Kwa muda sasa nimekuwa nikisikia tuhuma mbalimbali zikielekezwa kwa huyu mtu anayeitwa Ole Sabaya — Mkuu wa Wilaya ya Hai (by then).
Sijui ni ugoigoi wangu huu ama elimu duni niliyonayo inayonifanya nisielewe hasa kiini cha jinamizi linalomuandama huyu mtu?
Mwanzoni, nilikuwa namfahamu sabaya kama Kijana jasiri, shupavu, anayejiamini, na aliyefanya kazi chini ya falsafa madhubuti za Rais Magufuli za uchapa kazi na uwajibishaji wa mafisadi yaliyoitafuna nchi hii.
Kwa kadiri ya vyombo vya habari vilivyomripoti, alikuwa anaonekana ni kiongozi anayeshughulikia ujambazi kwa wakati mwingi - eg, ukamataji wa madawa ya kulevya, mabangi, fedha bandia nk...
Zaidi ya yote, alionekana ni kiongozi aliyehusika kwa kiwango kikubwa kukipaisha chama cha mapinduzi na kukiweka kwenye chati, huku akiwashughulikia wapinzani kwa namna za hapa na pale.
Hivi karibuni, baada ya Rais Magufuli Kufariki dunia, huyu Kijana amekuwa akizongwa na majinamizi yaliyoibuka kutoka pasipojulikana.
Kuna wale majasusi wa twitter (wenyewe wanaitwa Twirrah) ndio walikuwa vinara wa kuibua shutuma na tuhuma za kila aina dhidi yake.
Ukiachana na hawa majasusi uchwara wa twirrah, kulikuwa na jopo kubwa la multiple ID's Jamiiforums na kwenye mitandao mingine ambazo zilikuwa zinamuandama mpaka hapo aliposimamishwa kazi na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Hizi tuhuma za mitandaoni, kwa bahati mbaya, hazina ithibati yoyote.
Mimi binafsi huwa napenda kufuatilia mambo na kujiridhisha pasipo shaka kuhusu ukweli na uhalali wake. Sipendi kurukia rukia tu habari.
Kuna majasusi wengine kutoka twirrah wanasema sabaya kabaka wanawake mia mbili. Wengine wanasema sijui kalawiti makada wa chadema.
Stori zimekuwa nyingi sana bila ushahidi kuwekwa hadharani. Kila mtu anaibuka na lake.
Zamani nilisikia pia hata humu kuna majasusi (wanaitwa sijui TISS?) — Ningefurahi kama wangetujuza kwa hakika kuhusu tatizo alilonalo huyu mtu wa kuitwa Sabaya.
Kwa sisi wenye akili duni zisizoweza kuchambua mambo kwa ufasaha tumebaki kwenye mshangao bila kuelewa ni nini hasa tatizo!
Tunaangalia tu huko twirrah kila mtu anasema lake.