakati tukio linatokea alikuwa yupo kazini. Anaendelea kusema binti huyo wa kazi ana muda wa wiki moja tu aje kutoka singida.
Mwenyekiti wa mtaa huo Samweli Laizer amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa walipoingia kwenye chumba cha kijana huyo walikuta damu zimetapakaa kila mahali hadi kwenye kuta za nyumba