Arusha: Lengai Ole Sabaya afikishwa Mahakamani kwa Uhujumu Uchumi, Utakatishaji Fedha

Arusha: Lengai Ole Sabaya afikishwa Mahakamani kwa Uhujumu Uchumi, Utakatishaji Fedha

Naona Mwana kamati wa kamati ya Kukoka moto majungu na fitina upo katika ubora wako
 
Mnaofanya utetezi wa Ole Sabaya kumbukeni hajakamatwa na kushtakiwa peke yake. Mabaunsa wake, vijana wenzake watano waliokuwa wanamlinda kikamilifu na kushirikiana naye katika kazi zake za kila siku nao wamekamatwa na kushtakiwa pamoja naye.Hao nao wanategemea utetezi wenu.

Chondechonde watetezi, msiwasahau hao vijana watano muhimu kwake Ole Sabaya ambao kwa pamoja waliweza kufanikisha mengi mkoani Kilimanjaro na Arusha.
Ni mwendo wa kusaga kunguni tu [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
DC (presidential appointee) ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya, ati anaajiri 'mabaunsa' wa kumlinda popote pale aendapo!

Akili zingine hizi hata mbayuwayu hanazo.

Nothing but criminal mentality.

-Kaveli-
 
Sasa ni dhahiri kuwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ameshtakiwa kwa makosa ya jinai. Amefikishwa Mahakamani huko Arusha na kusomewa mashtaka sita. Ninaandika hapa nikiamini kuwa mashtaka ya Ole Sabaya bado ni tuhuma tu hadi pale yatakapothibitishwa mahakamani kupitia ushahidi. Yaani, ukweli au la kuhusu mashtaka yake utapatikana mahakamani. Sitarajii tena Mkurugenzi wa Mashtaka kuwasilisha Hati ya Kutokuwa na Nia ya Kushtaki kama alivyofanya kwenye kesi ya Sabaya iliyopita (natania).

Kimsingi, makosa katika mashtaka yote dhidi ya Sabaya yanadaiwa kufanywa naye wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai. Hapa ndipo tafakari yangu inapoanzia. Bila hata ufahamu wa kisheria, inafahamika kuwa Mkuu wa Wilaya pamoja na mambo mwngine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika Wilaya yake. Ndiyo kusema, Mkuu wa Wilaya ndiye mlinzi kiongozi wa amani na utulivu katika Wilaya yake. Ndiye anayepaswa kuhakikisha kuwa wananchi wa Wilaya yake wanaishi kwa amani huku wakifanya shughuli zao za kimaendeleo katika kujitafutia mikate yao ya kila siku.

Haitarajiwi kuona Mkuu wa Wilaya 'akiwa kinara' wa uharibifu wa amani, utulivu na ustawi wa watu wake. Haitarajiwi pia kuona Mkuu wa Wilaya kutenda makosa ya jinai ambaye yeye mwenyewe ndiye anapambana nayo usiku na mchana ili wananchi wake wawe na amani, utulivu na ustawi. Haitarajiwi pia Mkuu wa Wilaya kutenda uhalifu ikizingatiwa pia yeye ni mwakilishi wa Rais katika Wilaya yake. Matendo yake na maneno yake yanawakilisha maono, maelekezo na taswira ya mamlaka yake ya uteuzi. HAIPENDEZI Mamlaka ya uteuzi kubeba taswira ya kijinai kwa wananchi kupitia kwa Mkuu wa Wilaya.

NI PICHA YA KUOGOFYA kuona Mkuu wa Wilaya akipokea rushwa; akitakatisha pesa; akiongoza genge la kihalifu na kadhalika. NI MAMBO YA KUTISHA kusikia au kushuhudia Mkuu wa Wilaya akikandamiza ustawi wa watu wake na kulinda kwa nguvu zake zote 'genge' lake. Tuhuma dhidi ya Sabaya zinatoa picha ya kujisahau au kujiachia kulikopitiliza kwa wateule. Au tuhuma hizo zinaonyesha jinsi tabia halisi ya mteule inapojianika pale ambapo kunapatikana nafasi ya kufanya chochote mahali popote. Mashtaka yote ni ya Arusha, bado ya mahali pengine ikiwemo Wilaya yake ya Hai. Inafikirisha sana.

Mashtaka ya Sabaya yawe funzo kwa Mamlaka ya Uteuzi. Yawe funzo katika vya kuzingatia kabla, wakati na baada ya uteuzi. Mamlaka ya uteuzi ina mikono mirefu. Ina vyombo mbalimbali vya kiuchunguzi na kiutafiti. Inafurahisha na kuleta imani na amani kwa wananchi kuona Mamlaka ya Uteuzi ikifanya kazi kubwa kuchuja wateule wake ili 'makandokando' kama ya Ole Sabaya yaepukwe. Hata kama mashtaka yote hayatathibitishwa mahakamani, kutuhumiwa tu kama kiongozi inatosha kuchafua picha ya mteule yeyote yule awaye. Kila jambo hutokea ili kutoa mafundisho kwa yajayo.
 
KING SABAYA under arrest...aisee siku zinakwenda kwa kasi mno !! Mzee wa GOLGOTA ndani ya 18 za Jamhuri duh!! huwezi amini mambo haya.
 
Ndugu, fahamu kwamba Sabaya ndiyo alikuwa main engine ya kumng'oa Mbowe pale Hai. Mbowe ni mwenyekiti wa chama chenye wafuasi wengi mitandaoni.
Hivyo basi Sabaya amekuwa adui na kuchukiwa na wengi sababu tu ya kumwangusha Mbowe. Hilo liliwauma sana CHADEMA na ndiyo maana wanamchukia Sabaya.
unamaanisha wate walioko hai ni chadema?
 
Dogo msibani pale uwanja wa uhuru alilia kilio fulani cha kutoka moyoni kabisa. Inaonekana alikuwa karibu sana na hayati na alipendwa.

Kile kilio ni cha maumivu ya kweli sio cha kujifanyisha.
 
Mwenye Majina ya Mawakili wote 'wanaomtetea' Ole Sabaya naomba aniwekee hapa tafadhali kwani Kesho naenda Kumtembelea 'Mtaalam' wangu wa ' Kipemba ' ili ikiwezekana wawe Vipofu au Wehu na ikiwezekana wawe Mashoga au sehemu zao za Siri Kupotea na Haja zao Ndogo na Kubwa watakuwa wanazitolea Midomoni na Masikioni mwao daima.

Na huyu 'Mtaalam' huwa hatanii kabisa.
 
Mwenye Majina ya Mawakili wote 'wanaomtetea' Ole Sabaya naomba aniwekee hapa tafadhali kwani Kesho naenda Kumtembelea 'Mtaalam' wangu wa ' Kipemba ' ili ikiwezekana wawe Vipofu au Wehu na ikiwezekana wawe Mashoga au sehemu zao za Siri Kupotea na Haja zao Ndogo na Kubwa watakuwa wanazitolea Midomoni na Masikioni mwao daima.

Na huyu 'Mtaalam' huwa hatanii kabisa.
Tupo pamoja boss
 
Labda hao mawakili watakuwa siyo wa Tanzania hii,labda ni wakenya au Uganda
 
Hatuko tayari kuona wazalendo wa nchi yetu wakinyanyaswa na wauza madawa ya kulevya.

Tunaanza kampeni rasmi ya kumchangia na kumuwekea wakili Sabaya kwenye kesi yake. Kama msaliti wa nchi mzee wa MIGA aliweza kuchangiwa, sisi kama Watanzania wazalendo hatuwezi kushindwa kumchangia Sabaya ambaye kwa uzalendo wake aliitoa wilaya ya Hai kutoka ya 63 kwenye ulipaji kodi hadi ikawa ya 4 kitaifa.

Hatuwezi kuhukumu watu kwa kusikiliza upande mmoja wa wanafiki Chadema ambao hawana jema kwa nchi yetu.

Chadema kila kitu wanapinga na kuponda, walipinga ndege, bwawa la umeme, elimu bure, ujenzi wa viwanda kila kitu wao ni kupinga tu, Ndege zilipokamatwa walishangilia.

Ndiyo tuwasikilize? Hapana.

#Justice for SABAYA
#Free SABAYA
 
Mwenye Majina ya Mawakili wote 'wanaomtetea' Ole Sabaya naomba aniwekee hapa tafadhali kwani Kesho naenda Kumtembelea 'Mtaalam' wangu wa ' Kipemba ' ili ikiwezekana wawe Vipofu au Wehu na ikiwezekana wawe Mashoga au sehemu zao za Siri Kupotea na Haja zao Ndogo na Kubwa watakuwa wanazitolea Midomoni na Masikioni mwao daima.

Na huyu 'Mtaalam' huwa hatanii kabisa.
Kila mtu ana haki ya kutetewa kisheria, la sivyo wangeshaingizwa gerezani.
Mawakili ni wajibu wao kutetea yeyote aliyewaajiri, wanaoshitaki waioneshe na kuishawishi mahakama kosa ili haki ya kila upande ipatikane.
 
Back
Top Bottom