Exogenous Factor
JF-Expert Member
- Nov 22, 2015
- 1,401
- 2,336
Mkuu unapendekeza kuwa na "treatment" tofauti kati ya wananchi wa kawaida ambao ni wahalifu na wale waharifu waliokuwa viongozi!? Na kama jibu ni ndio,basi ungependekeza huo utofauti mipaka yake iwe wapi!? ( Namaanisha ni wapi na hao waliowahi kushika madaraka watendewe sawa na walala hoi)
Kwa kifupi serikali aitakiwi kuwa na tabia za kusutana, kumuonyesha kiongozi kwa namna hiyo ni kama inashabikia ushambenga huku wakijua Sabaya katika nafasi yake alijitengezea maadui wengi kwa sababu mbalimbali (zingine hizo hasira za watu wana haki nazo).
Kitendo cha kumshitaki ni salamu tosha kwa wengine kuna kesho, ila kudhalilishana ni unnecessary.
Asilimia kubwa ya post za humu ni moja sababu mahususi kwanini mtuhumiwa apewe walau heshima au kama atakutwa katika hali ya udhaifu iwe kwa bahati mbaya.
Lakini kitendo cha serikali yenyewe kutengeneza mazingira ya kudhalilisha mahabusu ambae alikuwa kiongozi na katika muda wake wa uongozi ametengeneza maadui wa kisiasa ni unethical to say the least.
Anyway huo ndio mtazamo wangu ata angekuwa ameshitakiwa Mbowe, ningetaka apewe heshima yake sio kumuweka kwenye mazingira ambayo baadhi ya wana CCM watumie picha kumdhalilisha.
Baada ya kusema hayo simlazimishi mtu kukubaliana na mtazamo wangu, maana kuna mijitu imeshaanza kunitukana khaa, kwani watu atuwezi pishana mitazamo bila ya matusi. Mijitu mengine sijui ikoje.