Arusha: Lengai Ole Sabaya afikishwa Mahakamani kwa Uhujumu Uchumi, Utakatishaji Fedha

Arusha: Lengai Ole Sabaya afikishwa Mahakamani kwa Uhujumu Uchumi, Utakatishaji Fedha

Kamati nzima ya ulinzi na usalama ya ya wilaya ya Hai inatakiwa nayo iwajibishwe inakuaje Sabaya anatenda uhalifu nayo ipo inamuangalie tu ikiwemo kumpa hadi askari.Inatakiwa wakuu wa vyombo vyote wilaya ya Hai kuanzia Jwtz, polisi, Uhamiaji,TRA, usalama wa taifa na vyombo vyoote wawajibishwe ikiwemo kushushwa vyeo kwa kumpa sabaya ushirikiano kutenda uhalifu.
Alikuwa anazunguka na maaskari au vyombo vingine mfano maafisa TRA hali sio Kazi yake na wakuu wa vyombo vya ulinzi wapo tu wanamuangalia tu.Asiwajibishwe pekee yake ni kumuonea wawajibishwe na wakuu wa vyombo vyote vya ulinzi alivyoshirikiana navyo.
 
sabaya aliishalala mahabusu kabla ya kuwa DC,msiwe vilaza namna hii.

yaani ccm inaanua ijipigie wapi sawa tu,maana ina watazamaji mazezeta fulani hivi.
Nakuona nyumba ndogo ya sabaya,
Kibaya zaidi we Ni dume lakini si ridhiki.
 
UTU na sio CHEO,kwa minadhiri hiyo na yeye ni mmoja wa walinajisi utu wa wengine,ni sawa tu na yeye UTU wake ukinajisiwa.
Kwa kifupi serikali aitakiwi kuwa na tabia za kusutana, kumuonyesha kiongozi kwa namna hiyo ni kama inashabikia ushambenga huku wakijua Sabaya katika nafasi yake alijitengezea maadui wengi kwa sababu mbalimbali (zingine hizo hasira za watu wana haki nazo).

Kitendo cha kumshitaki ni salamu tosha kwa wengine kuna kesho, ila kudhalilishana ni unnecessary.

Asilimia kubwa ya post za humu ni moja sababu mahususi kwanini mtuhumiwa apewe walau heshima au kama atakutwa katika hali ya udhaifu iwe kwa bahati mbaya.

Lakini kitendo cha serikali yenyewe kutengeneza mazingira ya kudhalilisha mahabusu ambae alikuwa kiongozi na katika muda wake wa uongozi ametengeneza maadui wa kisiasa ni unethical to say the least.

Anyway huo ndio mtazamo wangu ata angekuwa ameshitakiwa Mbowe, ningetaka apewe heshima yake sio kumuweka kwenye mazingira ambayo baadhi ya wana CCM watumie picha kumdhalilisha.

Baada ya kusema hayo simlazimishi mtu kukubaliana na mtazamo wangu, maana kuna mijitu imeshaanza kunitukana khaa, kwani watu atuwezi pishana mitazamo bila ya matusi. Mijitu mengine sijui ikoje.
 
Instagram_post_by_Governor_Kaduma_•_Jun_4,_2021_at_12:40pm_UTC%22_.jpg
 
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne, leo Ijumaa, wako mahabusu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha akiwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi.

Bado haijafahamika mashitaka yanayomkabili

Pia soma
1) Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

2) Ole Sabaya akamatwa pamoja na mabaunsa wake. Ahojiwa na Vyombo vya Dola

View attachment 1807936
Ole Sabaya akitoka kwenye gari la Polisi akiwa kafungwa PINGU

View attachment 1807996
Ole Sabaya akiwa amechuchumaa mbele ya Mahakama
Instagram_post_by_Governor_Kaduma_•_Jun_4,_2021_at_12:40pm_UTC%22_.jpg
 
Kamati nzima ya ulinzi na usalama ya ya wilaya ya Hai inatakiwa nayo iwajibishwe inakuaje Sabaya anatenda uhalifu nayo ipo inamuangalie tu ikiwemo kumpa hadi askari.Inatakiwa wakuu wa vyombo vyote wilaya ya Hai kuanzia Jwtz, polisi, Uhamiaji,TRA, usalama wa taifa na vyombo vyoote wawajibishwe ikiwemo kushushwa vyeo kwa kumpa sabaya ushirikiano kutenda uhalifu.
Alikuwa anazunguka na maaskari au vyombo vingine mfano maafisa TRA hali sio Kazi yake na wakuu wa vyombo vya ulinzi wapo tu wanamuangalia tu.Asiwajibishwe pekee yake ni kumuonea wawajibishwe na wakuu wa vyombo vyote vya ulinzi alivyoshirikiana navyo.
Toa neno kumuonea hapo tafadhali. Sema tu wawajibishwe wote ila usirudie kusema ni kumuonea yeye kama yeye. Hata hivyo yeye si ndio mwenyekiti wa kamati hiyo ya ulinzi na usalama?
 
Mashtaka 4
1. Matumizi mabaya ya ofisi.
2. Uhujumu uchumi.
3. Unyang'anyi wa kutumia silaha.
4. Rushwa.
 
Toa neno kumuonea hapo tafadhali. Sema tu wawajibishwe wote ila usirudie kusema ni kumuonea yeye kama yeye. Hata hivyo yeye si ndio mwenyekiti wa kamati hiyo ya ulinzi na usalama?
Mnakosea kuwaingiza watu wengine kwenye kesi ya sabaya yani huyu alikjikuta Mungu mtu sana hata Mkuu wa mkoa alikuwa hapatani nae so kila mtu atalipwa kadiri ya kipimo chake kamwe usiwabebeshe wengine mzigo labda kama nawao walihusika kama mabody guard wake
 
2797548_Tutamtoa_Mkoloni_Mweusi_Soon_freedom_fighter_2025_posted_on_Instagram__Jun_4_2021_at_1...jpg


Bado wako wengi waliokuwa viongozi wa aina ya Ole Lengai Sabaya...

Ni aidha waadhibiwe kwa "natural death" kama Mwendazake au gereza likawafundishe namna ya kuwa watu bora na wenye manufaa ktk jamii..

Mwisho, hili ni swali la chemsha bongo tu...

Kati ya hawa waliochutama kichura, Ole Lengai Sabaya ni yupi? Je, ni wa kushoto kwako msomaji au kulia kwako....?

".......usilopenda kutendewa, basi vivyo hivyo wewe pia usimtendee mwenzako jambo hilo........"

Sasa tumuulize swali hili: Unalilia nini sasa Sabaya...??
 
Kwa muda sasa nimekuwa nikisikia tuhuma mbalimbali zikielekezwa kwa huyu mtu anayeitwa Ole Sabaya — Mkuu wa Wilaya ya Hai (by then).

Sijui ni ugoigoi wangu huu ama elimu duni niliyonayo inayonifanya nisielewe hasa kiini cha jinamizi linalomuandama huyu mtu?

Mwanzoni, nilikuwa namfahamu sabaya kama Kijana jasiri, shupavu, anayejiamini, na aliyefanya kazi chini ya falsafa madhubuti za Rais Magufuli za uchapa kazi na uwajibishaji wa mafisadi yaliyoitafuna nchi hii.

Kwa kadiri ya vyombo vya habari vilivyomripoti, alikuwa anaonekana ni kiongozi anayeshughulikia ujambazi kwa wakati mwingi - eg, ukamataji wa madawa ya kulevya, mabangi, fedha bandia nk...

Zaidi ya yote, alionekana ni kiongozi aliyehusika kwa kiwango kikubwa kukipaisha chama cha mapinduzi na kukiweka kwenye chati, huku akiwashughulikia wapinzani kwa namna za hapa na pale.

Hivi karibuni, baada ya Rais Magufuli Kufariki dunia, huyu Kijana amekuwa akizongwa na majinamizi yaliyoibuka kutoka pasipojulikana.

Kuna wale majasusi wa twitter (wenyewe wanaitwa Twirrah) ndio walikuwa vinara wa kuibua shutuma na tuhuma za kila aina dhidi yake.

Ukiachana na hawa majasusi uchwara wa twirrah, kulikuwa na jopo kubwa la multiple ID's Jamiiforums na kwenye mitandao mingine ambazo zilikuwa zinamuandama mpaka hapo aliposimamishwa kazi na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Hizi tuhuma za mitandaoni, kwa bahati mbaya, hazina ithibati yoyote.

Mimi binafsi huwa napenda kufuatilia mambo na kujiridhisha pasipo shaka kuhusu ukweli na uhalali wake. Sipendi kurukia rukia tu habari.

Kuna majasusi wengine kutoka twirrah wanasema sabaya kabaka wanawake mia mbili. Wengine wanasema sijui kalawiti makada wa chadema.

Stori zimekuwa nyingi sana bila ushahidi kuwekwa hadharani. Kila mtu anaibuka na lake.

Zamani nilisikia pia hata humu kuna majasusi (wanaitwa sijui TISS?) — Ningefurahi kama wangetujuza kwa hakika kuhusu tatizo alilonalo huyu mtu wa kuitwa Sabaya.

Kwa sisi wenye akili duni zisizoweza kuchambua mambo kwa ufasaha tumebaki kwenye mshangao bila kuelewa ni nini hasa tatizo!

Tunaangalia tu huko twirrah kila mtu anasema lake.
 
Back
Top Bottom